Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuunda Kizazi Kitakachopigania Hadhi ya Juu Zaidi Machoni mwa Mwenyezi Mungu (swt) Pekee

(Imetafsiriwa)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَنِ الْتَمَسَ رِضَاءَ اللَّهِ بِسَخَطِ النَّاسِ كَفَاهُ اللَّهُ مُؤْنَةَ النَّاسِ، وَمَنِ الْتَمَسَ رِضَاءَ النَّاسِ بِسَخَطِ اللَّهِ وَكَلَهُ اللَّهُ إِلَى النَّاسِ»

“Yeyote mwenye kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa hasira za watu, Mwenyezi Mungu atamtosheleza kutokana na watu. Na anayetafuta radhi za watu kwa hasira za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamuwakilishia watu.” (Tirmidhi)

Lengo ambalo Waislamu wanalo kwa kila mtu juu ya matendo yao ni katika kutaka Radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na si chengine. Tunapofunga mwezi wa Ramadhan, tunapotekeleza Swala, kutafuta elimu ya Dini, kuamrisha mema na kukataza maovu, kuhukumu kwa Uislamu, kupigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), kuhifadhi maisha ya wanadamu, kuwalea watoto wadogo wasiojiweza, kuwahudumia wazee, kuwapa matumaini na kuwauguza wazazi, kuwa waaminifu katika biashara, kuwa na huruma kwa wanyama, kufanya biashara, kulima au kuzalisha bidhaa viwandani, tunafanya haya yote huku tukitaka radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

Hivyo, Waislamu wanakuwa na lengo hilo wanalolikusudia katika kutafuta Radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na sio kuridhisha matakwa na matamanio yao kwa vile waonavyo katika manufaa ya dunia. Hata hivyo, kama kitendo cha mtu kimepotoshwa baina ya kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na kuwaridhisha watu, basi tendo hili la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu huwa ni Haram, linapelekea Ghadhabu za Mwenyezi Mungu (swt) kwetu!

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ]

“Ambao (wanapofanya matendo mazuri) wanajionyesha.” [Surah Al-Ma’un 107:6].

Imam at-Tabari ameisherehesha aya hii, "الذين هم يراءون الناس بصلاتهم إذا صلوا، لأنهم لا يصلون رغبة في ثواب، ولا رهبة من عقاب، وإنما يصلونها ليراهم المؤمنون فيظنونهم منهم" “Wale wanaotekeleza Swala ili watu wawaone wakiwa wanaswali, kwa sababu hawaswali kwa kutaka thawabu, wala kwa hofu ya adhabu, bali wanaswali ili waumini wawaone na kuwafikiria wao.”

Mtume (saw) amesema katika hadith ya Jandab aliyoipokea Bukhari, «مَنْ سَمَّعَ سَمَّعَ اللَّهُ بِهِ وَمَنْ يُرَائِي يُرَائِي اللَّهُ بِهِ» “Mwenye kuwafanya watu wamsikie, Mwenyezi Mungu atawafanya wamsikie, na mwenye kuwafanya watu wamuone, Mwenyezi Mungu atawafanya wamuone.” [Bukhari].

Kufanya riyaa (kujionyesha) sio wema, kwani wema ni kutaka radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Riyaa ni kujionyesha ili kuwaridhisha watu na hakuna kinachopatikana isipokuwa hasira za Mwenyezi Mungu (swt). Mtume (saw) amesema,

«يَكُونُ فِى آخرِ الزَّمَانِ دِيدَانُ الْقُرَّاءِ، فَمَنْ أَدْرَكَ ذَلِكَ الزَّمَانَ فَلْيَتَعَّوذْ بِاللَّه مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ، وَهُمُ الأَنْتَنُونَ، ثُمَّ تَظْهَرُ قَلَانِسُ الْبُرُودِ فَلَا يُسْتَحَى يَوْمَئِذٍ مِنَ الرِّيَاءِ، وَالْمُتَمَسِّكُ يَوْمَئِذٍ بِدِينِهِ كالْقَابِضِ عَلَى جَمْرَةٍ، وَالْمُتَمَسِّكُ يَوْمَئِذٍ بِدِينِهِ أَجْرُةُ كَأَجْرِ خَمْسِينَ»، قَالُوا: مِنَّا أَوْ مِنْهُمْ؟ قَالَ: «بَلْ مِنْكُمْ»

“Katika zama za mwisho, kutakuwa na mafunza wa wasomaji (Qura’n). Mwenye kudiriki zama hizo, na ajilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa na kwa hao (wasomaji) kwani ndio waliooza zaidi. Kisha kutakuwepo na maguo ya kujifinika, na wakati huo hawatakuwa na haya katika kufanya Riyaa. Yule mwenye kuishika Dini wakati huo ni kama aliyeweka mikono yake juu ya makaa ya moto, na yule aliyeishika Dini wakati huo ujira wake utakuwa kama wa watu hamsini.” Maswahaba wakauliza: Watakuwa hamsini katika sisi au katika wao” Akasema: “Bali katika nyinyi” [Haakim]

Kwa hiyo wale wenye shauku ya kufikia daraja ya juu kwa Mwenyezi Mungu (swt) hawatojali kwa jinsi gani watu watachukulia matendo yao mema. Yule anayesukumwa na Taqwa ya kweli ataamrisha mema na kukataza maovu, bila kujali ima watu wataridhika naye kwa kufanya hayo ama la. Huyu atazungumza haki kwa ushupavu na kuwa muwazi katika kuwawajibisha watu na watawala licha ya lawama ya wenye kulaumu.

Hivyo wale wanaotaka radhi za Mwenyezi Mungu (swt) hawatosumbuliwa na madai potofu ya watu kwani wataepuka kuwa ni wenye kuwafurahisha watu na kuwa na fikra ya hofu ya  kufanya jambo litalopelekea kuchafua hali na kuwashughulisha watu ambayo itapelekea hofu ya kushutumiwa au kubambikiwa na watu katika jamii kuwa ni wenye siasa kali, misimamo mikali nk. Tukielewa kuwa hii taswira hasi ya uongo kwa Waislamu kutoka kwa Makafiri Wamagharibi ni yenye kuendelezwa kupitia kila aina na njia inayopatikana.

Pia kuna fikra ya kuiangalia hali kama ilivyo kiujumla katika jamii za Kirasilimali ambayo ni kuangaliwa hadhi ya mtu kulingana na utajiri, au nasaba, au fursa ya kufikia kwenye cheo na heshima. Viwango kama hivyo vinaweza ima kumzuia yule anayejihisi ana hadhi ya juu zaidi kuliko wengine kusikiliza ushauri mzuri kutoka kwa wengine au inaweza pia kumzuia yule anayejihisi kuwa yupo katika hadhi ya chini kuwa hesabu wengine kwa makosa yao.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ]

“Enyi watu! Hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua, mwenye khabari.” [Al-Hujurat 49:13]

Hivyo muumini huachana na tamaa za kidunia, na huangazia katika kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na kuiangalia Akhera, huunda mahusiano yake kuegemea Uislamu, bila kuzingatia suala la nasaba au mali.

Mtume (saw) amesema,

«إِنَّ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ لَأُنَاسًا مَا هُمْ بِأَنْبِيَاءَ وَلَا شُهَدَاءَ يَغْبِطُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ وَالشُّهَدَاءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِمَكَانِهِمْ مِنْ اللَّهِ تَعَالَى» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ تُخْبِرُنَا مَنْ هُمْ؟ قَالَ: «هُمْ قَوْمٌ تَحَابُّوا بِرُوحِ اللَّهِ عَلَى غَيْرِ أَرْحَامٍ بَيْنَهُمْ وَلَا أَمْوَالٍ يَتَعَاطَوْنَهَا فَوَاللَّهِ إِنَّ وُجُوهَهُمْ لَنُورٌ وَإِنَّهُمْ عَلَى نُورٍ لَا يَخَافُونَ إِذَا خَافَ النَّاسُ وَلَا يَحْزَنُونَ إِذَا حَزِنَ النَّاسُ وَقَرَأَ هَذِهِ الْآيَةَ [أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ]»

“Hakika katika waja wa Mwenyezi Mungu kuna watu ambao sio Mitume wala Mashahidi – Mitume na Mashahidi watawaonea wivu Siku ya Kiyama kutokana na hadhi zao kwa Mwenyezi Mungu (swt). Maswahaba wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tuelezee ni nani hao? Akasema: Hao ni watu wanaopendana kwa roho ya Mwenyezi Mungu bila ya kuwa na mahusiano baina yao wala kwa ajili ya mali wanazopeana. Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, hakika nyuso zao zitakuwa na nuru. Hakika wao watakuwa juu ya nuru. Hawatokuwa na hofu wakati watu watakapokuwa na hofu, wala hawatohuzunika wakati watu watakapohuzunika. Kisha akasoma aya hii: “Hakika vipenzi wa Mwenyezi Mungu hawatokuwa na hofu wala hawatohuzunika.” [Abu Dawud]  

Waumini hao, hata kama sio bora kuliko Mitume na Mashahidi, watakuwa na heshima ambayo hata Mitume au Mashahidi wataitambua hadhi yao kubwa. Basi, muumini na atekeleze jukumu lake wakati wa mwezi huu wa Ramadhan Tukufu, na kila miezi na miaka inayokuja, katika kuweka msingi imara kwa ajili ya zama mpya ya kuibuka kwa Uislamu, kuunda kizazi ambacho kitapigania kwa ajili ya hadhi iliyo kuu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) Pekee.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Tsuoryya Amal Yasna

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu