Jumatano, 23 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi ya Ukombozi: “Wito wa Haraka kwa Maafisa na Wanajeshi: Nyinyi ndio wenye Uwezo zaidi wa Kulitokomeza Umbile la Kiyahudi!”

Mnamo Ijumaa, 10 Oktoba 2025, matembezi makubwa yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, kutoka Msikiti wa Al-Fath kufuatia swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kuinusuru Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka ambapo ulinganizi ulielekezwa kwa watu wa Tunisia watoe wito wa haraka kwa maafisa na wanajeshi chini ya kichwa,

“Nyinyi ndio wenye Uwezo zaidi wa Kulitokomeza Umbile la Kiyahudi!”

Wakati wa matembezi hayo yaliohudhuriwa na watu wengi wa Tunisia yalianza kwa takbira, tahlil na Waandamanaji walizunguka barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra, na kuinua mabango bango kuu likiwa limeandikwa kichwa cha maandamano hayo, na mengine yakisomeka, “Kwa mahakama ya kijeshi... Mwachilieni huru mtetezi wa Gaza... Ustadh Mohammed Al-Nasser Shuwaikha.” Maandamano hayo yalihitimishwa mbele ya ukumbi wa maonyesho wa manispaa, ambapo wahudhuriaji waliobarikiwa walikusanyika, wakiimba kauli mbiu za kuwataka maafisa na wanajeshi waaminifu kuwanusuru ndugu zao wanaokandamizwa mjini Gaza. Waliimba kauli mbiu zikiwemo: “Waamerika na Mayahudi... Hakuna mapatano wala maagano,” “Enyi Maafisa na wanajeshi... Mayahudi hawana maagano,” “Enyi Maafisa na askari... Marekani haina maagano,” “Gaza inawaita wanajeshi... Mayahudi hawana maagano,” “Gaza inawaita wanajeshi... Tunataka kuangamizwa Mayahudi,” “Enyi Maafisa na askari... Ni wajibu wetu kuling'oa umbile hilo”, “Enyi majeshi ya Waislamu... tunataka kukombolewa Palestina”, “Enyi maafisa na askari... lengo letu ni kuling'oa umbile.”

Matambezi hayo yalifuatiwa na hotuba iliyotolewa na mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kuhusu ukombozi. Aliyakumbusha majeshi ya Waislamu juu ya vyeo vya aibu vya watawala na usaliti wao kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kuhusu Gaza, pale walipoacha chaguo la vita kwa kufuata mabwana zao. Alieleza kwamba wao, askari wenye ikhlasi, ni watu wa vita na jihad. Alifichua kuwa njama na mpango wa Trump unasubiri kutekelezwa na kufikiwa kwa kile chombo cha vita kimeshindwa kukifikia. Alieleza kwamba Ummah leo unangojea hatua yenu ya kuangamiza umbile la Kiyahudi, huku nyuma yenu kuna jeshi kubwa la Waislamu wanaotafuta ushindi au kuuawa shahidi. Vile vile alieleza kuwa ni nyinyi tu askari mnao uwezo wa kulisaga umbile la Kiyahudi na kuziponya nyoyo za waumini baada ya kuteseka kwa muda mrefu na kusubiri.

Hivyo basi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inaendelea na wito wake kutoka kote ulimwenguni kwa wenye ikhlasi miongoni mwa majeshi ya Ummah ili kuipa nusra Hizb ut Tahrir na kusimamisha jengo kuu la Uislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume iliyoahidiwa kutoka juu ya mbingu saba, ambayo itaokoa watu wa Gaza na kukomboa Bait Al-Maqdis, na kubeba Uislamu kama ujumbe wa uongofu na nuru kwa walimwengu wote (وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ، بِنَصْرِ اللَّهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ) “Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia

Ijumaa, 18 Rabi’ Al-Khair 1447 H sawia na 10 Oktoba 2025 M

- Picha za Amali ya Matembezi -

- Alama Ishara za Amali -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu