Ijumaa, 20 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Tarehe 5 Agosti 2024 ni Siku ya Uasi wa Watu dhidi ya Dhalimu na Utawala wa Kidhalimu, ambao ungali Unaendelea; kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni Hati ya Usaliti wa Vyama vya Kisiasa vinavyounga mkono Marekani ili kuangamiza Uasi wa Watu

Wananchi wakiwa wamekata tamaa sana, wamepita mwaka mmoja tangu kuanguka kwa Hasina katika uasi mkubwa dhidi ya dhalimu Hasina na utawala dhalimu mnamo Agosti 5, 2025. Kwa sababu baada ya kuanguka kwa dhalimu Hasina, vibaraka wa Marekani na vyama vya kisiasa vyenye uchu wa madaraka vimechukua mshiko wa kubainisha hatima ya watu na kuweka vikwazo katika kutekeleza matumaini na matarajio ya watu na wameendelea na majaribio yao maovu na kuteka nyara uasi huo. Kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni hatua isiyo na aibu ya jaribio hili ovu. Watu wamekataa utumwa wa Marekani na sarakasi za kisiasa kwa chuki. Yaliyo mbali na kuakisi matarajio ya watu, Tangazo hili la Julai halitambui hata matukio kama vile njama ya India huko Pilkhana na mauaji ya halaiki ya watu wanaopenda Uislamu huko Shapla Chattar.

Ni Lazima ikumbukwe kwamba Marekani ni Nchi ya Kikoloni; Kujisalimisha kwa Sera zake za Ushuru Kutahatarisha Ubwana wa Taifa!

Marekani, mchuuzi wa kimataifa wa ubepari, imeibua 'dhoruba ya ushuru' duniani kote, ikipuuza kanuni za uchumi wa soko huria – moja ya falsafa kuu za ubepari – na sheria na kanuni za kile kinachojulikana kama Shirika la Biashara Duniani (WTO) ililounda. Hii, kwa mara nyingine, inathibitisha kwamba mfumo wa kibepari hauna utu na wa kinyonyaji. Serikali ya mpito ya Bangladesh imetabanni sera ya utiifu katika kukabiliana na hatua za ushuru za Marekani. Tayari wamefanya uamuzi wa kujitoa mhanga kununua ndege 25 za gharama kubwa aina ya Boeing, pamoja na kuagiza pamba na LNG kutoka Marekani, ingawa nchi nyingi zinaghairi oda zao kutokana na utendakazi duni wa Boeing. Na wanafanya mikutano ya moja kwa moja na Marekani, wakiweka umma katika giza kupitia 'makubaliano fiche ya kihistoria' (NDA).

Sudan: Janga la Karne Lililofichika Machoni mwa Ulimwengu

Dola ya Kiislamu, mlinzi wa watu wake, haipo. Waislamu wameishi katika taabu, mateso, na majanga duniani kote. Sudan hivi sasa inakabiliwa na moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu katika historia ya kisasa kutokana na mapigano ya umwagaji damu ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili kati ya jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), na kusababisha maafa ya kutisha ambayo hakuna anayezungumza au kujaribu kuzuia. Huu ni mzozo uliosahaulika ambao vyombo vya habari haviupi mwanga, na ambao maelezo yake hayafichuliwi na dola yoyote au hata taasisi zake.

Mbwa Mwitu Hapaswi Kulaumiwa kwa Uvamizi wake ikiwa Mchungaji ndiye Adui wa Kondoo

Watoto watatu walifariki katika Jimbo la Khartoum baada ya kupokea dozi ya chanjo ya ukambi. Wizara ya Afya imefungua uchunguzi kuhusu dhurufu za vifo vyao. Sudan Tribune iligundua kuwa watoto wawili walikufa ndani ya saa moja baada ya kupokea chanjo ya ukambi, huku mtoto wa tatu akifa siku tisa baada ya kusaidiwa kupumua katika Hospitali ya Al-Balak mjini Omdurman. (Sudan Tribune, Agosti 5, 2025)

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu