Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 4 Muharram 1443 | Na: 1443/01 |
M. Alhamisi, 12 Agosti 2021 |
Raisi Japarov wa Kyrgyzstan Kamwe Hataweza Kusitisha Wimbi la Dawah Kupitia Kuwakamata Walinganizi Wake wa Kike
(Imetafsiriwa)
Kwa mujibu wa huduma ya habari ya Idara Kuu ya Mambo ya Ndani ya jimbo la Chuy, mwanaharakati mmoja katika Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir, mzaliwa wa mkoa wa Jalal Abad, katika wilaya ya Alamüdün ya jimbo la Chuy, alikamatwa.
Arstanaliava Bakhtikul Tajimirzayavna, mwenye umri wa miaka 41, pia alihukumiwa mara mbili hapo awali kwa madai kwamba alikuwa amesajiliwa kwenye mtandao wa kijamii wa kielektroniki na kusambaza nyenzo zenye msimamo mkali, kwa hivyo alielekezwa chini ya kifungu cha 315 (Utayarishaji na Usambazaji wa Nyenzo zenye Msimamo Mkali) cha Kanuni ya Jinai ya Kyrgyzstan katika Daftari la Jumuishi la Makosa na Uhalifu la Idara ya Mambo ya Ndani katika Wilaya ya Alamüdün ya Mahakama ya Jinai ya Alamüdün, ambayo iliidhinisha kusimamishwa kwake kwa miezi miwili kusubiri uchunguzi kabla ya kesi.
Serikali ya Kyrgyz inaendelea kwa kiburi kuwalenga wanawake wa Kiislamu kwa miaka kadhaa, ikiwashutumu kwa ugaidi na kutaka kuchukua mamlaka. Kipjakibayava Serthan Kinjatyavna, aliyezaliwa mnamo Novemba 16, 1960, wenye ulemavu wa kiwango cha pili, alihukumiwa kifungo cha miaka nane gerezani katika Mahakama ya Wilaya ya Pervomaisky huko Bishkek mnamo 10/9/2014. Kıjakibayava pia alikamatwa kwa kazi ya Colzina Kajkinavna Orazbekava, ambaye ameolewa na mama wa watoto wawili, alizaliwa mnamo 17/3/1986 katika jimbo la Naryn, na alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani na mwaka mmoja kifungo cha nje.
Katika mwaka huo huo, Zulfiya Amanova alitozwa faini ya som za Kyrgyz 50,000 baada ya miezi miwili gerezani, na Gomazio Soyotbekovna Tukhtaboeva alihukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani.
Mnamo tarehe 30/9/2014, nyumba kadhaa zilipekuliwa katika jiji la Tash-Komur katika mkoa wa Jalal Abad, kama sehemu ya operesheni ya "kupambana na ugaidi". Kama matokeo ya operesheni hizi, wanawake 7 kati ya umri wa miaka 20 hadi 25 walikamatwa kwa tuhuma za kuwa wanachama wa Hizb ut Tahrir. Kesi za jinai zilifunguliwa dhidi yao.
Mnamo 18/11/2014, nyumba za wanawake kadhaa madhaifu walioshukiwa kuwa wanachama wa Hizb ut Tahrir zilipekuliwa huko Bishkek na Chuy: K.W. ambaye alizaliwa mnamo 1989 katika kijiji cha Mangit, Wilaya ya Arvan, Wilaya ya Osh, ambaye kwa sasa anaishi Bishkek, alizaliwa mnamo 1988 katika Wilaya ya Ak Tallin, Wilaya ya Naryn, ni mwalimu wa shule ya michezo, na pia J.A. ambaye anaishi katika kijiji cha Igki Su katika wilaya ya Issyk Kul wilayani Chuy, na alizaliwa mnamo 1987, jimbo la Issyk Kul, katika wilaya ya Tüp. Pia katika wilaya ya Issyk Kul zile zinazoitwa nyenzo zenye msimamo mkali zilipatikana katika nyumba ya K.J. aliyezaliwa mnamo 1984, na alipewa adhabu anuwai.
Nidhamu fisidifu ya leo ya kidemokrasia haiwezi kutatua matatizo ya wanadamu. Hata watu wa Ulaya na Amerika, ambao hubeba mfuimo mbovu kote ulimwenguni, wanalia kwamba mfumo huu unapaswa kutupwa kwenye jaa la taka. Zama Urasilimali zimekwisha. Hauwezi kuiokoa dunia kutokana na uharibifu ulioleta.
Vita vilivyotangazwa na serikali ya Kyrgyz dhidi ya Uislamu chini ya pazia la kupambana na misimamo mikali, ili kumridhisha mtawala wake wa Urusi, vimeilazimisha kutekeleza dori hii iliyotawalishiwa kwa ukamilifu. Hawaoni haya kuwafunga wanawake madhaifu hata kama wana watoto wadogo.
Kyrgyzstan, mithili ya nchi zengine za Asia ya Kati, imefikia kilele cha umaskini na kuna mambo kadhaa huko ambayo bado hayajashughulikiwa. Pamoja na hayo, serikali hii kibaraka haiwezi kutatua shida za ukosefu wa ajira, janga la kiuchumi, shida za kijamii, madeni ya serikali kwa nchi za nje, mfumo wa matibabu uliopooza, nk., lakini ina uwezo tu wa kuwafunga wanawake dhaifu wanaofanya kazi ya kurudisha sheria za Mwenyezi Mungu (swt) maishani. Ni aibu ilioje hii?! Bali, aibu ya kesho Akhera itakuwa kali na kubwa zaidi.
Leo, Hizb ut Tahrir inawasilisha, kupitia machapisho yake na tovuti za mawasiliano ya elektroniki, malengo yake, shughuli, na madhumuni ya amali zake. Hivyo basi, kutoa taswira msimamo mkali ya chama hiki na kukishutumu kutafuta mapinduzi ya vurugu dhidi ya serikali kumepitwa na wakati, na ni ngumu kuushawishi umma jumla kwa hili, lakini serikali inayoongozwa na Japarov ingali inajaribu kuwashawishi wengi uongo huu.
Sasa, wamepitwa na gari ya moshi, na sifa njema zote ziwe kwa Mwenyezi Mungu (swt), Umma wa Kiislamu umeamka, na umegundua kuwa maisha ya halisi ya Kiislamu yatakuwa chini ya dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. Umegundua pia kuwa hili haliwezi kufanywa kwa njia yoyote chini ya mfumo wa kisekula uliojengwa juu ya msingi wa kutenganisha dini na serikali.
Ndio maana kina dada hawa Waislamu wataendelea na juhudi zao licha ya kifungo cha miaka gerezani. Na serikali itabaki haina nguvu mbele ya wanawake hawa ambao hubeba wito wa Uislamu licha ya kumiliki kwake silaha na nguvu za kijeshi.
Je! Ni wanawake wangapi wapya wanaojiunga na da'wah, kama Bakhtikul, Sirhan na Zulfiya Amanova, licha ya kukamatwa na kudhalilishwa?! Kama ambayvo washirikina mjini Makka hawakuweza kuushinda Uislamu, genge la Japarov halitaweza kuwazuia wabebaji hawa wa ulinganizi wa Uislamu kutokana na kutekeleza amali zao. Mwenyezi Mungu (swt) ameahidi kuifanya Dini Yake (mfumo wa maisha) itawale duniani, Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ * هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawba: 32-33].
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |