Enyi Waislamu: Msiikubali Marekani kama Mpatanishi, Kwa Maana sio tu kuwa ina Upendeleo; bali, ni Sehemu ya Mzozo!
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Januari 15, makubaliano yalifikiwa kusitisha vita dhidi ya Gaza kati ya umbile la Kiyahudi na harakati ya Hamas. Makubaliano hayo yalianza kutekelezwa mnamo Januari 19 mwezi huo huo na yalisimamiwa na nchi tatu: Amerika, Misri na Qatar. Tangu wakati huo hadi leo, umbile la Kiyahudi limetekeleza ukiukaji mwingi wa makubaliano haya na limeshindwa kutimiza wajibu wake mwingi, kama ilivyo kawaida kwa Mayahudi katika khiyana na uvunjaji ahadi na makubaliano.