Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Waislamu, Kuvunjwa kwa Khilafah, Ngao Yetu, ni Ukumbusho Mchungu wa Haja ya Haraka ya Kuisimamisha tena

(Imetafsiriwa)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alifikisha kwa Ummah wake kwamba,

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika, Imam (Khalifa) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake.” (Muslim).

Enyi Waislamu, tusemeje kuhusu kupotea kwa ngao yetu, Khilafah, mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na tarehe 3 Machi 1924 M?!

Baada ya kuvunjwa Khilafah yetu yenye kuunganisha, wakoloni wa Magharibi hawakuacha katika karne zao za uadui wa kikruseda.

Waliunda dola kutoka ndani ya dola, kiasi kwamba tunahisi uchungu kamili wa sera ya kugawanya et impera (gawanya utawale) ya Wamagharibi.

Licha ya wingi wetu, kutokana na kukosekana Khilafah ya kutukinga, mataifa ya maadui yanatushambulia kama tulivyoonywa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

«يُوشِكُ الأُمَمُ أنْ تَدَاعَى عَليْكُم كَمَا تَدَاعَى الأكَلَةُ إلَى قَصْعَتِهَا»

“Mataifa yataitana dhidi yenu kama walaji wanavyoitana kwa ajili ya mlo.” Wakauliza, “Je, tutakuwa ni wachache siku hiyo?” Yeye (saw) akajibu,

«بَلْ أنْتُمْ يَوْمَئِذٍ كَثِيرٌ، وَلَكِنّكُمْ غُثَاءُ كَغُثَاءِ السّيْلِ، وَلَيَنْزِعَنّ اللّهُ مِنْ صُدُورِ عَدُوكُمْ المَهَابَةَ مِنْكُمْ، وَلَيَقْذِفَنّ اللّهُ في قُلُوبِكُم الَوَهْنَ»

“Bali siku hiyo mutakuwa wengi, lakini mtakuwa kama povu la mafuriko. Na Mwenyezi Mungu ataondoa kutoka vifuani mwa adui zenu hofu kwenu na atatia katika vifua vyenu al-Wahn.” Wakauliza, “Al-Wahan ni nini, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Yeye (saw) akajibu,

«حُبّ الدّنْيَا وَكَرَاهِيَةُ المَوْتِ» “Kupenda dunia na kuchukia kifo.” (Abu Daud).

Bila ngao yetu, Khilafah, ardhi zetu zimekaliwa kimabavu na watu wetu wanauawa kishahidi, licha ya sisi kuwa na wanajeshi zaidi ya milioni tatu. Tuna njaa, licha ya kuwa na rasilimali bora zaidi duniani chini ya miguu yetu. Upotofu unawanyesha juu ya watoto na familia zetu, ingawa tumebeba Dini moja ya haki nyoyoni mwetu!

Enyi Waislamu, kwa hakika, Khilafah haikuanguka bila majibu kutoka kwa babu zetu!

Kuvunjwa kwa Khilafah kulitikisa wasomi wa Kiislamu wa Bara Dogo la India, ingawa lilikuwa linakaliwa na Waingereza wakati huo.

Iqbal alisoma “Jawab-e-Shikwa (Jibu la Malalamiko)” katika Msikiti wa Bhadshahi wa Lahore, mnamo Novemba 1912, ili kukusanya fedha kwa ajili ya Khilafah. Shaukat Ali na Muhammad Ali Johar kutoka Utter Pradesh walianza juhudi za kuwahamasisha Waislamu kwa ajili ya kuinusuru Khilafah, katika Tehreek e Khilafat (Harakati ya Khilafah).

Waislamu waliwashutumu makhaini miongoni mwa Waarabu, walioasi dhidi ya Khilafah.

Baada ya msaliti mzalendo wa Kiarabu, Sharif Hussain, kuipiga vita Uthmani Khilafah, mnamo Juni 1916, maandamano yalifanyika katika Bara Dogo la India dhidi ya uasi wake. Mnamo tarehe 26 Juni 1916, azimio lilipitishwa huko Lucknow la kulaani "mwenendo wa kuchukiza" wa Hussain. Baada ya kukaliwa kwa Khilafah, fatwa ilisambazwa katika India Iliyokaliwa, mnamo Februari 1919, ambayo ilitangaza kwamba kuteuliwa kwa Imam au Khalifa ni faradhi.

Waislamu hawakutulia wakati wahaini miongoni mwa Waturuki walipoindoa Khilafah, mnamo tarehe 3 Machi 1924. Tarehe 9 Machi 1924, Waislamu wa India Iliyokaliwa kwa mabavu walikusanyika ili kuandaa matukio, kwa ajili ya kuirudisha Khilafah.

Walitoa onyo la telegram kwamba kuondolewa kwa Khilafah "kungefungua mlango kwa matarajio mabaya." Waraka ulitolewa ukitaka jina la Khalifa aliyeondolewa madarakani, Abdul-Majeed, litajwe katika Swala za Ijumaa.

Hivi ndivyo mababu zetu watukufu walivyokuwa, walipoiona Khilafah ikianguka. Basi tunapaswa kuwa vipi, wakati imepita zaidi ya karne moja ya Hijri, tangu Khilafah ilipoanguka?

Enyi Waislamu, sisi ni wenye dhambi isipokuwa tukifanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah!

Hairuhusiwi kwetu kuwa bila ya Khalifa, kutuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَـفِرُونَ)  “Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [Surah Al-Ma’idah 5:44]

Abdullah Ibn ‘Abbas (ra) amesherehesha, من جحد ما أنزل الله فقد كفر ومن أقر به ولم يحكم فهو ظالم فاسق “Yeyote wenye kuyakataa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru, na anayeyakubali aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na wala hakuhukumu kwayo, basi huyo ni dhalimu na Fasiq (muasi) na mwenye dhambi.” [Imepokewa na Ibn Jarir]

Kumteua Khalifa inakuwa ni faradhi juu yetu, kuanzia pale Khalifah aliyetangulia anapokufa, au kuondolewa.

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (ra) kuwa Mtume (saw) amesema:

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ، قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»

“Banu Isra'il wanasiasa wao walikuwa ni Mitume. Kila Mtume mmoja akifa, alifuatiwa na Mtume mwengine; na hakika yake hakutakuwa na Mtume mwengine baada yangu na kutakuweko na makhalifa na watakuwa ni wengi. Maswahaba wakamuuliza: je, watuamrisha nini? Akasema: mpeni bay’ah (ahadi ya utiifu) mmoja baada mmoja, na muwape haki zao (yaani watiini) kwani hakika Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya yale aliyowatawalisha kwayo.” (Bukhari na Muslim).

Ijma’a ya Maswahaba (ra) inatufikishia amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), enyi Waislamu. Kwa Ijma’a hii, imethibiti kwamba hairuhusiwi kwetu kutokuwa na Bayah kwa Khalifa kwa zaidi ya michana mitatu na masiku yake. Al-Bukhari ameripoti kupitia Al-Miswar Bin Makhramah aliyesema: فَقَالَ أَرَاكَ نَائِمًا، فَوَاللَّهِ مَا اكْتَحَلْتُ هَذِهِ اللَّيْلَةَ بِكَبِيرِ نَوْمٍ Abdul-Rahman aliniita baada ya kipande cha usiku kupita na akabisha mlango wangu mpaka nikaamka, na akaniambia, “Naona ulikuwa umelala! Wallahi, katika masiku matatu yaliyopita sijalala vya kutosha.”

Imepita karne moja ya Hijri, sio tu michana mitatu na masiku tatu, bila sisi kutimiza faradhi ya Khilafah. Kwa hivyo hatujachelewa kujiunga na kazi ya kuisimamisha upya?!

Enyi Waislamu, ni lazima tusimamisha tena Khilafah, ili tutawaliwe na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt)!

Khalifa hatawali kwa maoni yake ya kibinafsi, wala maoni ya maafikiano ya mkusanyiko.

Anatawala kwa mujibu wa Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Yeye yuko chini ya Sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) katika mzozo wowote na wale anaowatawala. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ)

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” [Surah an-Nisa’a 4:59]

Khalifa Muongofu (Rashid) wa kwanza, Abu Bakr as-Sadiq (ra), alilinda haki za wanyonge, kwa kuhukumu kwa mujibu wa Uislamu. Yeye (ra) alitangaza, وَالضّعِيفُ فِيكُمْ قَوِيّ عِنْدِي حَتّى أُرِيحَ عَلَيْهِ حَقّهُ إنْ شَاءَ اللهُ, وَالقَوِيّ فِيكُمْ ضَعِيفٌ عِنْدِي حَتّى آخُذَ الحَقّ مِنْهُ إنْ شَاءَ اللهُ “Na mnyonge kwenu kwangu mimi ni mwenye nguvu mpaka ni mrudishie haki yake, Mwenyezi Mungu akipenda, na mwenye nguvu kwenu kwangu mimi ni mnyonge mpaka niichukue haki kutoka kwake, Mwenyezi Mungu akipenda.”

Khalifa Muongofu (Rashid) wa pili, Umar al-Farooq (ra), aliondoa agizo lake, pindi alipo sahihishwa na mwanamke mmoja, kwa msingi wa dalili ya Kiislamu. Yeye (ra) alitangaza, إِنَّ امْرَأَةً خَاصَمَتْ عُمَرَ فَخَصَمَتْهُ  “Hakika, mwanamke mmoja alizozana na Umar, hali ya kuwa ana haki katika mzozo huo.”

Imepita zaidi ya miaka mia moja ya Hijri ambapo Ummah wa Kiislamu umetawaliwa kwa mengine yasiyokuwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Je, tunawezaje kikaa kimya na bila kutikisika juu ya kuendelea kupuuzwa kwa Dini yetu?

Enyi Waislamu, Khilafah ilikuwa ni ngao kwa wasiokuwa Waislamu, vipi basi Waislamu?!

Mara tu baada ya Upanga wa Mwenyezi Mungu, Khalid Ibn al-Walid (ra), kufungua al-Hira huko kusini mwa Iraq, yeye (ra) aliandika barua kwa Khalifa Abu Bakr (ra). Akamweleza jinsi alivyotekeleza kodi ya Jizyah, lakini amewaacha wasiokuwa Waislamu ambao ni masikini, wazee na walemavu, akisema, طُرِحَتْ جزيتُه وعيلَ من بيت مال المسلمين وعياله “Aliye epushwa na Jizyah, atatajirishwa na Bayt ul Maal ya Waislamu pamoja na familia yake.”

Khilafah ya Umar al-Farooq ilitangaza kwamba Jizyah ingerudishwa kwa raia wasiokuwa Waislamu, kwa sababu haikuweza kuhakikisha ulinzi wao kutoka kwa jeshi la Warumi.

Hata hivyo, badala ya kuwaunga mkono Wakristo wa Kirumi, Wakristo wa Khilafah walitangaza,رَدَّكُمُ اللهُ إلينا، ولَعَنَ اللهُ الذين كانوا يملكوننا من الروم، ولكن والله لو كانوا هم علينا ما ردُّوا علينا، ولكن غصبونا، وأخذوا ما قدَرُوا عليه من أموالنا، لَوِلايتُكُم وعدلُكم أحبُّ إلينا مما كنا فيه من الظلم والغُشْم “Mwenyezi Mungu akurudisheni kwetu salama. Mwenyezi Mungu awalaani wale waliokuwa wakitutawala miongoni mwa Warumi. Lakini, Wallahi lau kama wangekuwa wao ndio wanaotutawala kamwe hawangeturudishia (jizya). Bali wangetubughudhi, na wakatupora mali zenu wawezavyo. Kwa usimamizi wenu na uadilifu wenu tunapendelea zaidi hali hii kuliko hali tuliokuwa chini yake ya dhulma na mateso.”

Baada ya kujua juu ya kufukuzwa kidhalimu kwa Mayahudi kutoka Uhispania, Khilafah ya Sultan Bayezid II ilituma jeshi lake la majini kuwaleta Mayahudi salama kwenye ardhi za Dola ya Khilafah, haswa katika miji ya Thesaloniki na İzmir. Khalifa alitangaza kuhusu mvamizi wa Uhispania, "Unasubutu kumwita Ferdinand "Mwenye Hekima" ilhali yeye ndiye aliyeifukarisha nchi yake mwenyewe na kuitajirisha yangu!"

Katika karne kumi na tatu za Khilafah, wasiokuwa Waislamu walilindwa kwa ngao yake. Hata hivyo, leo, bila ya ngao hii, Umma wa Kiislamu hauna kinga, kwa zaidi ya karne moja ya Hijri. Je! haujafika wakati wa kurudisha ngao yetu enyi Waislamu?

Enyi Waislamu, kufanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah ni faradhi juu yetu, huku Nasr (Ushindi) uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee!

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An-Noor 24:55].

Ibn Kathir amesherehesha katika Tafsir yake, هذا وعد من الله لرسوله صلى الله عليه وسلم . بأنه سيجعل أمته خلفاء الأرض ، أي : أئمة الناس والولاة عليهم ، وبهم تصلح البلاد ، وتخضع لهم العباد ، وليبدلن بعد خوفهم من الناس أمنا وحكما فيهم “hii ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa Mtume Wake (saw) kwamba ataufanya Ummah wake kuwa makhalifa duniani, yaani, watakuwa viongozi na watawala wa wanadamu, ambao kupitia kwao ataurekebisha ulimwengu na watu watasalimu amri kwao, na atawabadilishia hofu yao kwa watu iwe usalama utawala ndani yao.”

Hivyo basi, Mwenyezi Mungu (swt) ametuahidi kutupa Nasr (Ushindi) ikiwa tutamtii Yeye (swt), huku Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akitupa bishara njema ya kuregea Khilafah, baada ya utawala wa dhulma.

Amesema (saw),

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّة»

“Kisha utakuwepo utawala wa utenzaji nguvu, na utakuwepo kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka uwepo. Kisha atauondoa anapotaka kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Baada ya kauli hii, yeye (saw) akanyamaza.

Baada ya kuifahamu ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume (saw), je, haituhimizi sisi kuondosha kutojali au kutokuwa na matumaini, kutimiza faradhi yetu, bila ya kusitasita au kupuuza?!

Enyi Waislamu, hebu natufanye kazi ya kusimamisha tena Khilafah, mpaka Mwenyezi Mungu (swt) arudishe hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Yeye (swt).

Hakika Mtume (saw) na Maswahaba zake Watukufu (ra) walipata shida kubwa mikononi mwa madhalimu, ili kuhakikisha hukmu kwa yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Pindi alipoombwa (saw) na ami yake aachane na ulinganizi, yeye (saw) alijibu:

«يَا عَمّ ، وَاَللّهِ لَوْ وَضَعُوا الشّمْسَ فِي يَمِينِي ، وَالْقَمَرَ فِي يَسَارِي عَلَى أَنْ أَتْرُكَ هَذَا الْأَمْرَ حَتّى يُظْهِرَهُ اللّهُ أَوْ أَهْلِكَ فِيهِ مَا تَرَكْتُهُ»

Ewe ami!, Wallahi, lau wangeweka jua kwenye mkono wangu wa kulia na mwezi kwenye mkono wangu wa kushoto, ili niwache amri hii (Uislamu) sitaiacha mpaka Mwenyezi Mungu aidhihirishe Dini hii kuwa yenye nguvu au niangamie katika njia hii.” Hivyo, bora wa vizazi vyote (ra) waliamini, wakafanya kazi na wakajitoa muhanga pamoja na Mtume (saw), mpaka Mwenyezi Mungu (swt) Akatoa Nasr yake, akausimamisha Uislamu kwenye mamlaka, ndani ya Al-Madinah al-Munawarah.

Kutochukua hatua juu ya kuregesha Khilafah kumeendelea kwa zaidi ya miaka mia moja ya hijri.

Adhabu za dunia hii, katika upande wa mateso na udhalilifu zimefikia kilele. Udhalilifu mmoja haumaliziki isipokuwa huanza udhalilifu mwingine. Kila udhalilifu hupelekea tu udhalilifu mwengine mkubwa zaidi. Enyi Waislamu, dhambi la kutochukua hatua si chaguo kwa yeyote anayempenda Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Tusipoteze yale aliyotuneemesha Mwenyezi Mungu (swt) ya afya na wakati. Tuwekeze yote katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Natuchumeni idhini ya kuingia kwenye Jannah Yake, katika Aakhira yenye kudumu milele.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«نِعْمَتَانِ مَغْبُونٌ فِيهِمَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ الصِّحَّةُ وَالْفَرَاغُ»

“Neema mbili ambazo watu wengi huzipoteza ni: Afya njema wakati wa faragha.” [Bukhari]

Hakika ardhi za Waislamu zimetiwa giza na hukmu ya ukafiri, uasi na uonevu kwa muda mrefu sana. Kila mmoja wetu na atimize wajibu wake, mpaka nuru ya Uislamu ituangazie sisi sote kwa mara nyengine tena.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

#أقيموا_الخلافة                             #كيف_تقام_الخلافة

#ReturnTheKhilafah                 #YenidenHilafet

       #RealChange                            #TurudisheniKhilafah

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu