Jumanne, 18 Safar 1447 | 2025/08/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Marufuku ya Vitabu ya Serikali ya Kibaniani: Jaribio la Kufuta Mapambano na Mihanga ya Kiislamu katika Kashmir Inayokaliwa Kimabavu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika onyesho la wazi la ukosefu wa usalama na unafiki, serikali inayoitwa ya “kidemokrasia” ya India, chini ya utawala wake wa kibaniani wa BJP, imetoa amri ya kupiga marufuku vitabu 25 vinavyoandika uhalisia wa kihistoria wa ukaliaji wake wa kimabavu wa Kashmir. Hatua hii, ya tarehe 5 Agosti 2025, inatoka kwa Idara ya Mambo ya Ndani ya idara wa Jammu na Kashmir, ikitangaza kwamba kazi hizi “feki” chini ya Kifungu cha 98 cha Bhartiya Nyaya Sanhita 2023, ikizituhumu kwa kueneza “simulizi za uwongo”, kupigia debe kujitenga, na kutukuza “ugaidi”.

Maoni:

India inadai kuwa na nchi ya demokrasia lakini inasalia kutokuwa na amani kuhusu baadhi ya vitabu ambavyo ni matukio ya kihistoria ya ukaliaji wake kimabavu wa Kashmir. Inataka kufuta historia yake ya uvamizi huko Kashmir na ukiukaji wa haki za binadamu kuenea katika vizazi.

Marufuku hii inafichua udhaifu wa dola ya India, ambayo, huku ikiendeleza simulizi ya uongo ya hali ya kawaida kupitia matukio kama vile Tamasha la Vitabu la Chinar huko Srinagar – lililozinduliwa siku chache kabla ya kuonyesha taswira ya amani chini ya viatu vya wanajeshi zaidi ya 800,000 – wakati huo huo hutoa maagizo ya kukandamiza mazungumzo ya kifikra kuhusu masaibu ya Kashmir.

Kwa hivyo, kwa upande mmoja, inakuza maonyesho ya vitabu ili kuwasilisha simulizi ya uongo ya hali ya kawaida chini ya viatu vya majeshi 800,000; kwa upande mwingine, katika wiki hiyo hiyo, inatoa amri inayoonyesha orodha ya vitabu vya Kashmir kupigwa marufuku. Hiki ndicho kiwango cha chini cha ukosefu wa usalama wa utawala huo wa Kibaniani, ambao unakimbilia baada ya kushindwa kila upande na bila ya kujali hoja za kiakili za kuhalalisha ukiukaji wake wa haki za binadamu, ukaliaji kimabavu, na kumbukumbu jumla ya Waislamu kuinuka na kuzungumza dhidi ya uvamizi huu. Inafikiri kwamba kwa kuwakandamiza tu, wanaweza kuwanyenyekesha Waislamu na kumbukumbu zao jumla.

Vitabu vilivyopigwa marufuku, vilivyoorodheshwa katika Kiambatisho-A cha tangazo la serikali, vinajumuisha vitabu vya kielimu ambavyo vinaelezea ukandamizaji, upinzani, na matarajio ya Waislamu huko Kashmir. Miongoni mwao ni majina kama vile Colonizing Kashmir: State-Building under Indian Occupation cha Hafsa Kanjwal (Uchapishaji wa Chuo Kikuu cha Stanford), ambavyo vinafichua taratibu za ukoloni wa India katika eneo hilo, na Kashmir's Fight for Freedom na Moh'd Yousuf Saraf (Watoto wa Feroze Pakistan), kinachoelezea mapambano ya Waislamu dhidi ya uvamizi.

Kazi nyingine mashuhuri ni pamoja na Azadi ya Arundhati Roy (Penguin India Darya Gunj, New Delhi), The Kashmir Dispute 1947-2012 ya A.G. Noorani (Tulika Books Chennai Tamil Nadu), Kashmir in Conflict: India, Pakistan and the Unending War ya Victoria Schofield (Bloomsbury India Academic), na Resisting Occupation in Kashmir  ya Haley Duschinski, Mona Bhan, Ather Zia, na Cynthia Mahmood (Uchapishaji wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania).

Vitabu hivi vinaandika ukiukaji wa kimpangilio wa haki za binadamu, kupotezwa kwa lazima, ukatili wa kijeshi, na mmomonyoko wa kitambulisho cha Kiislamu cha Kashmir chini ya utawala wa India.

Upigaji marufuku huu si ujanja wa kisiasa tu bali ni shambulizi la moja kwa moja kwenye kumbukumbu jumla ya Ummah na wajibu wa kupinga ukafiri na ukandamizaji. Kashmir, ardhi yenye Waislamu wengi, imekuwa chini ya ukaliaji haramu wa kimabavu tangu 1947, na serikali ya Kibaniani, uliokita mizizi katika mfumo wa kikafiri wa kisekula wa demokrasia, unaotafuta kuugawanya Ummah kwa kufuta simulizi za jihad, muhanga, na wito wa ukombozi. Vitabu kama Do You Remember Kunan Poshpora? cha Essar Batool na wengineo (Vitabu vya Zubaan) vinaangazia ukatili waliofanyiwa wanawake wa Kiislamu, na kutukumbusha hadith ya Mtume Muhammad (saw) isemayo: «الْمُسْلِمُونَ كَرَجُلٍ وَاحِدٍ إِنْ اشْتَكَى عَيْنُهُ اشْتَكَى كُلُّهُ وَإِنْ اشْتَكَى رَأْسُهُ اشْتَكَى كُلُّهُ» “Waislamu ni kama mwili mmoja, jicho likishtakia maumivu, mwili mzima huuma, na kichwa kikiuma, mwili mzima huuma” (Sahih Muslim).

Vitendo vya serikali ya Kibaniani vinatokana na kushindwa kwake kutiisha ari ya uthabiti ya Waislamu wa Kashmir. Licha ya kufutwa kwa Kifungu cha 370 mnamo 2019, ambacho kiliondoa uhuru wa eneo hilo na kulijaza hatua na sera za kubadilisha sura yake ya kidemografia ya Kiislamu, upinzani unaendelea.

Marufuku hii ni jaribio tasa la kukandamiza haki, lakini Mwenyezi Mungu (swt) anaahidi:

[يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [As-Saff: 8]. Juhudi za utawala wa Kibaniani za kufuta historia yake ya kukalia kwa mabavu ardhi ya Waislamu kwa ukoloni, ukiukaji wake wa haki za binadamu, na kujitolea mhanga kwa Mujahidina kutachochea tu azma ya Umma. Utaifa na demokrasia vimethibitika kuwa nyenzo za mgawanyiko, zilizowekwa na dola za kikoloni ili kuwadhoofisha Waislamu.

Suluhisho pekee ni kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo itaunganisha ardhi za Waislamu, kukomboa maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu kama Kashmir, Palestina, na Uyghuristan, na kutabikisha Uislamu ili kulinda heshima, maisha, na akili ya Ummah. Kumbukumbu jumla ya Waislamu haiwezi kutawaliwa na marufuku au viatu – Ummah utasimama, insha'Allah, kuvunja uvamizi na kusimamisha uadilifu wa Uislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mohamad Bhat – Kashmir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu