- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mchezo wa Idadi nchini Malaysia
(Imetafsiriwa)
Habari:
Waziri Mkuu wa Malaysia aliye katika mvutano Muhyiddin Yassin mnamo Jumatano alisisitiza kuwa angali ana uungwaji mkono unaohitajika kuongoza nchi baada ya wanachama wa mshirika wake mkuu wa muungano kusema hawatamuunga mkono tena kufuatia ukemeaji nadra kutoka kwa mfalme, katika mvutano wa kisiasa unaoendelea katikati ya uongezeko la janga la virusi vya korona.
Muhyiddin, ambaye utawala wake dhaifu wa Perikatan Nasional umekuwa chini ya shinikizo kila wakati tangu alipoteuliwa kuwa waziri mkuu mnamo Machi 2020, alisema katika hotuba ya televisheni kuwa bado anaungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge 222 wa nchi hiyo na kwamba uhalali wake wa kuongoza utapimwa mara tu bunge litakapokutana tena mwezi ujao. (Chanzo: Aljazeera.com)
Maoni:
Demokrasia imefeli. Na hata ni hatari. Inaiweka jamii mikononi mwa wanasiasa wa kujigamba, na kulianika taifa kwa unyonyaji na hatari ya kigeni. Umekuwa ni 'mlango wazi' unaopendwa wa kuziingilia kati serikali za kimabavu, na waendeshaji vikaragosi wakoloni mamboleo. Uilize tu Malaysia.
Demokrasia huwaingiza wakoloni mamboleo. Kuna ushahidi kwamba serikali za kigeni zinaunga mkono na kuratibu pamoja na wanasiasa wa upinzani na mashirika 'huru' yasiyo ya kiserikali. Upinzani huu, ni muungano wa kibiashara wa urahisi, na sio wa kimaadili. Wanatoka pande tofauti za ramani ya kimfumo. Wabaguzi wa rangi na maadui wa Uislamu wanalala kitanda kimoja na wazalendo wa Kimalay na waliberali. Hakuna ruwaza mbadala, maadili mpya. Hakuna njia mpya. Hakuna chochote. Hakika uwepo wa muungano kama huo unasaliti udanganyifu ulio kinyume na maadili, na nia ya kuacha maadili yote. Maadui hawa wa zamani wanashirikiana kuiondoa serikali ambayo tayari imeshiriki pakubwa pande mbili: kindani - dhidi ya virusi aina ya Indian Delta, na kinje, 'kudhibiti' uvamizi wa jumla wa China wa bahari zake na rasilimali za hydrocarbon.
Amerika inafaidika ikiwa watafaulu kupandikiza vibaraka wao. China inafaidika kutokana na taifa dhaifu, la kioga la ASEAN.
Demokrasia inauweka 'upinzani', kinyume na ustawi wa watu. Malaysia inahitaji upinzani imara, unaolenga kupambana na Covid na kuwaokoa watu na uchumi. Lakini, upinzani huo lazima uzalishe machafuko. Kwani ikiwa serikali itafanikiwa kudhibiti virusi aina ya Indian Delta, (na ni serikali chache sana zimeweza, hata zile zenye mpango wa chanjo) unyakuzi wa mamlaka wa upinzani unaweza kupoteza mvuke.
Wanasiasa wa upinzani wa Amerika, pia wameingiza siasa katika Covid, kwa hasara ya watu wao na watoto wao wenyewe.
Kwa nini demokrasia ina kasoro? Kwa sababu inachanganya haki na uwezo wa kuchagua kiongozi, na uwezo na mamlaka ya kutunga sheria za maisha na jamii. Kila mtu anapiga kura kwa maslahi yake ya ubinafsi. Nchi za kidemokrasia ambazo hazijadhibitiwa husonga mbele kuelekea muono mfupi, kujiridhisha nyezo kibinafsi. Kwa sababu tu tunapenda au tunataka kitu, haimaanishi kuwa ni kizuri kwa mtu binafsi au jamii.
Mnamo 2017, Trump, mtu mrongo, mbaguzi wa rangi, anayepinga Uislamu na anayedaiwa kuwa mkwepaji ushuru, alikuwa rais aliyechaguliwa kihalali wa nchi ya kidemokrasia yenye nguvu zaidi, tajiri na iliyo na uhusiano duniani. Na licha ya kushindwa, bado angali ana ushawishi kwa karibu nusu ya wapiga kura wa Amerika.
Chuki, hofu, na ubaguzi wa rangi huuza. Katika nchi za kidemokrasia, uhalisia na ukweli hushawishiwa. Zuri na baya, sawa na kosa, hubadilishwa. Haishangazi nchi za kidemokrasia zenye 'huria na uangavu' huzaa ujinga na ufashisti, na ndizo zenye baadhi ya serikali zisizo na uvumilivu, zenye unafiki, zenye ukoloni mamboleo zaidi ulimwenguni. Usekula wa kiliberali unaozea ndani kwa ndani.
Uislamu una njia bora. Haitumii uwongo, ushabiki na chuki. Uislamu unatofautisha uchaguzi wa kiongozi mzuri na uwekaji wa kanuni na sheria ambazo zinadhibiti taifa lenye haki na maendeleo. Hauruhusu hata uchafu wa ufisadi au uingiliaji wa dola za kiadui. Mfumo wa kipekee wa utawala wa Kiislamu na mchakato wa uchaguzi wa Amir ul-Mu’mineen unahakikisha uongozi mmoja wenye thabiti na nguvu kwa Umma mzima na raia wote bila kujali rangi au dini.
Pamoja na majanga yote ambayo tayari tunakabiliwa nayo mikononi mwa wakoloni mamboleo, hatuwezi kukubali kuchukuliwa na mfumo wao wa machafuko na uliovunjika. Haufai kwa taifa lolote, sembuse Umma wa Kiislamu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Hamzah