Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  1 Rajab 1444 Na:
M.  Jumatatu, 23 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chazindua Kampeni ya Kimataifa:

“Mabadiliko Halisi ni kwa kupitia Ulinganizi wa Khilafah PEKEE”

(Imetafsiriwa)

Leo, ulimwengu uko katika machafuko na giza, karibu na mbali. Mateso na taabu za wanadamu zinaongezeka siku hadi siku huku mataifa yakiingia kwenye mgogoro mmoja hadi mwingine. Umaskini, utovu wa usalama wa kifedha, njaa, mauaji ya halaiki, uvamizi wa kikatili, udikteta, vita vya kinyama, kuvunjika kwa familia, maisha yenye uharibifu, milipuko ya uhalifu, unyanyasaji dhidi ya wanawake, matatizo ya afya na elimu na matatizo mengine yanayolemaza yanakumba nchi kote ulimwenguni, chini ya mifumo ya kibinadamu iliyoharibika na uongozi mtepetevu ambao haujui jinsi ya kuchunga ipasavyo mambo ya watu wao na kutimiza mahitaji yao. Badala yake sera, sheria na matendo yao yanazidisha mateso ya watu wao.

Ardhi za Kiislamu na dunia hazistahili ziwe katika hali hii ya giza, uharibifu, majanga na migogoro inayoonekana kutokuwa na mwisho. Hata hivyo, mabadiliko ya halisi hayawezi kufikiwa kwa kufanya mabadiliko madogo madogo kwa mifumo yenye dosari ambayo inatabikishwa kwa sasa, au mabadiliko ya hatua kwa hatua – kurekebisha tu ubavu wa matatizo, au kutoa ufumbuzi wa plasta ya kunata, au kurudisha mzunguko wa mifumo ya kidemokrasia ya kisekula iliyofeli kwa nyuso mpya kwenye usukani - mifumo ambayo imethibitisha mara kwa mara, kutokuwa na uwezo wa kutatua matatizo ya wanadamu, kuwalinda wanaodhulumiwa au kutoa haki - na inadumisha tu ahadi ya kurefusha machungu na mateso ya Umma wa Kiislamu na wanadamu.

Mabadiliko halisi yanatuhitaji sisi kama Waislamu kukumbatia ruwaza zaidi ya hali ilivyo sasa, mfumo wa sasa wa kibepari wa kiulimwengu, mifumo ya sasa iliyobuniwa na mwanadamu. Inatuhitaji kuinua macho yetu juu ya njia mbovu na angamivu za kutawala na kuendesha mambo yetu tunayoyaona yametuzunguka. Inahitaji mabadiliko makubwa, ya msingi na mapana. Inahitaji kuzaliwa kwa mfumo badali unaobeba masuluhisho halisi kwa matatizo ya binadamu. Inatutaka sisi kama Waislamu kuregea katika yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametuitia kwayo - Sheria Zake, Mfumo Wake, na kuutabanni ujumbe wetu wa Kiislamu, ili kusimamisha uongozi wa kweli kwa wanadamu: Khilafah kwa Njia ya Uislamu. Ni Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndio utakaoleta mafanikio kwa Ummah huu na kwa wanadamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 123-124].

Rajab hii, mwezi unaoadhimisha mwaka wa 102 wa kukosekana kwa Khilafah, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kitazindua kampeni ya kimataifa yenye kichwa: "Mabadiliko Halisi ni kwa Kupitia Ulinganizi wa Khilafah PEKEE". Itachunguza maoni ya sasa kuhusu jinsi mustakbali mwema zaidi unavyoweza kupatikana kwa ardhi za Kiislamu; jinsi Khilafah itageuza machafuko kuwa mwamko kwa kanda hiyo na jinsi inavyobeba masuluhisho halisi kwa matatizo ya wanadamu; na pia itajadili dori ya Waislamu katika kuleta mabadiliko halisi katika ulimwengu wa Kiislamu na kimataifa; na kama mabadiliko msingi na kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ni ndoto au inawezekana kweli. Kampeni hii inaweza kufuatiliwa kwenye: www.hizb-ut-tahrir.info na ukurasa wa Facebook: https://www.facebook.com/womenscmoht. Link ya video ya utambulishaji wa kampeni: https://youtu.be/zRk5dx2t1ew

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu