Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Juu ya Ufaradhi wa Khilafah

(Imetafsiriwa)

Utangulizi: Ufaradhi wa Khilafah Umesimama Juu ya Dalili za Kisharia

Baada ya kukombolewa Kabul, mjadala umeanza kuhusiana na hitajio la Khilafah katika eneo hilo ikiwa hatua inayofuata ni kuunganisha mataifa yaliopo kuwa ni dola moja. Kwa kweli ni mjadala makini katika Dini ya Uislamu na kwa hakika ni wajibu, ambao kuupuza ni dhambi.

Muadhamu Maulana Mohammad Ali Jauhar, aliyekuwa mmoja wa viongozi muhimu katika historia ya harakati za kupigania Khilafah katika bara dogo la India (Tehreek e Khilafat) aliwahi kuandika kuhusiana na kuanguka kwa Khilafah ya Uthmaniya: “…hasara za muda kwa Uturuki ambapo tulishauriwa na Ulaya “kukata” kumegusa mtambuko muhimu katika yaliofichika akilini, Mtambuko wa Dini, kwani Mtawala wa Uturuki alikuwa ni Khalifah au Mrithi wa Mtume na Amir ul-Muminin au Kiongozi wa Waumini na Khilafah ni suala msingi la dini kama Quran na Sunnah za Mtume (saw).”

Ni lazima iwekwe wazi kabisa kuwa Khilafah sio suala lililo nje ya Dini yetu. Kama Maulana alivyoelezea kwa usahihi, ni suala ambalo linahifadhi masuala mengi ya kidini kama yalivyo mengine ya wajibu yaliowajibishwa katika Quran Tukufu na Sunnah. Hii ni kwa sababu ni Faradhi kuhukumu kwa yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameyateremsha. Hivyo bila kusimamishwa kwa Khilafah, Dini haiwezi kutekelezwa kwa ukamilifu.

Haya yamefahamika na Masahaba wakubwa (ra) wa Mtume (saw) waliokimbilia kumtawaza Khalifah wa waumini baada ya kufariki Mtume (saw) na umoja wa Khilafah ulifahamika na wale walio na elimu na mamlaka kwa miaka 1300 iliyofuatia.

Hata hivyo, wakati Nchi Washirika na mawakala wao walipofanikiwa kuivunja Khilafah Uthmaniya mnamo 1924, kwa kushirikiana na wasaliti miongoni mwa Waarabu na Waturuki, wamezindua mkakati wa kuitenga dini na maisha katika Ulimwengu wa Kiislamu na kuufanya Ummah kusahau juu ya jukumu lao la kusimamisha Khilafah.

Ndipo hivi leo kuna wale wanaosema kuwa Khilafah sio Faradhi. Bali, kwa upotovu husema kuwa suala la Khilafah ni la hiyari na kuwa Ummah wanaweza kuamua kuisimamisha ama la. Wale wanaosema kauli kama hizo wanafanya hivyo kutokana na kukosa ufahamu au uelewa wa dalili za Ufaradhi wa Khilafah. Kwa hivyo, kutatua suala hili, na ili kupambanua vizuri kuwa Khilafah bila shaka ni Faradhi, dalili za kisharia lazima zichunguzwe, nazo ni Quran Tukufu, Sunnah, na Makubaliano ya Kauli moja ya Masahaba (ra) (Ijma as-Sahaba).

Miongoni mwa Dalili kutoka Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu (swt)

 Katika Surah al-Mai’dah, aya 44, Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ]

“Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Makafiri.” Ibn Kathir ameielezea aya hii katika tafsiri yake:

وقال علي بن أبي طلحة عن ابن عباس قوله: [وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ] قال: من جحد ما أنزل الله فقد كفر. ومن أقر به ولم يحكم فهو ظالم فاسق. رواه ابن جرير

“Amesema Ali bin Abi Talhah kuwa Ibn ‘Abbas (ra) ameifasiri kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ]

“Na wasiohukumu kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio Makafiri.” Yeyote anayekanusha juu ya aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) atakuwa amekufuru, na yeyote anayekiri juu ya aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) lakini asihukumu kwayo, ni dhalimu na fasiq na mtenda dhambi. Na ndivyo alivyosimulia Ibn Jarir.”

Dhana ya kuwa Dini imefungika kwenye nyanja maalum tu za kimaisha ni batili. Dini haianzii na kumalizia kwenye milango ya nyumba za ibada bali inajumuisha masuala yote, ya kibinafsi na ya Ummah. Ni uongozi uliokamilika na uliosahihi juu ya masuala yote ya kimaisha. Hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) sio tu ametuamrisha juu ya utekelezaji wa ibadah za kiroho, lakini pia ametuwajibishia muamalat, kupigana jihad na kutekeleza hudud na mengineyo. Kwa haya tunazo dalili. Kwa adhabu ya yule anayeiba, katika Surah al-Maidah, aya 38, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

 [وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

“Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyoyachuma, ndio adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu na Mwenye hikima..” Katazo la riba katika miamala yote ndani ya jamii, dalili ni aya 275 ya Sura al-Baqara:

[وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا]

“Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharamisha riba.” Na kuna maarisho mengi ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametuteremshia ili tuyatekeleze katika jamii. Yule anayekanusha maamrisho haya huwa amekiuka maagizo ya Mola wao na huo ni ukafiri.

Pia Mwenyezi Mungu (swt) katika Sura al-Ma’idah aya 48 amewaamrisha waumini kupangilia mambo yao kwa mujibu wa uteremsho:

[فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ]

Basi hukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Surah Al-Mai’dah, aya 48] “…matamanio yao” ni matamanio ya makafiri. Hawahukumu kwa Uislamu na hivyo kukubali sheria zao dhidi ya sheria za Mwenyezi Mungu (swt) ni kutenda dhambi kubwa.

Haya ndio mahitaji ya Khilafah, kwani ni dola ambayo huhakikisha utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu (swt), inawaunganisha Waislamu chini ya Khalifah na hivyo kukamilisha jukumu letu kwa Mola wetu. Dola hiyo itaongozwa na mtawala aliyechaguliwa ambaye tunalazimika kumtii. Haya yanapata ushahidi kutoka Sura An-Nisa, aya 59:

  [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ]

“Enyi Mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume.” Ni kwa kuchaguliwa mtawala tu ndipo mizozo huweza kutatuliwa na masuala ya dola kudhibitiwa. Imam Mawardi ameandika al-Ahkam as-Sultaniyyah (Hukmu za Utawala):

الإمامةُ موضوعةٌ لخِلافة النبوَّة في حراسة الدِّين وسياسة الدنيا، وعَقْدُها لِمَن يقوم بها في الأمَّة واجبٌ بالإجماع

“Uiongozi (Imamah) ni suala la Khilafah ya Utume, katika kusimamia Dini na siasa za Dunia. Mkataba wake juu ya yule awezaye kuyatekeleza kwa Ummah ni wajibu kwa Ijmaa’a.” 

Ni wajibu wa Ulamaa kuwashikilia watawala wahukumu kwa yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameyateremsha, kuelekeza mizozano yote kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume (saw). Kama Imam Ghazali alivyoelezea katika kitabu chake, Ihyaa’ Uluum ud Diin (Kuhuisha Elimu ya Dini) kuwa

 فساد الرعايا بفساد الملوك، وفساد الملوك بفساد العلماء، وفساد العلماء باستيلاء حب المال والجاه، ومن استولى عليه حب الدنيا، لم يقدر على الحسبة على الأراذل، فكيف على الملوك والأكابر

“Ufisadi wa raia ni kwa ufisadi wa watawala; ufisadi wa watawala ni kwa ufisadi wa Ulamaa, na ufisadi wa Ulamaa ni kwa upapiaji wa kupenda mali na ufahari. Na anayeelemewa na mapenzi ya dunia hatoweza kuwahisabu walio wachini, basi vipi kuhusu watawala na viongozi?” Imam Ghazali amesema,

فهذه كانت سيرة العلماء وعادتهم في الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر، وقلة مبالاتهم بسطوة السلاطين؛ لكونهم اتكلوا على فضل الله تعالى أن يحرسهم، ورضوا بحكم الله تعالى أن يرزقهم الشهادة، فلما أخلصوا لله النية؛ أثَّر كلامهم في القلوب القاسية فليَّنها وأزال قساوتها

“Basi huu ulikuwa ndio mwendo wa Maulamaa na taratibu zao za kuamrisha mema na kukataza maovu, na kutojali nguvu za watawala; kwa sababu ya kutegemea kwao fadhila za Mwenyezi Mungu (swt) za kuwahifadhi, na kuridhia hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) kuwaruzuku shahada na kuwa na ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kauli zao zinaathiri nyoyo ngumu, hivyo Mwenyezi Mungu (swt) huzilainisha na kuondoa ugumu wake.”

Miongoni mwa Dalili kutoka katika Sunnah za Mtume (saw)

Kila dola inahitaji mtawala na mtawala wa Khilafah ni Khalifah. Hili ndio jina ambalo Mtume (saw) amelichagua kwa wale wanaokuja nyuma yake katika uongozi, japokuwa Makhalifah hujulikana pia kwa majina mengine kama Imam au Sultan au Amir. Itakuwa ni kiongozi, Imam, Khalifah huyu ndiye ataehakikisha utekelezaji mzuri wa Dini. Katika Hadith kadhaa, Mtume (saw) amemzungumza Khalifah ambaye ataongoza waumini baada yake. Kutokana nao, Mtume (saw) amesema,

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ وَإِنَّهُ لاَ نَبِيَّ بَعْدِي وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ فَتَكْثُرُ‏.‏ قَالُوا فَمَا تَأْمُرُنَا قَالَ فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ وَأَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»‏

“Wana wa Israil walikuwa wakitawaliwa na kuongozwa na Mitume: kila anapofariki Mtume hufuatiwa na Mtume mwengine. Hakutakuwa na Mtume baada yangu, bali kutakuwa na Makhalifah na watakuwa wengi. Watu wakasema, "Basi nini unatuamrisha Ewe Mtume (saw)? Akasema, “Toeni bay’ah kwa wa kwanza na kisha kwa wanaofuatia, na wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya uongozi wao.” [Muslim].

Kwa hivyo yule anaepewa dhamana juu ya mambo ya Waislamu lazima apewe bay’ah na lazima atiiwe. Haimaanishi kuwa kila mtu lazima atoe bay’ah kwa Khalifah bali, ni faradhi ya kujitosheleza (fardhi kifaya) kwa waumini kuhakikisha kuwa mkataba wa bay’ah unapatikana. Wakati utiifu kwa Khalifah unawajibishwa kwa kila Muislamu, mkataba wa Khalifah ni kwa kundi kutoka miongoni mwao, kama ni faradhi ya kujitosheleza. Imam An-Nawawi ameeleza katika Sharh ya Sahih Muslim kuwa,

وَأَجْمَعُوا عَلَى انْعِقَادِ الْخِلَافَةِ بِالِاسْتِخْلَافِ وَعَلَى انْعِقَادِهَا بِعَقْدِ أَهْلِ الْحَلِّ وَالْعَقْدِ لِإِنْسَانٍ إِذَا لَمْ يَسْتَخْلِفِ الْخَلِيفَةُ وَأَجْمَعُوا عَلَى جَوَازِ جَعْلِ الْخَلِيفَةِ الْأَمْرَ شُورَى بَيْنَ جَمَاعَةٍ كَمَا فَعَلَ عُمَرُ بِالسِّتَّةِ وَأَجْمَعُوا عَلَى أَنَّهُ يَجِبُ عَلَى الْمُسْلِمِينَ نَصْبُ خَلِيفَةٍ وَوُجُوبُهُ بِالشَّرْعِ لَا بِالْعَقْلِ

“Na wamekubaliana (Wanazuoni) juu ya kumchagua Khalifah kwa mfuatano na juu ya kumchagua kwa mkataba wa Ahl ul Hal wal Aqd kwa mtu pindi Khalifah hakuchaguliwa kwa mfuatano. Na wamekubaliana juu ya kujuzu kuteuliwa Khalifah kuwa ni suala la Shura baina ya jamaa kama alivyofanya Umar (ra) kwa watu sita, na wakakubaliana juu ya uwajibu kwa Waislamu kumchagua Khalifah na utiifu ni kwa shariah na sio kwa akili ya mwanaadamu.” Hivyo imeonekana mwanzoni kuwa mkataba wa Bay’ah umetekelezwa na watu wenye ushawishi, Ahl al-Hal wal-Aqd (watu wenye sauti na ushawishi).

Makubaliano ya Masahaba (Ijmaa as-Sahaba)

Masahaba wa Mtume (saw) walielewa ufaradhi wa kumteuwa mtawala kuuongoza Ummah na kutekeleza Dini, kiasi cha kuchelewesha maziko ya Mtume (saw). Kama tuelewavyo, mazishi ya maiti ni faradhi na hivyo kwa baadhi ya Masahaba (ra) kuchelewesha maziko ya Mtume (saw), kwa kutanguliza suala la kumchagua mtawala inamaanisha kuwa wameelewa kuwa huo ni wajibu mkubwa zaidi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Ibn Khaldun amesema katika Al-Muqaddimah (Utangulizi),

إن نصب الإمام واجب قد عرف وجوبه في الشرع بإجماع الصحابة والتابعين؛ لأن أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم عند وفاته بادروا إلى بيعة أبي بكر رضي الله عنه وتسليم النظر إليه في أمورهم، وكذا في كل عصر من بعد ذلك ولم يترك الناس فوضى في عصر من الأعصار، واستقر ذلك إجماعا دالا على وجوب نصب الإمام

“Kumsimamisha Imam ni Wajib na uwajibu wake umeeleweka katika sharia kwa Ijmaa ya Masahaba na Tabi’in. Kwani Masahaba wa Mtume (saw) wakati wa kifo chake Mtume (saw) walikimbilia kutoa Bay’ah kwa Abu Bakar (ra) na kumpatia majukumu ya Khilafah ili asimamie mambo yao. Na vivyo hivyo katika kila zama baada ya hapo, kwani watu hawakupuuzia suala hilo, na hivyo kuepuka machafuko kwenye zama za baadaye. Hivyo, inaonyesha Ijmaa ya uwazi juu ya uwajibu wa kumchagua Khalifah.”

Hitimisho: Na Tufanyeni Kazi Pamoja na Hizb ut Tahrir Kwa Ajili ya Kusimamisha Khilafah

Na hivyo, imekuwa ni hakika kwetu kuwa kumchagua Khalifah na kuisimamisha Khilafah ni Faradhi. Amri ya kuhukumu kwa yale yalioteremshwa (kutoka kwa Mwenyezi Mungu) na kumchagua Khalifah ni wajibu juu ya Waislamu wote. Kwa hivyo, ni faradhi kifayah. Hadi jukumu hili liwe limetekelezwa, ni wajibu juu ya Waislamu wote kufanya kazi ili kulikamilisha.

Ama kwa upande wa namna ya kulifanyia kazi, ni kupitia kuanzisha kundi, miongoni mwa Ummah ambalo litaamrisha mema na kukataza maovu, kuhakikisha usimamishaji wa hukmu za Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika Quran Tukufu katika Surah al-Imran, aya 104:

[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

Na uwe kutokana na nyinyi  Ummah unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio waliofanikiwa.” Kutoka katika Tafsir ya Ibn Kathir:

والمقصود من هذه الآية أن تكون فرقة من الأمة متصدية لهذا الشأن

“Makusudio ya aya hii ni kuwepo kundi (Firqa) katika Ummah la kutekeleze jukumu hili, japokuwa ni jukumu la kila mtu katika Ummah huu, kila mmoja kwa mujibu wa uwezo wake.” Basi na tujielekeze katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah na kukamilisha utekelezaji wa Dini yetu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Khalil Musab – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu