Ijumaa, 25 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  21 Rabi' II 1447 Na: H 1447 / 017
M.  Jumatatu, 13 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maadhimisho ya Mwaka wa Pili wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa
Matunda Yaliyonyunyiziwa kwa Damu Safi

(Imetafsiriwa)

Tarehe 7 Oktoba iliadhimisha mwaka wa pili wa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa. Miaka miwili kamili imepita tangu umbile nyakuzi kulenga watu wetu mjini Gaza, likiwafungulia mpangilio wa kuua, kuhamisha, na njaa, na kutumia viwango vya juu vya ushenzi na ukatili dhidi yao. Kwa hivyo ni nini kimebadilika kwa vita hivi vya dhulma?!

Kwanza: Jeshi la Mayahudi lilijionyesha kuwa ni jeshi ambalo haliwezi kushindwa, pamoja na zana zake, vyombo vyake vya kijeshi na vya kijasusi, na ubora wake juu ya watu wa Palestina na majeshi ya nchi zinazowazunguka katika miongo kadhaa iliyopita. Kisha ikaja Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya kufuta sura hii kutoka kwa uwepo, kufichua uongo wake, na kuthibitisha kwamba ni umbile dhaifu kuliko utandu wa buibui, na kwamba majambazi wake ni wachache tu wa watu waoga, wadhalilifu. Kama sio usaidizi wa serikali jirani na usaidizi wa Marekani, lingekuwa limefutiliwa mbali katika ardhi kitambo.

Watu wachache kutoka Gaza walisugua pua za Mayahudi kwenye uchafu. Walipenyeza katika maeneo yaliyokuwa chini ya udhibiti wao, wakakamata vifaru, wakawakamata wanajeshi, na kufanya mashambulizi ya parwanja. Lilikuwa ni pigo chungu lililowadhalilisha mbele ya walimwengu na kufichua uongo wa tawala za khiyana zilizodai kutokuwa na uwezo na ukosefu wa nguvu za kumshinda mporaji huyu.

Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa itasalia kuwa ushahidi wa kushindwa kwa tawala na majeshi yao kuwanusuru ndugu zao, na madai yao ya uongo kwamba hawana uwezo. Tofauti iliyoje kati ya silaha na zana walizonazo Mujahidina na wanazomiliki majeshi! Na tofauti iliyoje kati ya wale waliosikia kilio cha wanawake waliofiwa na kukimbilia kuitikia, na wale waliosikia na kuziba masikio yao!

Pili: Operesheni hii ilifichua yale yaliyokuwa yamefichwa kutoka kwa ulimwengu ya unafiki wa wale wanaodai kutetea haki za binadamu, haki za wanawake, uhuru, nk. Ilifichua pengo kubwa kati ya mazungumzo ya Magharibi na kauli mbiu zake tupu, na kushiriki kwake katika kuwaua watu wasio na hatia na kuupa uvamizi huo silaha.

Dunia nzima iliona sura halisi ya yule anayeitwa “mlinzi wa maadili ya kibinadamu” na mashirika ya haki za wanawake na watoto yaliyoanzishwa na “walinzi wa haki na uhuru!” Wote walikaa kimya cha aibu huku wakishuhudia mauaji dhidi ya wanawake na watoto wa Gaza. Walipuuza sheria za kimataifa, mikataba ya wanawake, mikataba ya haki za binadamu, na madai yao yote ya kiburi, kwa hivyo barakoa ilivuliwa shukrani kwa hili kwa watu waheshimiwa duniani kote.

Maafa ya watu wa Gaza yalichochea watu wengi kuingia mabarabarani katika maandamano kwa mamilioni yasiyo na kifani katika miji kadhaa mikuu ya dunia, wakielezea kupinga kwao jinai za uvamizi huo, na kukaidi sheria na vikwazo vilivyowekwa juu yao na nchi zao. Pamoja na hayo yote, vita dhidi ya Gaza vilikuwa ni ufichuzi wa mfumo danganyifu wa kilimwengu na dhihirisho la pengo kubwa kati ya tawala za uhalifu zenye mikono iliyolowa damu ya watu wa Gaza na watu waliokataa na kulaani uhalifu ambao hata wanyama wangeuepuka.

Ubaya wa jinai za kivita mjini Gaza ulichangia kuunda mwamko mpya wa kimataifa wa kukataa udhalimu wa Magharibi katika kubainisha wema na ovu na kukataa unafiki wa binadamu. Dalili za mabadiliko haya zilionekana katika harakati za kususia, maandamano, na majaribio ya kuvunja mzingiro karibu na Gaza.

Tatu: Wanawake wa Gaza, licha ya maafa yao makubwa, waliwasilisha kwa ulimwengu wote katika miaka hii miwili mfano unaong'aa wa mwanamke Muislamu mvumilivu, dhabiti. Wanawake wengi wa Kimagharibi walipigwa na butwaa kwa ustahamilivu na uthabiti wao walipokuwa wakimuaga shahidi baada ya shahidi kutoka miongoni mwa wana, waume, na familia zao.

Makhansa wa zama hizi waliweza kuakisi athari za imani ya Kiislamu katika nafsi zao na tabia zao, kuthibitisha uhalisia kwamba hawatalainika wala hawatasalimu amri, na kwamba daima watabaki kuwa kiwanda cha mashujaa na kizazi cha wanaume, wakiendelea kujitolea mhanga na kutoa hadi pale Palestina itakapokombolewa kutoka mtoni hadi baharini, na hawatashuka kabla ya kufikia lengo hilo.

Wengi wa wanawake wa Gaza wanatambua kwamba suluhisho la dola mbili, lililoitishwa na Marekani na nyuma yake dola za Kiarabu, ni kufilisiwa kwa kadhia hiyo, na kwamba mihanga iliyotolewa lazima inyanyue shingo juu kuelekea ukombozi kamili wa kweli ambao unairegesha ardhi iliyonyakuliwa na kulishinda kabisa umbile la Kiyahudi.

Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azigeuze njama za maadui dhidi yao wenyewe, auandalie Ummah uongofu, aziunganishe safu zake, ili kadhia ya Palestina irudi kwenye asili yake, na majeshi yake yainuke kujibu kilio cha waliofiwa, kulipiza kisasi kwa wavamizi, na kuponya vifua vya waumini. Hakika Yeye ndiye Mlinzi wake na Muweza juu yake.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
hizb-uttahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-uttahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu