Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kitengo cha Wanawake: Kampeni "Mgogoro wa Mazingira: Sababu na Masuluhisho ya Kiislamu"


Wiki hii, mawaziri na wanadiplomasia kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanakusanyika mjini Glasgow kwa ajili ya Kongamano la 26 la Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, linalolenga kutibu kile ambacho wengi wamekitaja kuwa "dharura ya hali ya hewa" inayoikabili sayari ya dunia. Katika ajenda ni mipango ya kupunguza uzalishaji mkubwa wa gesi chafu duniani kama vile carbon dioxide, inayosababishwa zaidi na uchomaji wa nishati ya mafuta na ukataji miti kwa kiasi kikubwa. Hii inasemekana kusababisha ongezeko la wastani la hali ya joto duniani na kupelekea kuongezeka kwa kasi na ukubwa wa matukio ya hali ya hewa kali kama vile mawimbi ya joto, ukame na mafuriko pamoja na moto wa nyika. Suluhu zilizopendekezwa ni pamoja na kuondoa migodi ya makaa ya mawe, kuongeza uwekezaji katika nishati mbadala, kubadilisha miundo ya umeme na magari ya petroli, na kuongeza ufadhili wa kusaidia mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi mbalimbali. Hata hivyo, mabadiliko ya hali ya hewa ni sehemu tu ya majanga ya kimazingira yanayokumba sehemu nyingi za dunia hivi sasa, haswa mataifa maskini zaidi. Uharibifu wa mazingira, kutoweka kwa aina mbalimbali za wanyama, mmomonyoko wa udongo na uchafuzi wa mazingira, uchafuzi wa mito na bahari na takataka zenye sumu, na utupaji wa tani za plastiki, nguo na taka nyinginezo ni mifano michache tu ya matatizo yanayoathiri ardhi kote duniani. Uharibifu huo wa mazingira na majanga yana gharama kubwa ya kibinadamu, inayoathiri afya ya watu, kusababisha uharibifu wa mazao, kuhama kwa jamii za mitaa, hali duni ya maisha, pamoja na kuzidisha umaskini ndani ya madola.

Jumuiya ya kimataifa inadai kwamba iko katika haja kubwa ya kutafuta suluhu ya mgogoro huu. Katika miongo ya hivi karibuni, mikataba mbalimbali ya kimataifa imetiwa saini kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa na masuala ya mazingira, kama vile Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 1992, Itifaki ya Kyoto ya mwaka 1997 na Mkataba wa Paris wa 2015. Hata hivyo, wengi wanahoji kuwa maendeleo madogo sana yamepatikana. Imefanywa katika kushughulikia kwa ufanisi changamoto nyingi za kimazingira ambazo dunia inakabiliana nazo kwa sasa. Hii ni kwa sababu mjadala hadi sasa haujaweza kutambua na kushughulikia chanzo cha mgogoro wa mazingira duniani, kwa sababu mambo ambayo wengi wanayatafuta utatuzi wake kama vile matumizi makubwa ya nishati ya mafuta, ukataji miti mkubwa, kuongezeka kwa uzalishaji wa nyama, sera mbovu za kilimo, uzalishaji na matumizi ya kupindukia ya binadamu, na uchafuzi wa maji wa viwanda mbalimbali, kiasi kikubwa cha plastiki, nguo na bidhaa nyinginezo miongoni mwa taka; Kiuhalisia ni dalili za tatizo na sio chanzo cha tatizo. Maendeleo katika kushughulikia suala hili yatasalia kuwa kutokamilika mradi tu utambuzi na tiba ya tatizo yatabaki kuwa na dosari.

Chanzo kikuu cha mgogoro wa kimazingira ni “mfumo na nidhamu za kirasilimali” wa kimada uliopagawishwa na faida ambayo inatawala siasa, uchumi na maisha ya kijamii ya mataifa hivi leo, ambayo imeunda mtindo usio endelevu wa matumizi na uzalishaji ndani ya nchi katika harakati zao za kulinda mapato na faida za kiuchumi kwa gharama ya mahitaji na maadili mengine yote ya binadamu, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa mazingira. Unyanyasaji wa mazingira na kuibuka kwa shida nyingi za mazingira ni matunda tu ya mfumo huu; Mgogoro tunaoushuhudia si lolote bali ni urithi wa mfumo huu.

Ulimwengu wa leo uko katika njia panda kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na majanga ya kimazingira yanayoukumba. Hapana shaka kwamba sayari hii si salama maadamu mfumo wa kirasilimali unaitawala; Badala yake, si salama kwa njia yoyote, na hakuna tiba ya maradhi ya ulimwengu inaweza kupatikana chini ya usimamizi wa sheria yake. Kwa hiyo, ni hakika kwamba lazima kuwe na mbinu mpya ya kukabiliana na mgogoro huu na kulinda sayari hii na ubinadamu kutokana na madhara na uharibifu. Hivyo basi, katika muda wa wiki mbili zijazo, kitengo cha wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kitashughulikia sababu halisi za mgogoro huu wa kimazingira, na pia kuwasilisha masuluhisho yanayotolewa na mfumo wa Uislamu na nidhamu zake kama njia mbadala ya urasilimali katika kushughulikia matatizo ya mazingira yanayoathiri dunia hii leo. Tutaeleza misingi, kanuni na mbinu za Kiislamu za kulinda na kuhifadhi sayari hii, ikiwa ni pamoja na kusimamia rasilimali kwa njia inayowiana na maumbile huku ikidhamini maendeleo ya kiuchumi na uzalishaji kwa wanadamu.

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿.

"Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu." [Ar-Rum 30:41]

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Jumanne, 26 Rabi' ul-Awwal 1443 H sawia na 02 Novemba 2021 M

- Ili Kufuatilia kwa Lugha Nyenginezo -

 
 
 
 
 

Fuatilieni machapisho kuhusiana na maudhui ya kampeni kwenye kurasa maalum za mitandao ya kijamii za Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari:

facebook

https://www.facebook.com/womenscmoht/

twitter

@WomenForKhilafa

Instegram n

@womenshariah5

- Alama Ishara za Kampeni -

#EnvironmentalCrisis

 fb

tw

 instagram

#أزمة_البيئة  

fb

 tw

 

instagram

- Makala -

Kongamano la Hali ya Hewa Lamalizika kwa Makubaliano Machache

Adnan Khan

11 Rabi' II 1443 H - 16 Novemba 2021 M

Mkutano wa 26 Waangusha Jani la Mtini juu ya Ufisadi wa Mfumo wa Kiulimwengu na Kufichua Uongo wa Wale Wanaousimamia

Zeina As-Samit
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

4 Rabi' II 1443 H - 09 Novemba 2021 M

Majibu kuhusu Mgogoro wa Mazingira yako ndani ya Qur'an na Sunnah

Yasmin Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

4 Rabi' II 1443 H - 09 Novemba 2021 M

COP26: Jinsi Warasilimali Wanavyougeuza Uchafuzi wa Mazingira Kuwa Faida

Zehra Malik

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

2 Rabi' I 1443 H - 07 Novemba 2021M

Kampuni za Kimataifa na 'Msaada' wao Ghushi kwa Mazingira

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

29 Rabi' I 1443 H - 05 Novemba 2021 M

Je, Teknolojia Mpya ya Kijani ndio Suluhisho la Mgogoro wa Mazingira, au Wembe ni Ule Ule?

Sarah Mohammed – Amerika

28 Rabi' ul-Awwal 1443 H - 04 Novemba 2021 M

 Amerika Yaosha Dhambi Zake Juu ya Mgogoro wa Hali ya Hewa kwa Kuzihonga Nchi za Kiislamu za Kusini Mashariki mwa Asia

Dkt. Fika Komara

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

26 Rabi' ul-Awwal 1443 H - 02 Novemba 2021 M

Darasa

Hizb ut Tahrir / Uingereza

Mazingira - Iwapi Sauti ya Uislamu?

Dkt Abdul Wahid, Mwenyekiti wa Kamati Tekelezi ya Hizb ut Tahrir Uingereza, aelezea maslahi tofauti tofauti yaliyofungwa katika ajenda ya mabadiliko ya hali ya hewa - hayatokani na nia za dhati kwa ajili ya wanadamu.

Ukizingatia kuwa nchi nyingi za Waislamu zina viwango vibaya vya uchafuzi wa mazingira, anauliza kwa nini hatuna sauti leo!

Jumatano, 27 Rabi al Awwal 1443 H - 03 Novemba 2021 M

#COP26  #TimeForIslam  #TimeForKhilafah  #HizbBritain

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu