Mpango wa Mipaka ya Damu na Uhalifu wa Kujitenga kwa Darfur
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Baada ya kuanguka kwa kutia shaka kwa miji mikubwa ya Darfur, na kuondolewa kwa jeshi kutoka kwao, mbele ya utekaji nyara wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), pamoja na kuzingirwa kwa nguvu na vikosi hivi katika jimbo la mwisho lililosalia, Darfur Kaskazini na mji mkuu wake, Al-Fashir, wakati jeshi likishindwa kuwafukuza, ghafula yanakuja mazungumzo ya serikali sambamba yakiongozwa nao huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, ambao wanaudhibiti, kwa ushiriki wa vibaraka wa Amerika kama vile Al-Hilu, na uungaji mkono wake kwa serikali hii, hata kuwa naibu ndani yake.