Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kongamano la Hali ya Hewa Lamalizika kwa Makubaliano Machache

(Imetafsiriwa)

Kongamano kubwa la kimataifa la hali ya hewa la COP26 lilidumu kwa wiki mbili huko Glasgow nchini Uingereza. Lilileta pamoja karibu mataifa 200 ili kukubaliana viwango vya utoaji wa hewa chafu ili sayari isifikie kiwango kibaya. Kongamano hilo liliwaleta pamoja viongozi wapatao 200 ambao wameombwa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu hadi ifikapo mwaka 2030. Kumekuwa na hali ya majadiliano kuhusu hali ya dunia kutoka uchafuzi wa mazingira hadi takataka, ukame hadi uchafuzi wa maji duniani, jambo linahitaji kufanywa kwani tunaharibu sayari. Lakini baada ya wiki za majadiliano washiriki walikubaliana kurejea katika muda wa mwaka mmoja na kujadili kila kitu tena, awamu ya chini zaidi badala ya utumiaji wa makaa ya mawe. Kutajwa tu kwa upunguzaji wa kisukuku kumeonekana kama mafanikio.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998 Jopo la Kiserikali kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi (IPCC) limeongoza masuluhisho ya masuala ya hali ya hewa. Makongamano yake mbalimbali yamefanyika na kuhudhuriwa na nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Msimamo wa IPCC na wanasayansi wengi ni kwamba kiwango cha joto Duniani kinaongezeka. Ongezeko la gesi chafu zinazozalishwa na wanadamu kupitia uchomaji wa mafuta ya kisukuku ndio chanzo cha tatizo.

Suluhisho la matatizo haya ya kimazingira linalenga katika kupunguza kwa hatua utoaji wa hewa chafu kwa kuhama kutoka matumizi ya mafuta ya kisukuku hadi vyanzo vya kijani. Kongamano la G20 kabla ya kongamano la COP26 lilishuhudia mataifa kadhaa yakipendekeza jinsi yatakavyo punguza matumizi ya nishati ya kisukuku na kuhamia vyanzo vya nishati mbadala. Kuna changamoto nyingi katika kuafikiwa hili kwa mataifa mengi kutokuwa na mazingatio juu ya ahadi zao za kupunguza uzalishaji. Viwanda vingi vimejengwa kwa msingi wa matumizi ya nishati ya mafuta kuanzia viwanda vya magari, kemikali za petrol, kilimo, plastiki, saruji, chuma, vifaa vya elektroniki na vingine vingi. Muujiza wa kiuchumi wa China umejengwa juu ya matumizi yake makubwa ya nishati ya Makaa ya mawe na hata leo Makaa ya Mawe yanatoa 60% ya umeme wake. Magharibi wanaona kuachwa kwa nishati ya mafuta kama suluhu la matatizo ya kimazingira yanayoikabili dunia. Wanamazingira thabiti wanahoji kupigwa marufuku kwa nishati ya mafuta na wana wasiwasi kuhusu nishati ya nyuklia na wanasema watu wanapaswa kuacha kula nyama.

Wapinzani wa hili, ambao wanapatikana upande wa kulia wa wigo wa kisiasa ni ongezeko la joto duniani ni mahala fulani kati ya mambo ya kubahatisha sana na “uongo mkubwa zaidi”, kunukuu kutoka jina la kitabu juu ya jambo hili kwa kile kilicho andikwa na seneta James Inhofe ambaye ni mwana republican mwenye ushawishi mkubwa juu ya masuala ya hali ya hewa. Wanaamini wanamazingira wanatumia janga la mabadiliko ya hali ya hewa kusukuma ajenda yao wenyewe, ambayo inafadhilisha maumbile kuliko mahitaji ya watu, yenye kulazimisha kubadili kutoka matumizi ya mafuta ya visukuku kwenda kwenye vyanzo vya nishati mbadala, wakisimamia juu ya “uingilia kati mkubwa wa Serikali” wanasema kuwa sayansi haionyeshi kabisa kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanahitaji sera zinazofuatwa kwa sasa. Baadhi ya upande wa kulia pia wanadai kubadilisha mazingira kuwa kama zamani ni jambo lisilowezekana kiuchumi. Pia wanadai kuwa majaribio ya kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa kama vile kuzuia utoaji wa gesi chafu, yanaweza kusababisha madhara zaidi ya  kiuchumi kuliko manufaa yao ya mazingira. Ingawa wengine wanaona suluhisho pekee ni teknolojia mpya ambayo inaweza kuchukua nafasi ya vyanzo vya nishati tunavyotumia leo. Wanahitaji karibu miaka 50 mpaka 100 kuunda teknolojia kama hiyo. Upinzani dhidi ya wanamazingira umejizatiti kuendeleza uchumi wa dunia kama ulivyo na sio kufanya mabadiliko makubwa kama Upande wa Kushoto unavyotaka.

Hata kama hali ya hewa haikubadilishwa bado tuna tatizo kubwa ambalo chanzo chake ni binadamu. Uchafuzi uliosambaa angani, uchafu unaomwagwa kila mwaka katika mito na bahari. Taka za mabaki, janga la unene wa kupindukia, ufyekaji wa misitu, ili kuanzisha miji, haya yote ni majanga yanayo sababishwa na binadamu ambayo tunakabiliana nayo hapa na pale. Uchafuzi wa maji ya kunywa kutokana na kemikali za viwandani, mbolea inayotirirka kutokana na kilimo na majitaka. Vyuma vizito, kemikali hatari, microplastics na isotopes zenye miyonzi ni vichafuzi hatari. Shida hizi zote zipo kwetu bila kuzingatia hali ya mazingira.

Kongamano la COP26 halikuelezea mitindo ya maisha ambayo watu wanaishi. Ukuaji wa kudumu wa uchumi, ulaji, madeni na matumizi na utajiri wa mali ndio mitindo ambayo Ubepari unakuza na ndio mfumo unaotawala sehemu kubwa ya ulimwengu. Suala hili linahitaji mabadiliko ya kimfumo, kwani sababu nyingi zipo katika mfumo wa kiulimwenguni wa Kibepari, lakini hakuna anayependekeza kwa sasa suluhisho linaloshughulikia matumizi makubwa ambayo yanachochea mahitaji ya bidhaa za kimada, inayo chochoea uchafuzi wa mazingira pamoja na ukuaji wa uchumi. Kujikita zaidi katika mkakati wa utoaji wa hewa chafu ni kupuuza uhitaji wa kudhibiti mahitaji ya bidhaa za kimada katika mfumo wa kibepari ambao waziwazi hauna nia ya kubana matumizi na hamu isiyo na kikomo ya ukuzaji uchumi. Makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango huu yameegemea kwa mataifa yenye nguvu katika kulinda maslahi yao - kila moja likijaribu kufikia matokeo katika mazungumzo yanayoipendelea yenyewe.

أزمة_البيئة#    #EnvironmentalCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu