Ijumaa, 25 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  20 Rabi' II 1447 Na: 1447 / 03
M.  Jumapili, 12 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Mirza Ahmadov Miraziz
(Imetafsiriwa)

Kwa huzuni na majonzi makubwa, tunaomboleza kuondokewa na mwana wetu mwengine madhubuti na mchamungu, na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ndugu yetu Mirza Ahmad Mir Aziz alifariki dunia siku ya Ijumaa, 10 Oktoba 2025, na swala ya janaza iliswaliwa kwa ajili yake jana, Jumamosi. Mir Aziz alizaliwa Tashkent mwaka wa 1970. Alikuwa mmoja wa maelfu ya Waislamu wenye ikhlasi na ujasiri ambao waliitikia wito wa Hizb ut Tahrir kwa watu wa Uzbekistan kufanya kazi ya kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu.

Mir Aziz, kama wanaume wengine wengi, alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha muda mrefu gerezani katika umri wake wa makamu chini ya utawala wa kikatili na kandamizi wa dhalimu Karimov. Baada ya karibu miaka 20 jela, mnamo 2025, akiwa na umri wa miaka 55, aliachiliwa huru, karibu kufa, kutokana na mateso makali ya kimwili na kisaikolojia gerezani.

Muumini huyu, ambaye alitumia karibu nusu ya maisha yake katika magereza yaliyotelekezwa, alibaki mwaminifu kwa ahadi aliyoiweka kwa Mwenyezi Mungu. Hakuusujudia utawala wa umwagaji damu wa Karimov, hakuutambua, na hakukubali kitu chengine chochote isipokuwa Khilafah, inayotabikisha sheria za Mwenyezi Mungu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu ndugu yetu Mir Aziz na amjaalie hali njema na amjumuishe miongoni mwa safu za waumini ambao Yeye (swt) amesema juu yao:

[مِنْ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23].

Vile vile tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia na jamaa za ndugu yetu, na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira na uthabiti mzuri. Katika muktadha huu, tunaweza tu kusema:

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ] “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara 2:156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu