Alhamisi, 12 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  8 Rabi' I 1447 Na: Afg. 1447 H / 03
M.  Jumapili, 31 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwisho wa Uvamizi wa Kijeshi wa Marekani na NATO: Fursa ya Kukabiliana na Ukoloni Laini na Hatua ya Kuelekea Khilafah kwa Njia ya Utume!
(Imetafsiriwa)

Miaka minne iliyopita, mnamo 31 Agosti 2021, uvamizi wa kijeshi wa miongo miwili wa Afghanistan na vikosi vya Amerika na NATO ulimalizika, kwani mwanajeshi wa mwisho wa Amerika aliondoka nchi humu usiku wa manane. Hii ilikuwa hasa kwa sababu ya mhimili wa Wamarekani kuelekea Indo-pacifiki, kupunguza kasi ya maendeleo ya China. Nchi za Kiislamu, hususan Mujahidina wa Afghanistan walikuwa wamewaumiza kichwa Wamarekani na kukengeushwa na mkakati huu mpya. Tunatoa pongezi zetu kwa mafanikio haya ya kihistoria na siku kuu kwa Waislamu wote, hasa kwa watu wa Afghanistan, wabebaji Dawah, na Mujahidina.

Miaka hii minne ingeweza kuwa fursa ya kihistoria kwa utabikishaji kamili wa Uislamu na mwanzo wa mabadiliko makubwa nchini Afghanistan. Kama vile Dola ya Kiislamu mjini Madina, ndani ya miaka yake minne ya mwanzo, iliweka misingi ya Ummah, ilifafanua kanuni za wazi za sera ya ndani na nje ya nchi, na kuanzisha uwepo wa Uislamu kwenye jukwaa la kimataifa. Mfumo wa utawala nchini Afghanistan, pia, ungeweza kutumia nyakati hizi muhimu kutengeneza mfumo wa wazi na wa kipekee wa sera zake za ndani na nje, kutabikisha Uislamu si kama kauli mbiu, bali kama mfumo mpana na mtindo wa maisha katika utawala, uchumi, elimu, mahakama na mambo ya nje.

Walakini, cha kusikitisha, fursa hii nzuri haikutumiwa ipasavyo. Badala ya utabikishaji kamili, Uislamu umetekelezwa kwa kuchagua na hatua kwa hatua kwa msingi wa upendeleo wa kibinafsi na ndani ya mifumo iliyorithiwa kutoka kwa utawala wa jamhuri uliopita na muundo wa dola ya kisasa ya kitaifa. Matokeo yake, hakuna sifa za wazi au bainifu za dola ya Kiislamu zimeainishwa; sera ya mambo ya nje haijaegemezwa katika Dawah na Jihad; na Umma haujashuhudia dalili za mabadiliko ya kweli ya Kiislamu nchini Afghanistan. Kinyume chake, mwelekeo umehamia kufikia utulivu wa ndani ndani ya mipaka ya kitaifa, kutafuta kutambuliwa kutoka kwa mfumo wa kimataifa, na kusawazisha kati ya dola za kimataifa – mwelekeo ambao, hatimaye, inadhoofisha uhalali wa mfumo.

Ijapokuwa uvamizi wa kijeshi umekwisha, ukoloni laini unasalia kuwapo kila wakati, aina ya ujanja zaidi ya utawala ambayo hupenya siasa, uchumi na fikra. Inatiisha mataifa kutoka ndani, bila kelele za vita au uvamizi wa kijeshi. Aina hii ya ukoloni inatoa udanganyifu wa uhuru, inahujumu utashi wa Ummah, na kuzuia utabikishaji kamili wa Uislamu. Uzoefu wa kihistoria unaonyesha kwamba mataifa mara nyingi hushushwa na nguvu laini kuliko kwa nguvu za kijeshi. Kwa hiyo, kukabiliana na changamoto hii kunahitaji umakini, mwamko wa kisiasa, kufukuzwa kwa Mashirika ya kigeni yasiyo ya Kiserikali (NGOs) na balozi za kigeni, na kushikamana kikamilifu na Uislamu.

Kwa kumalizia, tunawakumbusha kwa dhati ndugu zetu mujahidina kwamba fursa bado haijapotea. Fursa zilizopo lazima zichukuliwe kwa busara, na ushindi huu wa kihistoria lazima ugeuzwe kuwa daraja la kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Khilafah inayounganisha Ummah, inayoung'oa ukoloni, na kubeba ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu. Vyenginevyo, kuna hofu ya kweli kwamba faida za leo zinaweza kupotea. Sawa na siku za nyuma, Afghanistan inaweza kwa mara nyingine tena kuanguka katika dimbwi la ukoloni na udhaifu.

Kama alivyoonya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ]

“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Surah Muhammad: 38].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu