Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Familia za Afghanistan Zawalevya Watoto wao ili Kukabiliana na Njaa

Mnamo Novemba 24, 2022, BBC iliripoti juu ya uhaba mkubwa wa chakula ambao unakumba Afghanistan. Mgogoro huo ni kiasi kwamba Abdul Wahab, baba mmoja wa kijijini, ananukuliwa akisema, "Watoto wetu wanaendelea kulia, hawalali, hatuna chakula. Kwa hiyo tunakwenda kwenye duka la dawa, tunachukua vidonge na kuwapa watoto wetu, hivyo wanahisi kusinzia."

Soma zaidi...

China Yawalazimisha Wanawake wa Kiislamu wa Uyghur kuolewa na Makafiri ili Kuufuta Uislamu kutoka Turkestan Mashariki

Mnamo tarehe 16 Novemba 2022, gazeti la Telegraph iliripoti juu ya dhurufu za ndoa ya kulazimishwa ambayo inawasibu wanawake wa Kiislamu huko Turkestan Mashariki. Makala hayo yana kichwa "Wachina walipwa kuwaoa Waislamu katika mpango wa kuwaangamiza Wauyghur".

Soma zaidi...

Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Wanawake na Haki Unatumikia CEDAW

Mnamo Novemba 4-5, 2022 jijini Istanbul, “Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Wanawake na Haki” ulifanyika, kwa hotuba ya ufunguzi ya Rais Recep Tayyip Erdogan. Uliandaliwa na kikundi cha utetezi wa wanawake, Chama cha Wanawake na Demokrasia (KADEM) pamoja na Wizara ya Huduma za Familia na Jamii. Tamko la mwisho la mkutano huo lilisisitiza umuhimu wa familia yenye nguvu kwa jamii yenye nguvu.

Soma zaidi...

Shambulizi juu ya Khimar (Kitambaa cha kichwa) barani Ulaya ni Vita vya Hadhara Dhidi ya Hadhara "Jibu kwa Makala ya Jean Chichizola"

Mnamo tarehe 11/09/2022, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kiliwasilisha mjadala kuhusu "Shambulizi dhidi ya Hijabu barani Ulaya", ambapo washiriki walizungumza kuhusu vikwazo ambavyo wanawake wa Kiislamu katika nchi za Magharibi wanakumbana navyo, ambao ulimkasirisha mwandishi wa habari Jean Chichizola kiasi kwamba aliandika makala yaliyochapishwa mnamo tarehe 19/10/2022 kwenye Gazeti la Le Figaro, yenye kichwa "Ufaransa inatuhumiwa kutaka "kuuondoa Uislamu" kwa vijana wa Kiislamu.

Soma zaidi...

Watoto wa Palestina Wanalilia Majeshi ya Waislamu

Tangu mwanzoni mwa 2022, zaidi ya watoto 45 wa Kipalestina wameuawa shahidi, na uvamizi wa Kiyahudi umeongezeka katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem, katika wiki chache zilizopita, ambao umesababisha vifo vya watoto zaidi, wa mwisho wao akiwa ni mtoto Mahmoud Al-Samoudi, mwenye umri wa miaka 12, ambaye alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.

Soma zaidi...

Kwa kukosekana Khilafah, Watoto wa Ummah wetu nchini Iraq Wanaanikwa kwa Hofu za Utaifa

Mnamo tarehe 29 Septemba 2022, shirika la Habari la ‘Arab News’ liliripoti juu ya mashambulizi ya droni yaliyoanzishwa na Iran kwa kile kinachoitwa mawakala wa waasi wa Kikurdi katika eneo hilo. Milipuko ilitokea katika mji wa Irbil, Kurdistan ya Iraq na kushambulia shule moja iliyokuwa imejaa wanafunzi. Waandishi wa habari katika eneo la tukio walisambaza picha za watoto wa shule waliotapakaa damu katika eneo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq.

Soma zaidi...

Watoto wa Afghanistan na Unafiki wa Kimagharibi

Tangu utawala wa Marekani uondoke Afghanistan na serikali ya Taliban kuchukua madaraka, maamuzi ya nchi za Magharibi yalianza kuongezeka, hasa baada ya kundi la Taliban kuchukua maamuzi ambayo Magharibi inayaona kuwa hayaendani na hadhara na mtindo wake wa maisha, kama vile kulazimisha niqab kwa wanawake na kutenganisha madarasa kati ya wanaume na wanawake, pamoja na maamuzi mengine.

Soma zaidi...

Kipindupindu Kinawaua Watu wa Syria, Hivyo Iko Wapi Dola ya Kuwanusuru?!

Wizara ya Afya ya Utawala wa Syria ilitangaza mnamo Jumatatu kuwa mkurupuko wa kipindupindu katika maeneo kadhaa umewauwa watu 29, vifo na majeruhi vilikolea katika jimbo la kaskazini la Aleppo, ambapo watu 25 walithibitishwa kufariki, na maelfu kadhaa ya visa vinavyoshukiwa kuripotiwa kote nchini kuanzia Septemba 19, kulingana na data iliyopatikana na chama cha misaada kutoka Kitengo cha Afya cha Serikali ya Syria (GoS), Idara ya Kibinafsi ya Mamlaka ya Afya ya Mitaa, Kaskazini na Mashariki mwa Syria.

Soma zaidi...

Lau Tungekuwa na Ngao ya Ulinzi na Imam, Mayahudi Wasingesubutu Kunyakua Ardhi Yetu na Kuifisidi

Mnamo tarehe 9/23/2022, Al Jazeera Kiingereza ilichapisha ripoti kuhusu mateso ya watu wa Masafer Yatta [Palestina] kutokana na mashambulizi ya walowezi. Ripoti hiyo ilinukuu ushahidi wa wanawake wa eneo hilo, waliozungumzia mateso yao na familia zao kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wavamizi na makundi ya walowezi, ambapo wanapigwa, kupigwa risasi za moto, kushambuliwa kwa gesi na kukamatwa.

Soma zaidi...

Watoto Wapendwa wa Ash-Sham Wafariki Baada ya Boti za Wakimbizi Kuzama. Je, Tunapoteza Wangapi Zaidi Bila Khilafah?!

BBC iliripoti mnamo tarehe 23 Septemba 2022 kwamba wakimbizi wahamiaji 71 walipatikana katika mashua inayozama nje ya pwani ya Syria. Makumi wameripotiwa kufariki. Watu 20 kati ya walionusurika walipelekwa katika jiji la Tartus kutibiwa hospitalini. Wanawake na watoto wa Lebanon, Syria na Wapalestina walikuwa miongoni mwa watu 120 hadi 150 waliokuwemo ndani.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu