Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  17 Rajab 1444 Na: 1444 H / 028
M.  Jumatano, 08 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kifungo, Kutengwa, Hakuna wa Kunusuru!!
(Imetafsiriwa)

Hivi majuzi, mfungwa wa Kipalestina, Shorouq Al-Badan, aliachiliwa huru kutoka Gereza la Damon baada ya kuwa katika kizuizi cha kiidara kilichochukua miezi 14. Alisema kuwa hajihisi kuwa uhuru, na anahisi uchungu na hofu kwa marafiki zake gerezani, ambao hakuweza hata kuwaambia kwaheri. Idara ya Gereza la Damon ilianzisha mashambulizi mapya ya ukandamizaji dhidi ya wafungwa wa kike kama adhabu kwa kusherehekea kwao operesheni ya shahidi Khairy Alqam katika Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu. Vikosi vya ukandamizaji vilijaza vyumba vya wafungwa kwa maji baridi, kisha wakaingia ndani na kuwapiga na kuwaburuta kwa kutumia vyuma vya umeme, na kuwahamishia kwenye korokoro za upweke.

Kulingana na data ya Klabu ya Wafungwa wa Palestina, uvamizi huo umewakamata wanawake 172 wa Kipalestina katika kipindi mwaka uliopita, na idadi ya wafungwa wa kike leo ni 28, wakiwemo watoto watatu. Miongoni mwa wafungwa wa kike, sita walijeruhiwa wakati wa kukamatwa kwao. Hali ya mfungwa, Israa Jaabis, inatajwa kuwa kesi ngumu zaidi, kwani ana ulemavu mkubwa katika mwili wake, kutokana na majeraha ya moto aliyoyapata wakati wa kukamatwa kwake mwaka 2015.

Ama Gereza la Damon, liko eneo la Daliat al-Carmel, wilaya ya Haifa inayokaliwa kimabavu, na ni mojawapo ya magereza ya umbile la Kiyahudi, sehemu yake moja ikiwa imetengwa kwa ajili ya wafungwa wa kike. Gereza hilo linarudi nyuma katika kipindi cha Mamlaka ya Uingereza, lilipoanzishwa kama ghala la tumbaku, kisha likabadilishwa kuwa moja ya magereza makali zaidi ya uvamizi huo ya wafungwa wa kiume na wa kike.

Dhulma za kimwili dhidi ya wafungwa wa kike zimeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ikilinganishwa na miaka iliyopita. Katika Gereza la Damon, wafungwa wa kike wanaishi katika ukandamizaji wa kila siku kupitia kifungo cha upweke, ambacho idara ya gereza hilo hutumia mara kwa mara kuwaadhibu kulingana na kisingizio chochote. Pindi mfungwa anapotengwa, ananyimwa "cantina", yaani, kantini ya gereza, na "fora", yaani, kwenda nje katika uwanja wa gereza. Pia anazuiwa kuchukua nguo zake, na anapewa blanketi yenye unyevu na harufu mbaya, na mlinzi wa jela anawekwa kwenye mlango wa seli ya gereza. Yaani, mfungwa wa kike anatengwa kabisa na uhalisia, kwa hiyo hana mawasiliano na wafungwa wa kike au wakili, na anazuiwa kutembelewa na wageni. Hii ni bila ya kutaja kamera za uchunguzi zilizowekwa gerezani humo ambazo zinakiuka faragha yao. Wafungwa hao wa kike walilalamika dhidi ya kamera hizo katika Gereza la Hasharon.

Miaka inapita kutoka kwa maisha ya wafungwa wa kike walio chini ya hali ngumu na zisizovumilika mbali na familia zao, waume, na watoto wao, na hakuna mtu yeyote wa kuwapunguzia au kuwatetea kutoka kwa mashirika ya haki za wanawake na vyama vya wanawake vivyonadai kujali kwao maisha, utu, na haki za wanawake. Jumuiya na taasisi hizo ambazo mapungufu na malengo yake maovu yamefichuliwa, zinataka kuwadhuru wanawake wa Kiislamu kwa kisingizio cha haki na usawa, lakini kwa hakika wanataka kumtoa nje ya nyumba yake, usafi na utu wake, ili kugeuzwa kuwa mwanamke wa Kimagharibi. Ni Dola ya Khilafah Rashida ya pili pekee kwa Njia ya Utume ndiyo itakayowakomboa wao na mateka wote, na itaikomboa ardhi na kulinda heshima.

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu