Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 555
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Licha ya kuongezeka kwa wito wa kusitisha vita vya Mayahudi mjini Gaza, jeshi la Mayahudi linaendelea kumwaga damu ya watu wasio na hatia katika kambi za watu waliokimbia makaazi yao huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kufanya mauaji mengine ili kuongeza rekodi yake nyeusi.
Katika tukio ambalo limekuwa la kusikitisha, watu waliamka siku chache zilizopita na kushuhudia maafa mengine ambayo yalisababisha vifo vya watu tisa wasio na hatia katika ajali iliyotokea kwenye Barabara ya Kanda katika Jimbo la Monufia, chini ya wiki moja baada ya maafa ya kuhuzunisha ambapo wasichana wachanga kumi na nane waliangamia katika ajali sawia, ikitofautiana na ile ya awali tu na kwa idadi ya wahasiriwa. Barabara ya Kanda - ambayo serikali imekuwa ikiitangaza kwa muda mrefu kama "mafanikio ya kitaifa" - imekuwa shahidi wa kudumu wa upuuzi wa yale yanayodaiwa kuwa mafanikio yanayosifiwa na watawala huku wakijificha nyuma ya mabango ya vyombo vya habari vya uwongo na kupuuza haki msingi ya watu: kuishi kwa usalama kwenye barabara ambazo hazinyakui maisha yao.
Marais wa nchi na serikali za nchi wanachama wa NATO walikutana jijini The Hague, Uholanzi mnamo tarehe 24-25 Juni.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni lilifanya kikao maalum kujadili hali ya Afghanistan. Katika mkutano huu, Roza Otunbayeva, mkuu wa Misheni ya Misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA), aliwasilisha mfumo mpya wa kina unaoitwa "Mpango wa Mosaic." Alisisitiza kuwa mpango huu haulengi "kusawazisha hali nchini Afghanistan," bali unalenga kuendeleza maslahi ya kweli ya watu wa Afghanistan.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Palestina mjini Gaza, Dkt. Munir Al-Barsh, alifichua kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaokufa kwa njaa, na kuthibitisha kwamba uvamizi "unafurahi kuwaua," huku kukiwa na mzingiro unaoendelea, kufungwa kwa vivuko, na kupuuza mfumo wa kimataifa. Katika mahojiano katika Chaneli ya Al Jazeera, Al-Barsh alisema kuwa idadi ya watoto waliouawa shahidi kutokana na utapiamlo uliokithiri imefikia 66 hadi sasa, kati yao wa hivi punde ni mtoto mchanga wa miezi mitatu Jouri Al-Masri, akibainisha kuwa makundi yaliyo hatarini zaidi, hasa miongoni mwao ni watoto, wamekuwa wahanga wakuu.
Makundi yenye silaha ya Rohingya yameanza kusajili kutoka kambi za wakimbizi za Cox's Bazar kusaidia katika mapigano dhidi ya Jeshi la Arakan huko Rakhine. Taarifa hiyo ilifichuliwa katika ripoti moja ya Shirika la Kimataifa la kutatua Migogoro yenye kichwa "Bangladesh/Myanmar: Hatari za Waasi wa Rohingya". Ripoti hiyo inabainisha kuwa, baada ya Jeshi la Arakan kupata ushindi dhidi ya jeshi la Myanmar huko Rakhine, makundi ya Rohingya yamezidi kuwa changamfu na yamekubali kufanya kazi kwa pamoja dhidi ya Jeshi la Arakan, kundi ambalo lenye Mabudha wengi wa Rakhine kuwa kambi yake. (The Business Standard, 18 Juni 2025)
Wiki hii iliyopita kumeshuhudiwa vurumai kubwa la vyombo vya habari na kisiasa kutokana na machapisho ya mitandao ya kijamii ambapo Waislamu waliwapongeza wahitimu wa mwaka huu huku pia wakiwasilisha mtazamo wa Kiislamu kuhusu kupanda malori ya kuhitimu yenye sifa ya ulevi na tabia mbaya.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inauona utambuzi huu kama sehemu ya mchakato mpana ambao kwao utawala wa sasa utayeyushwa hatua kwa hatua ndani ya mfumo wa kimataifa wa kisekula wa dola ya kitaifa. Mfumo huu, baada ya muda, utaiweka mbali serikali hii na lengo kuu la Kiislamu la kusimamisha na kubeba Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Zaidi ya hayo, utambuzi huo unaweza kuigeuza Afghanistan kuwa uwanja wa vita vya kiushindani kati ya dola za kikanda na kimataifa.
Semina ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kwa mnasaba wa Mwaka Mpya wa Kiislamu kwa kichwa "Hijrah... Kuzaliwa kwa Dola ambayo itaikoa Gaza."