Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  25 Jumada I 1446 Na: HTS 1446 / 28
M.  Jumatano, 27 Novemba 2024

Ripoti ya Habari
Hotuba ya Kisiasa katika Klabu ya Al-Hilal, Kusini mwa Soko la Port Sudan
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa mnamo siku ya Jumatatu, 23 Jumada al-Awwal 1446 H, sawia na tarehe 25 Novemba 2024, katika Klabu ya Al-Hilal, kusini mwa soko kuu la Port Sudan. Anwani ya hotuba hiyo ni:

“Mali ni ya Mwenyezi Mungu, na Watu ni Wadhamini Wake.”

Mzungumzaji, Ustadh Yaqub Ibrahim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumzia kanuni za msingi za mfumo wa uchumi wa Kiislamu na uwezo wake wa kutatua migogoro inayoikabili Sudan. Aliangazia rasilimali na uwezo mkubwa wa Sudan, akiunganisha hili na umaskini unaovumiliwa na watu wake. Ibrahim alihusisha tatizo hili na utekelezaji wa mfumo wa uchumi wa kibepari wa Magharibi, unaotawaliwa na mataifa ya kibepari na zana zao za kikoloni, kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia.

Alieleza msimamo wa wazi wa Uislamu juu ya mali, umilikaji wake, matumizi yake na maendeleo, na akasisitiza kwamba tatizo la kiuchumi katika Uislamu linatokana na ugavi wa mali badala ya uhaba wake, kama wanavyodai mabepari. Mzungumzaji pia alifafanua juu ya aina tofauti za umiliki katika Uislamu, hasa umiliki wa umma, ambao unapatikana kwa wingi nchini Sudan. Alihoji kuwa Sudan inahitaji tu dola imara kutekeleza mfumo wa Kiislamu ili watu wake wanufaike na utajiri wa nchi hiyo. Alithibitisha kwamba hilo litapatikana, Inshallah, kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo iko karibu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Wahudhuriaji walishiriki kwa uchangamfu hotuba hiyo. Mzee mmoja alitamka kwa shauku huku akiwa ameshikilia Liwaa’ iliyoandikwa Shahada (La ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah”: “Tunataka Raya hii inyanyuliwe na dola isimamishwe kwa misingi ya Uislamu.” Mhudhuriaji mwengine aliuliza: “Kwa nini serikali haitekelezi mfumo wa Kiislamu leo ​​ili kufikia haki na usalama?”

Ust. Yaqub alijibu maswali, maoni, na maulizo kwa njia ya hali ya juu, ambayo ilipokelewa vyema na waliohudhuria.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu