Jumatatu, 17 Dhu al-Qi'dah 1444 | 2023/06/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uacheni! Hakika ni Uvundo

(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[لَقَدْ مَنَّ اللَّهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولا مِنْ أَنْفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِنْ كَانُوا مِنْ قَبْلُ لَفِي ضَلالٍ مُبِينٍ]

“Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwa waumini vile alivyowaletea Mtume aliye miongoni mwao wenyewe, anayewasomea aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima, ijapokuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotovu ulio wazi.” [Aal-Imran:164].

Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika aya hapo juu kuwa Mtume (saw) ameitakasa jamii (وَيُزَكِّيهِمْ) kutokana na njia ya Jahiliyah.

Ni muhimu kufahamu maana na uhalisia wa neno “Jahiliyah” ili tuifahamu jamii ya sasa ambayo tunaishi. Ili, hitajio la kurejesha tena Khilafah liwe na umuhimu wa kipekee katika maisha ya Waislamu. Tunapoangalia uhalisia wa jamii ya Makkah yenyewe na Waarabu kwa jumla, tunaona kwamba kulikuwa na baadhi ya makabila yanayo hama hama na kulikuwa na uwepo wa makabila kama Thaqif, Quraish, Shaiban na mengineyo. Maquraish hasa walifaidika na uongozi jumla miongoni mwa makabila yote ya Kiarabu kutokana na Usimamizi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu. Walikuwa wakijadili sera katika Dar An-Nadwa ambapo viongozi wa Kiquraish wakifanya maamuzi kuhusu Makkah. Hili lilionekana wazi wakati walipoingia katika vita na mikataba na Mtume (saw).

Kwa upande wa uchumi, Maquraish walikuwa na muungano imara wa kibiashara na maeneo ya kaskazini na kusini, yaani wakiweza kusafiri kutoka Yemen wakati wa baridi na Sham wakati wa joto. Mwenyezi Mungu (swt) amelieleza hili katika Surat Quraysh,

[إِۦلَـٰفِهِمْ رِحْلَةَ ٱلشِّتَآءِ وَٱلصَّيْفِ]

“Kuzowea kwao safari za siku za baridi na siku za joto” [Quraysh: 2].

Wakati wa msimu wa Hajj, waliweza kuwa na itifaki kwa ajili ya hajj na kuwa na haki ya pekee juu ya nguo ya Ihram; hii inaonyesha kuwa Maquraish walijulikana sana kwenye biashara ndani na nje ya Bara Arabu na walikuwa na umiliki juu ya Ka’aba na uchumi wake. Haiwezi kusemwa kuwa Waarabu na Maquraish hawakuwa wakitambua siasa na uchumi wa wakati wao na jamii zao.

Hata hivyo, tunapoangalia maana ya kilugha ya neno Jahiliya, humaanisha watu wasiokuwa na elimu ya kuandika na kusoma, lakini Maquraish na Waarabu walikuwa ni wabobezi katika lugha yao; ni maarufu katika ufasaha na ushairi. Kwa kweli lugha ya Kiarabu ni tajiri zaidi katika ufasaha hata kabla ya kuja kwa Mtume wa mwisho katika mji wa Makkah. Washairi walishindana masokoni na mashairi bora zaidi yakitundikwa ndani ya Ka’aba.

Masuala ya siasa, uchumi na lugha yalidhihirisha kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakuainisha Maquraish kuwa watu wa Jahiliya kwa maana ya kilugha. Bali ilikusudiwa katika maana ya ‘hali ya wanadamu’ ambapo jamii iliamini kuwa Mwenyezi Mungu ni bwana wa mbinguni lakini sio ardhini.

Mtume wetu Mpendwa alilitumia neno hili kwa maana hii katika sehemu nyingi. Baadhi yazo kwa uchache ni hizi:

1. Swahaba aliye na hasira alisema kumwambia mwenzake "يا ابن السوداء

“Ewe mtoto wa mwanamke mweusi” ambapo Mtume (saw) alimkemea Swahaba huyo kwa kusema:

«إنك امرؤ فيك جاهلية»  “Wewe ni mtu mwenye mabaki ya jahiliya.”

2. Wakati kundi la Answar na Muhajirina wakikaribia kupigana, Mtume (saw) aliingilia kati na kusema مَا بَالُ دَعْوَى الْجَاهِلِيَّةِ؟ دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ»  « “Nini hii miito ya kijahiliya? Iacheni, huo ni uvundo.”

Katika jamii ya kijahiliya, watu walibaguana kwa misingi ya rangi, asili na kabila. Katika jamii ya Kijahiliya, watu walikuwa wakiunga mkono kabila lao hata kama walikuwa ni wakosa.

Japokuwa matukio haya yalitokea Madina baada ya kuasisiwa dola ya Kiislamu, Mtume (saw) aliendelea kutumia neno Jahiliya. Katika matukio haya Jahiliya inahusu hali ya wanadamu, na sio ujinga wao. Hali hii ya wanadamu haijafungwa kwa Maquraish au Makkah tu, bali ilihusishwa na jamii nyengine na pindi uhalisia wa jamii hizo ulipowiana.                                           

Neno “Jahiliya” limetumiwa na Mwenyezi Mungu (swt) katika mazingira yafuatayo:

1. Fikra isiyo sahihi kuhusu Muumba (ظن الجاهلية)

2. Hukmu katika Jahiliya (حكم الجاهلية)

3. Tabarruj za Kijahiliya (تبرج الجاهلية)

4. Majivuno ya Kijahiliya (حمية الجاهلية)

Fikra isiyo sahihi kuhusu Muumba (ظن الجاهلية)

Tokea kuumbwa kwa mwanadamu, amekuwa akipokea uongofu kutoka kwa Muumba kupitia Mitume na Manabii ili wamtakase na kumtii Muumba kama walivyoamrishwa. Hata hivyo, pote la wenye nguvu na athari la wanadamu lilipotoka katika kumtakasa Muumba kutokana na kukataa uongofu wa Mwenyezi Mungu (swt).

Ukristo unaamini kuwa Malaika ni watoto wa Mwenyezi Mungu. Wapagani wanaamini kuwa Malaika pia wanaabudiwa kama waungu.

[وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ ۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغْنِى مِنَ ٱلْحَقِّ شَيْـًۭٔا]

“Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipokuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.” [Al-Najm: 28]

Wapagani wamekuwa wakimsifia Mwenyezi Mungu kuwa ana watoto

[أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلْأُنثَىٰ]

“Je! nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?” [Al-Najm: 21]

Madai yote haya ya uongo na sifa hizo kwa Mwenyezi Mungu zitaulizwa Siku ya Kiyama.

[وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ]

“Na nini dhana ya wanaomzulia Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ana fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.” [Yunus: 60]

Katika karne za karibuni, tulishuhudia ujio wa Ukomunisti na Ubepari ambapo Ukomunisti unakanusha uwepo wa Muumba na Ubepari unaamini kuwa Muumba hana dori katika masuala ya kijamii, huku Ukomunisti ukiwa na mantiki potofu ya kufikiri na Ubepari ukigusia suali kubwa zaidi la mwanadamu kwa namna ya maafikiano.

Ubepari umegonganisha akili za Waislamu ambapo manufaa yamekuwa jambo kuu hata katika masuala yanayohusu kumtakasa Muumba kuliko kupata thamani ya kiroho.

[وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللَّـهَ عَلَىٰ حَرْ‌فٍ ۖ فَإِنْ أَصَابَهُ خَيْرٌ‌ اطْمَأَنَّ بِهِ ۖ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِ خَسِرَ‌ الدُّنْيَا وَالْآخِرَ‌ةَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَ‌انُ الْمُبِينُ]

“Na katika watu wako wanaomuabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na akhera; hiyo ndio khasara iliyo wazi.” [Al-Haj:11]

Sababu ya uelewa wote huu mbaya kwa Muumba ni kutokana na kufuata fikra za Kijahiliya. Kwa maana nyengine, huu ni “ujinga wa kabla ya Uislamu” na kufuata wazee wa zamani kibubusa bila kufikiri Mapenzi ya Muumba.

[وَطَآئِفَةٌۭ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِٱللَّهِ غَيْرَ ٱلْحَقِّ ظَنَّ ٱلْجَـٰهِلِيَّةِ]

“Na kundi jengine nafsi zao ziliwashughulisha hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyo kuwa ya haki, dhana ya kijinga.” [Aal-Imran:154]

Hukmu za Kijahiliya (حكم الجاهلية)

Nidhamu ya kisiasa ambayo Mwenyezi Mungu ameileta kwa Mtume Wake wa mwisho ni nidhamu ya Khilafah ambapo Mwenyezi Mungu amejiweka Yeye Mwenyewe kuwa ndiye mwenye mamlaka, na Ummah utafanya ijtihad kuvua sheria kutoka vyanzo vya Wahyi, na utakuwa na mamlaka ya kumchagua mtawala mmoja yaani, Khalifah.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ]

“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu” [Yusuf:40]

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ]

“Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [Al-Ma’ida:44].

Wakati wa maisha ya Mtume wa mwisho (saw), uongozi wa kikabila ulikuwa ukiendesha mambo ya makabila katika maeneo ya Arabuni ambapo utukufu wa kikabila, kuwakandamiza madhaifu, uuaji wa watoto wa kike, uzinifu vilikuwa ni mambo yaliokubalika na jamii hiyo; kulikuwa na ustaarabu wa jamii nyengine kama Warumi wa Mashariki, Bizantino, Waajemi, zikiwa na idadi kubwa sana ya watu wakitawaliwa na mahitajio na matamanio ya tabaka tawala. Ilikuwa ni wakati huu ambapo Mtume (saw) alisimamisha dola Madina kama alivyotakiwa na Muumba. Aliyalingania Uislamu makabila yote ya Arabuni na kuyaweka chini ya utawala wa Kiislamu. Mnamo mwaka wa sita wa Hijra, aliwapelekea barua wafalme wa mataifa akiwataka kuja katika utawala wa Kiislamu na mataifa haya yaliingizwa ndani ya utawala huo wakati wa Makhalifa waongofu (Khulafaa Rashidin).

Kwa zaidi ya milenia moja, Uislamu ulikuwa ukitabikishwa kama mfumo wa kisiasa ulioenea Asia, Afrika na Ulaya ambako kabla maeneo hayo yalikuwa chini ya mfumbato wa Jahiliya. Mnamo karne ya 18, kulizuka mifumo mipya ya kisiasa, Urasilimali na Ukomunisti, kutokana nayo kukaja fikra za kisiasa kama Demokrasia/Jamhuri (Serikali: Ya watu, Kupitia kwa watu, Kwa ajili ya watu), Usekula (Kumtenganisha Muumba na masuala ya kisiasa) na aina ya dola ya Wana-kamati wa Kikomunisti.

Japokuwa istilahi hizi zinaonekana ni mpya, lakini ni za Kijahiliya zikiwa katika aina ya kisasa kwa kuwa ni mifumo inayowatawala watu kwa fikra zilizoundwa na wanaadamu zinazopingana na Ubwana wa Muumba kwa viumbe wake.

Aina ya mfumo wa dola za Kidemokrasia na Ukomunisti zimeisukuma jamii kwa fikra msingi ya kukataa Ubwana wa Muumba, kutukuza fikra za kisayansi kuwa ndio msingi wa jamii lakini bado kulipatikana mpambano baina ya Urasilimali na Ukomunisti uliokuwa katika karne ya 20 hadi kuvunjika kwa USSR kulikofikisha mwisho wa Ukomunisti. Kutokea hapo dunia imetawaliwa na mfumo mmoja pekee uitwao Urasilimali ambao wanafikra wake wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea itikadi ya usekula na nidhamu ya demokrasia kuwa ni suluhisho muafaka kwa dunia yote. Kwa bahati mbaya, baadhi ya Waislamu, kutokana na kuwa na msingi dhaifu katika Uislamu, hawakuweza kuonyesha makosa ya fikra za Magharibi badala yake walishawishiwa na fikra hizo hizo na kujikuta ni wahanga wake; hivyo, baadhi ya wanafikra wa Kiislamu wanatetea njia ya Wamagharibi ya kuusanifu Uislamu kama kutangaza (fikra za) ‘Demokrasia ya Kiislamu’, ‘Jamhuri ya Kiislamu’, na Dini mesto.

Mwenyezi Mungu (swt) amekemea matendo haya kwa kusema,

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللّهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’ida:50].  

Tabarruj za Kijahiliya (تبرج الجاهلية)

Fikra ya kujirembesha kwa wanawake sio mpya, wanawake wanahaki ya kuhangaikia mahitaji yao. Makkah kabla ya kuja kwa Mtume wa mwisho, wanawake walikuwa wakijirembesha na kujasirisha kutoka nje ya nyumba zao. Mwenyezi Mungu (swt) alielezea suala hili na kufafanua Hukmu kwa wanawake kuhusiana na kujirembesha nje ya maeneo yao khasw.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ ٱلْجَـٰهِلِيَّةِ ٱلْأُولَىٰ]

“Na wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahiliya ya kizamani.” [Al-Ahzab:33].

Propaganda, kama “Hijab inawakandamiza wanawake wa Kiislamu”, fikra ya utetezi wa haki za wanawake inayofanyiwa kazi na mfumo wa Kimagharibi ina athari katika Ulimwengu wa Kiislamu. Kukua kwa fikra ya utetezi wa haki za wanawake kumepelekea dhana kama ‘wanawake wapo juu zaidi ya wanaume’, ‘mwili wangu ni haki yangu’, ‘chagua jinsia (hata ukiwa na umri wa miaka 11!) zimevunja muundo wa kijamii na kuzusha changamoto zaidi kwa wanawake na kuwalazimisha kuingia kwenye soko la ajira.

Fikra ya Kimagharibi imekuza fikra za uhuru binafsi, imehalalisha ushibishaji wa ghariza ya kijinsia nje ya mahusiano ya ndoa kama ilivyokuwa katika Jahiliya ya Makkah. Kama mama wa waumini Aisha (ra) alivyosema, النِّكَاحَ كَانَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ عَلَى أَرْبَعَةِ أَنْحَاءٍ فَنِكَاحٌ مِنْهَا نِكَاحُ النَّاسِ الْيَوْمَ يَخْطُبُ الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ وَلِيَّتَهُ فَيُصْدِقُهَا ثُمَّ يَنْكِحُهَا وَنِكَاحٌ آخَرُ كَانَ الرَّجُلُ يَقُولُ لاِمْرَأَتِهِ إِذَا طَهُرَتْ مِنْ طَمْثِهَا أَرْسِلِي إِلَى فُلاَنٍ فَاسْتَبْضِعِي مِنْهُ وَيَعْتَزِلُهَا زَوْجُهَا وَلاَ يَمَسُّهَا أَبَدًا حَتَّى يَتَبَيَّنَ حَمْلُهَا مِنْ ذَلِكَ الرَّجُلِ الَّذِي تَسْتَبْضِعُ مِنْهُ فَإِذَا تَبَيَّنَ حَمْلُهَا أَصَابَهَا زَوْجُهَا إِنْ أَحَبَّ وَإِنَّمَا يَفْعَلُ ذَلِكَ رَغْبَةً فِي نَجَابَةِ الْوَلَدِ فَكَانَ هَذَا النِّكَاحُ يُسَمَّى نِكَاحَ الاِسْتِبْضَاعِ وَنِكَاحٌ آخَرُ يَجْتَمِعُ الرَّهْطُ دُونَ الْعَشَرَةِ فَيَدْخُلُونَ عَلَى الْمَرْأَةِ كُلُّهُمْ يُصِيبُهَا فَإِذَا حَمَلَتْ وَوَضَعَتْ وَمَرَّ لَيَالٍ بَعْدَ أَنْ تَضَعَ حَمْلَهَا أَرْسَلَتْ إِلَيْهِمْ فَلَمْ يَسْتَطِعْ رَجُلٌ مِنْهُمْ أَنْ يَمْتَنِعَ حَتَّى يَجْتَمِعُوا عِنْدَهَا فَتَقُولُ لَهُمْ قَدْ عَرَفْتُمُ الَّذِي كَانَ مِنْ أَمْرِكُمْ وَقَدْ وَلَدْتُ وَهُوَ ابْنُكَ يَا فُلاَنُ فَتُسَمِّي مَنْ أَحَبَّتْ مِنْهُمْ بِاسْمِهِ فَيُلْحَقُ بِهِ وَلَدُهَا وَنِكَاحٌ رَابِعٌ يَجْتَمِعُ النَّاسُ الْكَثِيرُ فَيَدْخُلُونَ عَلَى الْمَرْأَةِ لاَ تَمْتَنِعُ مِمَّنْ جَاءَهَا وَهُنَّ الْبَغَايَا كُنَّ يَنْصِبْنَ عَلَى أَبْوَابِهِنَّ رَايَاتٍ يَكُنَّ عَلَمًا لِمَنْ أَرَادَهُنَّ دَخَلَ عَلَيْهِنَّ فَإِذَا حَمَلَتْ فَوَضَعَتْ حَمْلَهَا جُمِعُوا لَهَا وَدَعَوْا لَهُمُ الْقَافَةَ ثُمَّ أَلْحَقُوا وَلَدَهَا بِالَّذِي يَرَوْنَ فَالْتَاطَهُ وَدُعِيَ ابْنَهُ لاَ يَمْتَنِعُ مِنْ ذَلِكَ فَلَمَّا بَعَثَ اللَّهُ مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم هَدَمَ نِكَاحَ أَهْلِ الْجَاهِلِيَّةِ كُلَّهُ إِلاَّ نِكَاحَ أَهْلِ الإِسْلاَمِ الْيَوْمَ‏.‏ “Ndoa katika zama za Jahiliya zilikuwa ni aina nne: Moja ya hizo ni ndoa kama wanayofanya watu hivi leo. Mtu huposa mtoto au ndugu wa mwenzake. Wanakubaliana mahari na kumuoa. Na ndoa nyengine mume humwambia mkewe anapotwahirika na hedhi kwenda kwa mtu fulani na kufanya nae tendo la ndoa. Mume hujitenga nae na hamuingilii hadi amebeba mimba ya yule mtu. Inapodhihirika kuwa amebeba mimba mume huambatana naye pindi akitaka. Ndoa hii ilijulikana kama ndoa ya ‘istibdha’ (kumtumia mwanamume kwa ajili ya kizazi chenye hadhi). Aina ya tatu ilikuwa ni kundi la watu chini ya kumi humuingilia mwanamke. Anaposhika ujauzito na kujifungua na kupita masiku kadhaa huwaendea na kukusanyika wote. Huwaambia “Mnaelewa juu ya jambo lenu. Nimejifungua mtoto. Na huyu ni wako wewe fulani. Anamtaja yeyote anaempenda kati yao na mtoto hunasibishwa naye. Aina ya nne ilikuwa watu wengi huenda kwa mwanamke kufanya naye tendo la ndoa bila kumzuia yeyote anaemwendea. Hawa ni makahaba. Wakipandisha bendera milangoni ikiwa ni alama kwa anayetaka kuingia. Anapokuwa mjamzito na kujifungua mtoto, wanajitokeza kwake na kuwataka wataalamu kufuatilia mahusiano kutokana na sifa za umbile la mtoto. Wanamhusisha mtoto kwa yule wanayemzingatia kufanana na hupewa mtoto. Mtoto huambiwa kuwa ni wake na hawezi kumkana. Wakati Mwenyezi Mungu (swt) alipomtumiliza Muhammad kuwa Mtume, alikataza aina zote za ndoa zilizokuwepo wakati huo isipokuwa ile ambayo Waislamu wanaitekeleza hivi leo. (Sunan Abi Dawud 2272)

Fikra za Wamagharibi zinatoa kipaumbele matamanio na maslahi dhidi ya maadili na kuruhusu aina zote za uovu unaovuruga familia na maadili ya kijamii. Ulaya na Amerika zimekuwa zikihuisha matendo maovu baina ya wanaume na wanawake kwa jina la uhuru. Matendo haya yaliondolewa na Uislamu zaidi ya milenia moja nyuma kwa muongozo wa Muumba ulioletwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw).

Majivuno ya Kijahiliya (حمية الجاهلية)

Watu hujigamba na kujifakharisha kwa kabila zao, lugha na taifa, nayo hujulikana kama utaifa; fikra hii ya dola ya kitaifa imekuzwa na Wamagharibi wakati wa baada ya Vita vya Dunia ili kudhibiti mamlaka ya dola hii mpya iliyoundwa iliyo dhaifu. Hivi ndivyo fikra ya uzalendo na utaifa ilivyopata nguvu zaidi japokuwa huu ni wito dhaifu; ambapo Uislamu ni mfumo wa kilimwengu unaounganisha watu waliotafautiana makabila, rangi na lugha, kwani itikadi yake imeegemea juu ya fikra pana kuhusu mwanadamu, uhai na ulimwengu. Mtume (saw) ameweka mfano mzuri wa mwanadamu utakaokuwa na athari njema hata kwa jamii nyengine.

[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَـٰكُم مِّن ذَكَرٍۢ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَـٰكُمْ شُعُوبًۭا وَقَبَآئِلَ لِتَعَارَفُوٓا۟ ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ ٱللَّهِ أَتْقَىٰكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌۭ]

“Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika alie mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” [Al-Hujurat :13].

Zaidi ya hivyo, udugu miongoni mwa waumini unashinda mipaka bandia ya kitaifa ya Sykes-Picot na mstari wa Durand. Kwani Uislamu unasema, utiifu na kukana ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwa Shariah. Na katika utaifa, utiifu unahama kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye amewaamrisha waumini kwa kusema:

[إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُواْ]

“Hakika Rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walioamini.” [Al-Ma’ida:55]. Na kauli yake:

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ]

“Hakika waumini ni ndugu” [Al-Hujurat:10]. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt),

[إِذْ جَعَلَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ ٱلْجَـٰهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ وَأَلْزَمَهُمْ كَلِمَةَ ٱلتَّقْوَىٰ وَكَانُوٓا۟ أَحَقَّ بِهَا وَأَهْلَهَا ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمًۭا]

“Pale waliokufuru walipotia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya waumini, na akawalazimisha neno la kuchamungu, na wao walikuwa ndio wenye haki nalo na wenye kustahili. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.” [Muhammad: 26].

Hitimisho

Hii ni mitazamo tafauti ya jamii za Kijahiliya ambayo imeonyeshwa katika vyanzo vya Wahyi ambapo athari zake zimen’golewa kwa utabikishaji wa mfumo wa Kiislamu na kisha imehuishwa tena na makafiri, na waliweza kufanya hayo kwa kuivunja Khilafah mnamo 1342 H. Ili Waislamu waweze kuhuisha njia ya maisha ya Kiislamu, ni muhimu kupata utambuzi kuhusu Jahiliya mambo leo na athari zake katika maisha ya wanadamu. Hivyo, Jahiliya kama ilivyozingatiwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ifahamike kuwa ni “Hali ya wanadamu” ambao wanakataa muongozo wa Muumba.دعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» « “Uacheni (Ujahiliya). Kwani kwani hakika huo ni uvundo”

Kurejeshwa kwa Khilafah kutapelekea kuirejesha njia kamili ya maisha ya Kiislamu kivitendo na kujitenga na matendo ya Kijahiliya ambayo yamekatazwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa hakika, dola ya Khilafah itaeneza Uislamu duniani kote kupitia da’wah na Jihad.

Mtume (saw) amesema, «أَلَا كُلُّ شَيْءٍ مِنْ أَمْرِ الْجَاهِلِيَّةِ تَحْتَ قَدَمَيَّ مَوْضُوعٌ» “Kila kinachofungamana na mambo ya kijahiliya ni chenye kuwekwa chini ya miguu yangu.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Abdur Rahman bin Hamid

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu