Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 8 Jumada II 1446 | Na: HTS 1446 / 33 |
M. Jumanne, 10 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba ya Kisiasa mjini Port Sudan
Haki ya Kisheria ya Waislamu katika Dhahabu, Petroli, na Rasilimali Nyenginezo
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa mbele ya Klabu ya Al-Shabiba katika Soko Kuu la Port Sudan, mnamo siku ya Jumatatu tarehe 7 Jumada al-Akhirah 1446 H, sawia na 9/12/2024 M, yenye kichwa: “Haki ya Kisheia ya Waislamu katika dhahabu, petroli na rasilimali nyenginezo”, ambapo Ustadh Ahmed Abkar, wakili, mjumbe wa baraza la Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan alizungumza, ambapo ilifafanua mali ya umma kuwa ni vitu vilivyoainishwa na sheria kwa ajili ya jamii, vinavyoshirikiwa kati yao, na kukatazwa kumilikiwa na mtu binafsi peke yake. Hii inapatikana katika aina tatu: yale ambayo ni katika huduma za jamii, na kwamba ikiwa nchi au jamii haitazipata, hutawanyika kuzitafuta; mithili ya maji, malisho, moto, na kila kitu kinachohusiana nazo, kama vile mito, bahari, na mashini zinazozalisha umeme kutoka kwa mabonde na nguzo zake...nk, na madini yasiyomalizika; kama vile migodi ya dhahabu, visima vya mafuta, na yanayofanana nayo, na vitu ambavyo kwa maumbile yake hayakubali umiliki wa mtu binafsi juu yake; kama vile umiliki wa barabara ya umma, na chochote kinachohusiana nayo. Akitoa dalili kwa mujibu wa Hadith ya Mtume (saw): «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ؛ فِي الْكَلَأِ وَالْمَاءِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: katika malisho, maji na moto.” Imepokewa na Abu Daawuud.
Ustadh Ahmed alieleza kuwa Sudan ni nchi yenye utajiri mkubwa: dhahabu, petroli na madini mengine na utajiri mwengineo unaoonekana na uliofichika, lakini watu wake wanaishi chini ya mstari wa umaskini, kama matokeo ya dhulma ya Watawala, utekelezaji wao wa mfumo wa kibepari wa kikoloni, na kujisalimisha kwao kwa dola na taasisi za kibepari, ambazo zinaweka maagizo ambayo yanaleta umaskini na kuharibu uchumi, kama vile maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia.
Pia alieleza kuwa dhahabu, petroli, na mfano wake zinazozalishwa zinatosha kutatua matatizo ya kiuchumi ya Sudan. Lakini hili linahitaji kuanzishwa kwa mamlaka ya Uislamu, kwa kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo inatabikisha mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unaofanikisha uadilifu na kutoa haki kwa watu wake, hivyo kuhakikisha usalama na usalama amani na utulivu.
Waliohudhuria walithamini masuluhisho na tiba zilizowasilishwa, na msimamizi muhadhara Ustadh Yaqub Ibrahim aliwashukuru wahudhuriaji kwa kushiriki na usikizi mzuri.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/4411.html#sigProId0a22334379
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |