Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Mabrouk Ben Nasser
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inaomboleza kwa huzuni na majonzi makubwa kuondokewa na ndugu yetu Mabrouk Ben Nasser, aliyefariki siku ya Alhamisi, 23 Dhu al-Hijjah, 1446 H, sawia na 19 Juni 2025 M. Alikuwa mmoja wa Mashababu (wanachama) wa Hizb ut Tahrir ambao walifanya kazi ndani ya safu zake wakati wa nyakati za giza za dhulma na ukandamizaji, akiwa amezuiliwa kwenye jela za Bourguiba na kisha Ben Ali. Alitumia muda wake kwa subira na imani, akiendelea kushikamana na ulinganizi wake na kujitolea kuubeba, akilingania Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.