Al-Waqiyah TV: Je, hili linakutosheleza Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ?
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik (ra) kuwa amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): “Hajaamini yule ambaye analala tumbo lake likiwa limeshiba na hali ya kuwa jirani yake ana njaa na yeye anajua.” Basi vipi kuhusu mji wa Gaza ambao watu wake wanakufa njaa, huku pambizoni mwake kuna ardhi zilizo jaa neema na kheri nyingi, chini ya utawala wa watawala walioisaliti, na kula njama dhidi yake pamoja na maadui zake, wakafunga mipaka na kuziba midomo ya wale walioomba msaada na nusra. Hawakuridhika na kuisaliti tu, walizuia nusra yake na wakajitahidi kuizingira, wakiinyima chakula na dawa.