- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Kikao cha Majadiliano “Mradi wa Ukombozi... Katika Mizani ya Hukmu za Sheria ya Kiislamu”
Mnamo Jumapili, 12 Oktoba 2025, Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Tunisia iliandaa kikao cha mazungumzo kwa kichwa “Mradi wa Ukombozi... Katika Mizani ya Hukmu za Sheria ya Kiislamu” katika eneo la Kairouan. Kikao hicho kilihudhuriwa na idadi kubwa ya wakaazi wa eneo hilo. Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri alihutubia kipindi kilichofuatia kuanguka kwa Khilafah na jinsi wakoloni walivyounda wanasiasa wachache baada ya kuwashibisha fikra zao zinazotenganisha Uislamu na kiti cha utawala, kama vile utaifa, dola ya Madina na demokrasia. Kisha wakawaweka katika nafasi ambazo kwazo walitekeleza fikra na sheria hizi, ambazo zilikuwa sababu kuu ya hali ya sasa ya nchi ya utegemezi na kurudi nyuma. Alieleza kuwa wakoloni ndio wanaolazimisha sera za nchi, na masuala yote ya taifa, madogo na makubwa, yako mikononi mwa nchi za Magharibi ambazo zimekuwa na bidii ya kutenganisha dini na maisha ya watu. Alimalizia kwa kueleza kwamba Hizb ut Tahrir imechukua mradi wa dola kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake, ambazo ni hukmu za kivitendo, zenye uwezo wa kutabikishwa na kutekelezwa. Ni wajibu kwa Umma kuzitekeleza kwa sababu ni faradhi iliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu juu yake, na ni mradi wa ukombozi wa kweli, halali na unaowezekana.
Ustadh Taher Nasr alihutubia katika uchangiaji wake kwamba nchi za Magharibi ndizo zilizowaleta wanasiasa waliofuatana madarakani ili kutekeleza sheria na fikra zao na kuzuia Uislamu, fikra zake, na sheria zake kuingia madarakani. Alieleza kuwa Uislamu ni seti ya hukmu za kisheria zinazoshughulikia matatizo yote yanayowakabili wanadamu na ni mfumo kamili wa maisha. Vile vile ameeleza kuwa Umma wa Kiislamu na ulimwengu mzima wanatamani na kutafuta mfumo mpya badali ya mfumo huu wa kibepari. Hatimaye, alieleza kuwa matatizo yanayozuia mfumo huu kuingia madarakani yanaweza kutatuliwa iwapo wanaume watasimama, na kupatikana rai jumla juu yake, na wale wenye nguvu na mamlaka kuuingiza madarakani. Hii ndiyo njia ya halali aliyotuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) tuifuate. Kikao kilihitimishwa kwa maswali machache kutoka kwa baadhi ya hadhira.
Kikao hiki ni muendelezo wa semina na mikutano inayoandaliwa na mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia katika ardhi ya Zaytouna ili kujenga rai jumla ya watu kuhusu mradi wa ukombozi wa kweli utakaoutoa Umma kutoka katika masaibu na matatizo yake hadi kwenye uadilifu na rehema ya Uislamu mtukufu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari katika Wilayah ya Tunisia
Jumapili, 20 Rabi' al-Akhir 1447 H sawia na 12 Oktoba 2025 M
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/5065.html#sigProIde8ae2fd3b8
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir