Ijumaa, 20 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Enyi Waislamu: Je, bado mna matumaini kwa Watawala wenu Ruwaibidha?!

Umbile la Kiyahudi bado linatekeleza uhalifu wake dhidi ya watu wa Gaza, hivyo makumi ya mashahidi huongezeka kutokana nao kila siku. Pia bado linapiga mzingiro wake juu ya Gaza, hivyo watu wake wanakufa kwa njaa, kwa kuwa hawana chakula, vinywaji, dawa, au makao, licha ya jitihada fulani za kupeleka misaada kwao kwa uoga! Lakini mamia ya maelfu hawapati tonge ambalo kwalo wanaweza kuzuia njaa zao au kunyamazisha njaa ya watoto wao, kwa hiyo wamekuwa wanakufa kwa njaa mbele yao na mbele ya macho ya ulimwengu wote bila msaidizi au mwenye kuwanusuru.

Sio Taarifa ya Bogotá wala Tangazo la New York litaweza kuliokoa umbile la Kiyahudi!

Wakati sera ya mauaji ya halaiki na njaa huko Gaza ikiendelea huku ukatili wake wote ukionekana na kusikilizwa na dunia nzima, Uturuki vile vile, inaendelea na hatua zake rasmi za kukabiliana na ongezeko la misimamo ya rai jumla nchini Uturuki. Hata hivyo, haikutia saini taarifa iliyotayarishwa na The Hague Group huko Bogotá, mji mkuu wa Colombia, Julai 15–16. Lakini katika kujibu majibu hayo, Wizara ya Mambo ya Nje ilidai kuwa taarifa hiyo huenda ikatiwa saini hadi Septemba 20, na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan alitangaza kuwa wana dukuduku katika muktadha wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari.

Mkataba wa Gesi na Umbile la Kiyahudi Ununuzi wa Utajiri wetu ulioibiwa na Msaada kwa Adui yetu Mnyakuzi

Katika kitendo kipya kinachojumuisha kiwango cha mporomoko na ubaraka ambao utawala wa Misri umefikia, ilitangaza kusainiwa kwa makubaliano makubwa na umbile la Kiyahudi ya kuagiza gesi asilia kutoka kwa uwanja wa Leviathan katika ardhi iliyonyakuliwa ya Palestina, kwa thamani inayokaribia dolari bilioni 35 hadi mwaka wa 2040. Chini yake, umbile la Kiyahudi linauza nje ya nchi karibu mita za ujazo 130 za gesi nchini Misiri, kutumika kukidhi mahitaji ya ndani na kusafirisha nje kupitia vituo vya kutengeneza gesi vya Misri. Makubaliano haya yamepigiwa debe kama "kuimarisha usalama wa nishati," huku kiuhalisia yakiwa ni usaliti kwa Ummah, kupuuza utajiri wake, muungano na adui yake, na msaada kwa uchumi wake unaodhoofika.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu