Kinachoitwa “Tamasha za Hisia” (Zambo) jijini Tripoli ni Jaribio la Kulionyesha Jiji lisilo na Hisia zake kwa Ummah Kwa hivyo Zisusieni na Komesheni utoaji Leseni Kwazo!
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Kwa ukaidi wa wazi wa hisia za Umma na maumivu yake, na kwa ukaidi wa wazi wa Tripoli, jiji la elimu na wanazuoni, na licha ya kutolewa kwa tamko kutoka kwa Kamati ya Utunzaji wa Familia katika Dar al-Fatwa jijini Tripoli na Kaskazini kuonya juu ya njia hii hatari kwa jamii, ambapo ilikuja katika taarifa: “Kamati pia inatahadharisha juu ya hatari ya tamasha, sherehe, filamu, na mipango ambayo imejitokeza hivi karibuni katika jiji letu na ambayo yanaathiri maadili na akhlaki, na ambayo hutumiwa kupitisha ujumbe potovu chini ya kauli mbiu za kisanii au kithaqafa, katika jiji linalojulikana katika historia yake kama jiji la elimu na wanazuoni, na kama ngome ya maadili ya kweli na kitambulisho kinachounganisha. Kamati inasisitiza kwamba kuilinda jamii kutokana na hatari ni jukumu tunaloshirikiana pamoja: linaanza na familia na jamaa, kwenda hadi kwa walimu, na wanazuoni, na pia linajumuisha asasi za kiraia, manispaa, na wanasiasa, kufikia hadi kwa watoa maamuzi katika ngazi ya serikali…”