Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
H. 23 Safar 1447 | Na: BN/S 1447 / 02 |
M. Jumapili, 17 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ni Wakati sasa wa Kugeuza Ukurasa wa Giza wa Oslo
(Imetafsiriwa)
Smotrich alitangaza kuangamia kwa mradi wa Dola ya Palestina kwa kuzinduliwa kwa mradi wa E1 au East One, ambao unachukuliwa kuwa utekelezaji wa kinachojulikana kama Mpango wa Jerusalem Kuu. Mpango huu unatenganisha Ukingo wa Magharibi wa Kaskazini kutoka Ukingo wa Magharibi wa Kusini, na, sambamba na hatua zilizochukuliwa na umbile la Kiyahudi uwanjani, unaunda viunga vilivyotengwa ndani yake ambavyo vinawazingira watu wa Ukingo wa Magharibi. Hili lilitanguliwa na kubomolewa kwa kambi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi na kuorodheshwa kwa UNRWA kama shirika lisilo halali, ili suala la wakimbizi libaki kuwa lisilo na umuhimu wowote.
Hatua hizi zote zinazofuatana na zinazoongezeka zinaacha jambo moja tu la kusema: Hakuna chochote kilichosalia katika Makubaliano ya Oslo uwanjani ambacho kitaacha sura yoyote ya Dola ya Palestina kwa watetezi wa dola moja, hata ikiwa haina mamlaka na hata ikiwa haina silaha!
Hakuna maswala ya suluhisho la mwisho (Jerusalem, mipaka, na wakimbizi) ambayo yanaweza kujadiliwa!
Hakuna kilichosalia katika Makubaliano ya Oslo isipokuwa usaliti wa makubaliano ya PLO kwa sehemu kubwa ya Palestina na utambuzi (batili na wa makosa) wa haki ya Mayahudi kwa sehemu kubwa ya ardhi ya Palestina!
Mabaki pekee ya Oslo yaliyosalia ni uratibu wa usalama unaowaweka salama Mayahudi na walowezi, na kufungua milango kwa serikali shirikishi kabla na baada ya PLO kuamiliana na umbile hilo nyakuzi kama umbile halali!
Hakuna kilichosalia katika makubaliano hayo ya khiyana isipokuwa utekelezaji wa ajenda za Mayahudi, Wamarekani, na Wazungu katika kuwapiga vita Mujahidina na kubadilisha mitaala ya kuondoa maadili ya Uislamu katika nafsi za Waislamu, na badala yake kuweka fahamu za ukafiri, amani na kuishi pamoja!
Makubaliano ya Oslo hayakuacha chochote zaidi ya wale wenye nguvu katika Mamlaka ya Palestina wanaonyakua pesa za watu wa Palestina, kuwanyonga kwa kodi, na kuwafunga kwenye mfumo wa benki unaohesabu pumzi zao!
Licha ya ukweli huu wote, na licha ya tangazo la mara kwa mara la umbile nyakuzi kwamba halitaruhusu kuanzishwa kwa Dola ya Palestina, na kwamba hakuna nafasi mjini Gaza kwa Mamlaka ya Palestina. Wapambe wake wanakwamia huduma yoyote wanayoweza kuitoa kwa badali ya kuendelea kuwepo Gaza, Ukingo wa Magharibi, au mabaki yoyote ya Palestina ambayo wao na watu wao wameyafuja.
Makubaliano ya Oslo, ambayo yalizikwa na umbile la Kiyahudi, isipokuwa mabaki ya yale yaliyowahudumia, na Dola ya Palestina, ambayo waliiavya kabla hata haijachukua sura katika tumbo la usaliti, yamefikia mwisho kwa Umma wa Kiislamu kugeuza ukurasa wa sura hii ya giza kwa ukurasa wake wa mwisho, wa giza zaidi: Gaza na majeraha yake ya historia, na kufungua ukurasa wa historia na jiografia. Katika jiografia, Palestina ni lulu ya ash-Sham, iliyopambwa na Muhammad (saw) usiku ambao alipelekwa huko. Ilikuwa ni Kibla chake cha kwanza (mwelekeo wa swala) na Kibla cha kwanza cha Waislamu, kisha wa tatu ya Misikiti miwili Mitukufu. Kutoka bahari yake hadi mto wake, ni mali ya Umma wa Muhammad (saw). Kihistoria, ni ardhi ya ufunguzi wa Maswahaba na Khilafah Rashida, ukombozi wa watu wema, na masimulizi ya Mujahidina. Juu yake, Makruseda walishindwa, na ndani yake, Mwenyezi Mungu aliwashinda Watatari. Ni ardhi ambayo lazima iregee jinsi ilivyokuwa—si jambo lililopangwa, bali ni Ummah mmoja, ambao wanajeshi huingia ndani yake kutoka katika maeneo yake, wakifuta athari za walioikalia kimabavu, na kuwachukulia hatua wale walioisaliti. Kisha hapo itakuwa kiini cha Uislamu.
[وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِنْ بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ * إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِقَوْمٍ عَابِدِينَ]
“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema. Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbya 21:105-106]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: 0598819100 www.pal-tahrir.info |
E-Mail: info@pal-tahrir.info |