“...Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.”
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hali chungu ya Waislamu na maisha yao duni katika sehemu zote za ardhi haifichiki kwa mtu yeyote. Popote unapogeuza macho yako, utaona mataifa yanayopigana dhidi yao na nchi zao na uwezo wao, na watawala wao wahalifu wanawatawala, na utaona vita, umaskini, njaa, ukosefu wa usalama na vikwazo juu yao katika kutekeleza ibada zao na kushikamana na ibada za dini yao.