Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mkutano wa 26 Waangusha Jani la Mtini juu ya Ufisadi wa Mfumo wa Kiulimwengu na Kufichua Uongo wa Wale Wanaousimamia
(Imetafsiriwa)

Ni kongamano la 26! Kongamano hilo, ambalo lilifanyika Januari 31, 2021, linamaanisha kuwa kulikuweko na makongamano mengine 25 ya hali ya hewa yaliyotangulia, lakini hayakuleta matokeo ya maana. Kongamano hili lilifanyika na hali za dharura za hewa ziliendelea (kurekodi mafuriko, moto mkubwa, ongezeko la joto duniani, kupungua kwa mazingira asilia, kuenea kwa jangwa, uchafuzi wa mazingira, matetemeko ya ardhi...nk.) kutoa ushuhuda wa kufeli kwa majaribio hayo ya mara kwa mara ya kutatua matatizo haya ya kimazingira ambayo yameenea kwenye sayari hii, na kwamba ulimwengu ulianza kutambua uzito wa hatari ambazo zingeizunguka sayari hii na wale waliomo ndani ya yake katika cha miaka 30 au 40 ijayo.

Kongamano hili, au kama lilivyoitwa, Kongamano la Glasgow, ni fursa kwa viongozi wa dunia kujadili kile ambacho kimetimizwa tangu Kongamano la kihistoria la Paris mnamo 2015 hadi sasa. Kongamano hili lilizingatiwa kuwa muhimu zaidi katika suala la kulazimisha nchi kote ulimwenguni kuchukua hatua za kupunguza ongezeko la joto duniani.

Wajumbe kutoka karibu nchi 200 walikusanyika jijini Glasgow kutafuta njia ya kufikia malengo ya Makubaliano ya Hali ya Hewa ya Paris, ambayo ni kupunguza ongezeko la joto hadi kati ya nyuzi 1.5 na 2, ambapo inahitaji kupunguza uzalishaji unaoongezeka kila mwaka. Nchi 20, ikiwwemo Amerika na Canada, ambazo ni miongoni mwa wafadhili wakuu wa sekta hiyo, zimeahidi kuacha kufadhili miradi ya mafuta ya kisukuku ng'ambo ifikapo mwishoni mwa 2022. Ndiyo, nchi hizi zimeahidi, lakini maelezo ya ahadi hizi hayaeleweki na hakuna ratiba iliyotolewa.

Zaidi ya nchi 40 zimejitolea "kutangaza mabadiliko kutoka kwa makaa ya mawe - aina chafu zaidi ya mafuta ya kisukuku - hadi kwenye nishati safi" katika mpango uliokuzwa na serikali ya Uingereza, na wengi wao wametoa ahadi sawa kama vile Poland na Ufaransa, lakini nchi kubwa zinahusika katika sekta hii, kama vile Australia, China, India, Amerika, Japan na Urusi, hazikuwa miongoni mwa waliotia saini. Je, ni sababu gani ya nchi hizi kupinga kutia saini ili kujifunga na utaratibu huu? Je, sababu kuu ya hilo sio kuhifadhi maslahi yao na kung'ang'ana kupata faida, hata kama ni kwa kuhatarisha wanadamu wote?!

Katika ufunguzi wa kongamano la hali ya hewa, katika wakati ambapo wataalam wa mazingira wanapaza sauti za onyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito wa kuchukua hatua ili "kuokoa wanadamu," akisema: "Ni wakati sasa wa kusema 'Imetosha'." Na akaendelea, "Inatosha kukiuka maumbile anuwai. Inatosha kujiua wenyewe kwa kaboni. Inatosha kuyachukulia maumbile kama jaa la taka. Inatosha kuchoma na kuchimba na kufukua vina virefu. Tunajichimbia makaburi yetu wenyewe.”

Anamlilia nani? Nchi maskini zinazosubiri misaada, usaidizi na mikopo kutoka nchi hii, benki ile, au muungano ule? Nchi kubwa zinazoongoza ulimwengu na kuchangia zaidi majanga haya ya mazingira, kisha kukwepa jukumu na kutojitolea kutia saini na kuahidi tu pekee, na kuibakisha ahadi hiyo kama wino tu kwenye karatasi? Nani atawaokoa wanadamu na hatari hii na kiongozi wake ni mfumo wa kirasilimali usio na uwezo wa kutafuta suluhu, uliozoea kuakhirisha mambo, kukwepa na kueneza majivu ili dosari zake zisifichuliwe na ufisadi ukadhihirishwa? Wanadamu watatarajiaje suluhisho kutoka kwa wale wanaosababisha matatizo ndani yao? Mnawezaje kusubiri maisha mazuri na kunusurika kutokana na utawala uliojaa ufisadi na wenye kueneza vifo na maangamizi?!

Wanaelezea wasiwasi wao, kwani ni "nafasi ya mwisho" kama ilivyoelezwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye alisisitiza kwamba "lazima tuchukue hatua sasa" na alizungumzia mlipuko wa hasira ya wananchi ambayo "haiwezi kuzuiwa" endapo kongamano hilo halitafanikiwa kufikia lengo inalotaka! Kufeli kunakaribia, na kufeli ni anwani pana ya kongamano hili, mithili  ya watangulizi wake. Kumekuwepo na makongamano mingi, na kwa kila kongamano linalofanyika, swali linabaki: Je, matatizo ya mazingira yalitatuliwa au yalizidi kuwa magumu zaidi? Na kwa nini?!

Si ajabu kwa nchi za kirasilimali kwamba ahadi zao ni za hazitabiriki na hazieleweki. Nchi hizi ni sawa na vinyonga wanaobadilika rangi kulingana na sehemu zao, hivyo hujitokeza katika makongamano kama hayo, kutafuta suluhu, kueleza kero zao, kusaidia kuziokoa nchi maskini. Kwa kweli, wao ni wanyonyaji damu wa watu, wezi na wakiukaji wa mali na uwezo, kikundi cha unyonyaji, ambacho wasiwasi wao pekee ni kufikia maslahi na kukusanya faida.

Kwa kila kongamano la hali ya hewa linalofanywa, ahadi huwa nyingi - lakini baada ya kongamano hili kupita na mikataba kubaki wino kwenye karatasi tarehe ya kongamano jengine huwasili - washiriki wanasimama kukosoa na kutaka kutekelezwa kwa ahadi za kongamano lililopita ili kupanda matumaini ya uwongo ya utekelezaji wao katika kongamano lao jipya, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Vasos, ambaye aliongoza kongamano la Paris hivyo Kongamano la Glasgow ni "kongamano la kufanya kazi ambalo kwalo tunatekeleza Makubaliano ya Paris." Maneno, maamuzi na ahadi lazima zibadilishwe kuwa vitendo. António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kinachoendelea kuwa ni tahadhari nyekundu kwa wanadamu, akitoa wito kwa viongozi wa dunia kutoa majibu wakati Kongamano lijalo la Dunia la Mabadiliko ya Hali ya Hewa litakapofanyika.

Ijapokuwa matatizo ya kimazingira yanamhusu binadamu kama mtu ili aishi katika mazingira yanayofaa, pingamizi ya Amerika ya kujitolea kufanyia kazi kukabiliana na matatizo hayo, haswa ongezeko la joto duniani, linafichua sera yake mbovu. Je, viwanda hivi ni viwanda vyao wenyewe au vilikuwa katika maeneo mengine kwa njia ya utandawazi, jambo ambalo litapelekea kufungwa au kubadilisha baadhi ya viwanda, jambo ambalo litakuwa na athari mbaya na kupunguza faida ya mali ya watengenezaji, jambo ambalo linapingana na thamani ya kimada yaani juu ya ngazi ya maadili yote kwao... Amerika inakataa kutii yale yaliyoamuliwa katika kongamano hilo, hata kama watu watakosa hewa na kuangamia, au uchafuzi wa mazingira kuongezeka na kuenea, yote hayo hayana thamani maadamu thamani ya kimada hupatikana. Imeshughulikia hali kama hizi hapo awali, kwani hiyo - ambayo ni dola kuu - ilivipa (vita dhidi ya ugaidi) maelezo maalum na fahamu maalum na ya kipekee, na hii hapa inatoa maelezo yayo hayo kwa uchafuzi wa mazingira. Maadamu uchafuzi huu wa mazingira unahuisha kiwanda chake na kuhudumia maslahi yake, unakubalika na ni wa kupongezwa, lakini ukiwa ni kinyume na kile anachokiona na anachokitaka, ni wa kulaumiwa, kukataliwa, na unadhuru mazingira, unadhuru wanadamu.

Ni kongamano litakalofichua tena ahadi na viapo vya uongo vya viongozi wa dunia za kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake; kutokana na kupanda kwa viwango vya bahari, hali mbaya ya hewa, na kadhalika. Ni kongamano ambalo halitakuwa bora zaidi kuliko makongamano yaliyolitangulia, na kuibuka kwa maelfu ya wanaharakati na mwaliko wa waandaaji wa vuguvugu la kimataifa "Fridays for Future" - katika jiji hilo la Scotland ambako kongamano hili linafanyika - ili tu kushinikiza viongozi na kupinga ucheleweshaji wao katika kuchukua hatua zinazofaa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, wanaahidi kwamba watakutana. Hawaamini na kutoa ahadi na hawatimizi, na kusisitiza kwamba kongamano hili, kama watangulizi wake, halitazaa matunda.

Tatizo la mazingira, kama matatizo mengine yanayowazonga wanadamu; linazidi kuwa baya na kuongezeka, na mfumo wa kimataifa umeshindwa kulitatua, kwa hivyo unaahidi na hautimizi na kuwasilisha maagano na hauyatekelezi, na masharti ya makubaliano na wajibu yanabaki kuwa wino kwenye karatasi yasiyokuwa na uhalisia, na wanadamu wanaendelea kuteseka kutokana na ulafi wa mfumo fisadi wa kirasilimali uliofilisika ambao unaweza tu kuchukua hatua zinazoleta manufaa, hata kama hilo litasababisha kutokomeza zaidi wanadamu. Utawala mbovu, unaosababisha ufisadi, mauaji unaoeneza uvundo wa kifo kila mahali, unaeneza ufisadi bara na baharini na kuleta uharibifu kwa wanadamu, miti na hata mawe.

 [ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوالَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ]

Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu. [TMQ Ar-Rum: 41]

#أزمة_البيئة        #EnvironmentalCrisis                 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeina As-Samit

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu