Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ni Bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliyesema:
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Ambayo kwayo tunaweka tegemeo letu

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 7 Mei, Hay’at Tahrir al-Sham (HTS), alivamia nyumba za wanachama wa Hizb ut Tahrir na kuwaweka kizuizini wanachama wake 18. Uhalifu wao ukiwa ni, mara kwa mara kuufahamisha Ummah kwa mitazamo sahihi ya Kiislamu wakati unapoamiliana na masuala mengi ndani ya Syria. Waliwafahamisha Waislamu wanyoofu wa Syria kwamba mbinu za HTS k.m., "kushirikiana na ujasusi wa kimataifa, kuziba midomo, kuiga mbinu ya utawala wa kikandamizaji na kufungia maeneo yake" sio njia ya kusonga mbele kwa umma wa Syria.

Baada ya kukamatwa kwa wanachama 18 wa Hizb ut Tahrir maandamano ya amani yalizinduliwa dhidi ya HTS. Maandamano haya yalipoendelea kukua, HTS iliamua kuingilia kati,” Orwa Ajoub, mchambuzi mkuu katika ‘COAR Global’, aliiambia ‘The New Arab’.

Kukamatwa huko kulizua maandamano, ambayo vikosi vya usalama vya HTS vilisambaratika, na kusababisha mapigano ya moto kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

HTS inatafuta kujionyesha kama mtekelezaji pekee anayewajibika kaskazini-magharibi mwa Syria na haijiepushi kuchukua mbinu zisizo za Kiislamu kufanikisha hili. Hili limewafanya kuwa wakali haswa kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir ambao wako thabiti katika kufikisha njia sahihi za Kiislamu, bila kujali ni matokeo.

Waislamu wanyoofu wa Syria hawatafumbwa macho kwa ajili ya haki. Wanafahamu vyema khiyana ya jumuiya ya kimataifa, ambayo licha ya ushahidi mwingi wa miundo ya utekelezaji wa mukhtasari, kuwekwa kizuizini kiholela, kupotezwa kwa nguvu, mateso, ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia, mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia, njaa kama njia ya vita, uporaji, uchukuaji mateka, mauaji, kuangamiza na vitendo vyengine vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu vinavyofanywa na serikali na vikosi shirika vya kijeshi, pamoja na makundi ya upinzani yenye silaha vimeshindwa kuingilia kati na kuwalinda. Na kwa muda mrefu wamepoteza imani yao kwa wale wanaojiita viongozi wa ulimwengu wa Kiarabu ambao walikubali kwa kauli moja kumregesha mchinjaji Assad kwenye umoja nchi za Kiarabu, licha ya uhalifu wake wa kikatili.

Wanaelewa vyema kabisa kwamba masuluhisho yao yapo kwa Mola wao tu na kwa njia ambazo Yeye (swt) ameziteremsha. Kukamatwa, jela na unyanyasaji hakutawazuia wanachama wa Hizb ut Tahrir kusonga mbele katika kufichua mipango ya wakoloni katika nchi za Kiislamu. Kwani wao wanajua vyema kwamba kukamatwa na kusumbuliwa ndio gharama ya kubeba ulinganizi, na wanakubali, wakisubiri bishara njema, na hawaogopi kwani wamemtegemea Mola wao Mlezi na wanaamini kwa yakini kamili maneno Yake (swt):

[وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ]

“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?” [Fussilat: 33]

«عَجَبًا لِأَمْرِ الْمُؤْمِنِ إِنَّ أَمْرَهُ كُلَّهُ خَيْرٌ وَلَيْسَ ذَاكَ لِأَحَدٍ إِلَّا لِلْمُؤْمِنِ إِنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فَكَانَ خَيْرًا لَهُ وَإِنْ أَصَابَتْهُ ضَرَّاءُ صَبَرَ فَكَانَ خَيْرًا لَهُ»

“Ajabu ni kwa jambo la muumini. Hakika kila jambo lake kuna kheri na hilo halipatikani kwa yeyote isipokuwa kwa muumini. Akisibiwa na jambo la furaha hushukuru basi huwa ni kheri kwake, na akisibiwa na jambo la madhara husubiri basi huwa ni kheri kwake.”

Pia hakuna kiasi cha ukamataji kitakachoakhirisha mabadiliko ya kweli, yanakuja, Mwenyezi Mungu akipenda. Ni bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Ambayo kwayo tunaweka tegemeo letu.

Mwenyezi Mungu asahilishe hali za ndugu zetu na dada zetu wanyoofu kutoka Ash-Sham!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yasmin Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu