Enyi Watu wa Sudan, Mnaweza Kutibua Mpango wa Kuitenga Darfur, Basi Inukeni Kumtii Mwenyezi Mungu!
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Katika hatua inayotarajiwa, kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Mohamed Hamdan Dagalo, alikula kiapo cha kikatiba kama mkuu wa Baraza la Rais la kile kinachoitwa serikali sambamba huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, mnamo Jumamosi, 30/8/2025. Makamu wa Rais, wajumbe wa Baraza la Rais, na Waziri Mkuu pia walikula kiapo.