Ijumaa, 20 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Al-Waqiyah TV: Kwa Nini Kuwahisabu Watawala ni Faradhi ya Kisheria

Unapomteua mtu wa kutekeleza jukumu ambalo asili yake ulikabidhiwa, hii ina maana kwamba ni wajibu wako wa Shariah kumfuatilia na kumhisabu ikiwa ameghafilika, anafanya makosa, au anadhulumu, na kadhalika. Ni jambo la kawaida kwa Ummah kuendelea kuwa macho juu ya mtawala. Haya ni faradhi yake ya Shariah na Shariah yake kwa wakati mmoja. Maana ya faradhi yake ya Shariah ni kuwa Ummah utakuwa ni wenye dhambi ukilipuuza hili. Haki yake Shariah ni kwamba mtawala atatenda dhambi ikiwa atauzuia kutekeleza wajibu wa kuhisabu, ufuatiliaji, na ushauri, na kadhalika.

Wakati Mahouthi Wakishangilia Uhamasishaji wa Makabila ya Bakil na Hashid na Kupigwa kwa Ngoma za Vita Baina Yao!

Mnamo Jumamosi, 26/07/2025, Sheikh Hamid Mansour Radman aliuawa katika eneo la Al-Hayit, Wilaya ya Ayal Surayh, katika Mkoa wa Amran, na mkwe wake, Hamir Saleh Rattas Falyatah (Abu Udhr) mkuu wa idara ya polisi ya Al-Hayit. Mauaji ya Sheikh Radman yalikuja baada ya kuondoka nyumbani kwake, kufuatia mzozo wa kifamilia. Muuaji anashikilia wadhifa wa mkuu wa idara ya polisi, ambaye wajibu wake ni kulinda maisha, mali, na heshima, na kuhakikisha faraja na usalama wa jamii, kuondoa shida zake, kudumisha amani kote, na kuwazuia wakjukaji na wavamizi dhidi ya maisha ya watu – sio kumuua bamkwe wake kwa kukusudia kwa kumpiga risasi kwenye barabara ya umma!

Tarehe 5 Agosti 2024 ni Siku ya Uasi wa Watu dhidi ya Dhalimu na Utawala wa Kidhalimu, ambao ungali Unaendelea; kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni Hati ya Usaliti wa Vyama vya Kisiasa vinavyounga mkono Marekani ili kuangamiza Uasi wa Watu

Wananchi wakiwa wamekata tamaa sana, wamepita mwaka mmoja tangu kuanguka kwa Hasina katika uasi mkubwa dhidi ya dhalimu Hasina na utawala dhalimu mnamo Agosti 5, 2025. Kwa sababu baada ya kuanguka kwa dhalimu Hasina, vibaraka wa Marekani na vyama vya kisiasa vyenye uchu wa madaraka vimechukua mshiko wa kubainisha hatima ya watu na kuweka vikwazo katika kutekeleza matumaini na matarajio ya watu na wameendelea na majaribio yao maovu na kuteka nyara uasi huo. Kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni hatua isiyo na aibu ya jaribio hili ovu. Watu wamekataa utumwa wa Marekani na sarakasi za kisiasa kwa chuki. Yaliyo mbali na kuakisi matarajio ya watu, Tangazo hili la Julai halitambui hata matukio kama vile njama ya India huko Pilkhana na mauaji ya halaiki ya watu wanaopenda Uislamu huko Shapla Chattar.

Ni Lazima ikumbukwe kwamba Marekani ni Nchi ya Kikoloni; Kujisalimisha kwa Sera zake za Ushuru Kutahatarisha Ubwana wa Taifa!

Marekani, mchuuzi wa kimataifa wa ubepari, imeibua 'dhoruba ya ushuru' duniani kote, ikipuuza kanuni za uchumi wa soko huria – moja ya falsafa kuu za ubepari – na sheria na kanuni za kile kinachojulikana kama Shirika la Biashara Duniani (WTO) ililounda. Hii, kwa mara nyingine, inathibitisha kwamba mfumo wa kibepari hauna utu na wa kinyonyaji. Serikali ya mpito ya Bangladesh imetabanni sera ya utiifu katika kukabiliana na hatua za ushuru za Marekani. Tayari wamefanya uamuzi wa kujitoa mhanga kununua ndege 25 za gharama kubwa aina ya Boeing, pamoja na kuagiza pamba na LNG kutoka Marekani, ingawa nchi nyingi zinaghairi oda zao kutokana na utendakazi duni wa Boeing. Na wanafanya mikutano ya moja kwa moja na Marekani, wakiweka umma katika giza kupitia 'makubaliano fiche ya kihistoria' (NDA).

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu