Jumatano, 29 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  24 Dhu al-Hijjah 1446 Na: H 1446 / 49
M.  Ijumaa, 20 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni kutokana na Usaliti wa Watawala Vibaraka wa Ulimwengu wa Kiislamu ambapo Wakatili Wawili wa Amerika - Umbile la Kiyahudi katika Ardhi za Kiarabu na India ya Hindutva huko Asia Kusini - wanaonyesha Kusubutu kwao Kukiuka Ubwana wa Ardhi za Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, leo (Juni 20, 2025) Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa, iliandaa maandamano katika misikiti mbalimbali ya Dhaka na Chittagong kupinga kuendelea kwa mauaji ya halaiki huko Gaza ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kwa chakula na shambulizi dhidi ya Iran na umbile nyakuzi la kiyahudi. Mukhtasari wa hotuba zilizotolewa katika mkutano huo umetolewa hapa chini:

Kwa kupuuza hasira, chuki na dhamiri za walimwengu, kwa uungwaji mkono wa moja kwa moja wa Marekani, umbile la Kiyahudi lililolaaniwa limekuwa likitekeleza mauaji ya kikatili zaidi katika historia dhidi ya Waislamu huko Gaza kwa muda wa miezi 20 iliyopita; nyumba na hospitali zimebomolewa, waandishi wa habari wasiohesabika, madaktari na wafanyikazi wa misaada wameuawa. Katikati ya mzingiro unaoendelea, ili kusababisha njaa bandia huko Gaza, misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na chakula imesimamishwa kwa makusudi, na kwa jina la kusambaza misaada, wananchi wa Gaza wenye njaa wamekusanywa na kuuawa kwa kupigwa risasi. Maandamano ya Waislamu duniani kote na wito kwa jeshi kuwakomboa Waislamu wa Gaza, au matembezi ya Rafah ya mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani hayajaweza kuwashawishi hata kidogo watawala wahalifu wa Waislamu wa nchi za Kiarabu zinazozunguka umbile la Kiyahudi. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَهُمْ قُلُوبٌ لَا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَا يَسْمَعُونَ بِهَا أُولَٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ]

Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. [Surah Al-A’raf: 179].

Khiyana ya watawala vibaraka wa ulimwengu wa Kiislamu imezidisha ushupavu wa Marekani, na Wamarekani wanapanua vita vyao dhidi ya Waislamu. Hakika mumeshuhudia kwamba ndege za kivita za wanyakuzi ‘Waisraeli’ zilivuka anga za watawala wa nchi za Kiislamu, zikaishambulia Iran, zikafanya uharibifu na kuua, na zikaregea salama. Hakuna hata mtawala yoyote wa Syria, Iraq, Misri, Uturuki, au watawala walioizunguka aliyefyatua risasi hata moja dhidi ya ndege hizi! Kwa upande mwingine, mtawala khaini wa Jordan aliyatungua makombora ambayo Iran ilirusha kwa mnyakuzi 'Israel' katika anga yake, ikifanya kama ngao kwa umbile la Kiyahudi. Walishambulia na kurudi, huku watawala wa nchi za Kiislamu wakitazama kama watazamaji kimya. Watawala hawa walisahau—au walipuuza kimakusudi—matokeo mabaya ya kutochukua hatua huku.

Marekani imewapa jukumu umbile la Kiyahudi lililolaaniwa katika nchi za Kiarabu na dola ya Hindutva ya India huko Asia dhidi ya Waislamu. Kwa sababu wanajua kwamba hawa Mayahudi na washirikina ni maadui wa milele wa Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا]

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. [Surah Al-Ma’idah: 82]. Wakati vikosi vya majeshi ya Kiislamu vilipochukua nafasi ya mbele katika kuwashinda makafiri hao dhaifu na wafisadi na Umma wa Kiislamu ukasherehekea ushindi wake, hapo watawala vibaraka kwa upatanishi wa Marekani, walisimamisha vita na kuvuta hatamu za kijeshi ili kuushinda Umma wa Kiislamu. Trump ana udhibiti na imani kiasi gani juu ya watawala hawa vibaraka ambao anaweza kuchapisha kwenye jukwaa lake la kijamii la Truth akisema, "Iran na Israel zinapaswa kufikia makubaliano na watafikia, kama vile nilivyolazimisha India na Pakistan kufikia makubaliano ... na pia alisema: Vile vile, amani itaanzishwa hivi karibuni kati ya Israel na Iran, simu na mikutano mingi inaendelea kwa sasa" [Sky News, 15/6/2025].

Sura ya halisi ya vibaraka wa wakoloni wa Magharibi imefichuliwa kwa Umma wa Kiislamu. Umma wa Kiislamu duniani kote unawalingania watoto wake wa kiume wenye ikhlasi wanaohudumu katika jeshi ili kuikomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, ikiwemo Arakan-Kashmir, kutokana na kukaliwa kwa mabavu kinyume cha sheria, na pia wanaitikia wito wa Umma wa Kiislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»“Hakika Imam (Khalifa) ni ngao (kamanda) ambayo Waislamu hupigana nyuma yake na kujihami kwaye” [Sahih Muslim]. Khalifa pekee ndiye kamanda wa Umma wa Kiislamu, ambaye chini ya uongozi wake jeshi la Waislamu litakata mikono ya mkoloni kafiri Amerika, kwa kupinga umbile la Kiyahudi na Hindutva India, Insha’Allah. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَا يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِن يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ]

Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. [Surah Aali-Imran: 111]. Zaidi ya yote, wito wetu kwenu kwa niaba ya Hizb ut Tahrir ni kuungana katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, dola yenye nguvu ya Umma wa Kiislamu, na kuwahimiza wana wenu wanaofanya kazi ndani ya jeshi kutoa nusrah (nguvu) kwa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah.

[فِي بِضْعِ سِنِينَ لِلَّهِ الأَمْرُ مِنْ قَبْلُ وَمِنْ بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. [Surah Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu