Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  15 Sha'aban 1444 Na: 1444 H / 029
M.  Jumanne, 07 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhamiaji Haramu au Nia ya Ubaguzi wa Rangi?
(Imetafsiriwa)

Katika ajali mbaya inayozidisha maafa mengi yanayoshuhudiwa na Ummah, boti iliyokuwa imebeba wahamiaji waliotoka Uturuki kuelekea Italia, wakiwa na matumaini ya kuishi maisha salama na yenye staha, ilizama. Kifo kiliwatangulia, na zaidi ya watu 65 walikufa maji, wakiwemo watoto wapatao 12 na watoto wachanga kati ya watu 200. Muitikio wa tukio hilo unaonyesha ukubwa wa maafa yaliyoupata Ummah miaka 102 iliyopita, katika siku hizo. Tangu kuvunjwa kwa dola yetu, Khilafah ya Kiislamu, tumekuwa kama mayatima kwenye meza za watu wanyonge. Maisha yetu, damu na heshima hazina thamani. Ardhi zetu ni ruhusa kwa adui wetu kutushambulia katikati ya nyumbani kwetu, na hakuna imam tunayeweza kupigana na kujikinga nyuma yake. Nchi yetu haina ukaribishaji tena, hakuna usalama, hakuna uchungaji, hakuna utu, hakuna hata kiwango cha chini cha maisha ya staha. Muislamu anakimbia pamoja na familia yake, akitarajia kupata nchi ambayo ataishi kwa heshima, lakini bila mafanikio. Nyinyi ni Waislamu kutoka ulimwengu wa tatu; kwa hiyo mumehukumiwa kutupwa mukiwa hai na mukiwa mumekufa, hakuna anayesongea kuwachunga katika maisha yenu kama ambavyo hakuna anayekimbilia kukuokoeni katika ajali, na hakuna anayejutia kifo chenu!

Huu ni ulimwengu unaotufurikia kwa kauli mbiu za uhuru na haki za binadamu na kuwalazimisha watawala wa Kiislamu kutia saini makubaliano na mikataba ya kimataifa ya haki za watoto na wanawake na kuziweka rehani kwa kubadilishana na Benki ya Dunia kwa njia ya mikopo yenye riba. Ni ulimwengu wa kinafiki ambao mashua hii iliyobeba watu waliokandamizwa wanaotafuta haki na uhuru ilizama. Nyangumi wake walikimbilia ili kuhalalisha kutochukua hatua kwao, na wakashindana katika kuwatupia tuhuma samaki wadogo katika bahari ya uhalifu ili watoke bila hatia ya damu ya familia zilizokufa kwa kuzama.

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye alichaguliwa mwaka jana kwa ahadi ya kukomesha wimbi la wahamiaji nchini Italia, alionyesha "majuto makubwa" kuhusu tukio hilo, akilaumu vifo hivyo kwa wasafirishaji haramu. "Ni unyama kufanya biashara na maisha ya wanaume, wanawake na watoto kwa bei ya tikiti waliyolipa kwa ahadi za uongo za safari salama," alisema katika taarifa yake. Ama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezitaka nchi kufanya zaidi kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji, na kusema, “Maadamu magenge ya wahalifu yanadhibiti njia za wahamiaji, matukio ya kuzama maji yataendelea.”

Je, mfumo wa kimataifa ungeridhika na taarifa kama wahamiaji wangekuwa Waukraine?! Je, wangeridhika na ufuatiliaji na kurusha tuhuma kupitia vyombo vya habari ili kuipamba sura yao na kufinika damu mikononi mwao?!

Waislamu leo wamo katika haja kubwa ya mfumo wa Khilafah unaolinda ardhi zetu, unaohifadhi neema zake kwa ajili yetu, na unaotudhaminia maisha ya staha, unaotuokoa na matatizo ya kuhama na taabu za mateso hapa duniani. Khalifa anawajibika kwa raia wake na anachelea kuwa Mwenyezi Mungu atamuhisabu kwa ajili yao, kwa hiyo yeye ni mchungaji wao ambaye anachelea kuwa mgumu juu yao na Mwenyezi Mungu atakuwa mgumu juu yake. Na wanadamu wote wanahitaji Khilafah ambayo msingi wake ni kuwaheshimu watu na kuhifadhi usalama wao kwa njia ya kweli, badala ya kupora mali za watu, kunyonya damu zao, na kisha kuwazamisha kwa kauli mbiu za uwongo. Ni dola yenye maadili inayobeba kheri duniani na ujumbe wake ni kuupeleka Uislamu kwa watu wote ili wamuabudu Mwenyezi Mungu kama atakavyo. Haitendi kulingana na maslahi na haiendelei mbele kwa mtazamo wa ubaguzi wa rangi kwa watu. Inaongozwa na maneno ya Mola Mlezi wa walimwengu wote:

  [وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّى يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ]

Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. [At-Tawbah 9:6]. Hata washirikina wakipigana, Mola wetu Mlezi ametuamrisha kuwalinda ikiwa watakimbilia kwetu, na tuwafikishe mahali pao pa usalama.

Ewe Mwenyezi Mungu, urehemu Ummah wa Muhammad, kwa kufuata njia na uongofu wake, kwani hakuna mlinzi, msaidizi, wala mtawala ila Wewe. Njia zimetukuzwa, basi tutunze.

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu