Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kushiriki katika Mafunzo ya Kijeshi pamoja na Adui wetu ni Fedheha kwa Majeshi yetu na Usaliti kwa Watu wetu mjini Gaza

Mnamo tarehe 1/11/2024, Wizara ya Ulinzi ilitoa taarifa ikisema: “Tunisia itakuwa mwenyeji, kuanzia Novemba 4 hadi 15, wa zoezi la majini la kimataifa “PHOENIX EXPRESS 24”, kwa ushirikiano na Kamandi ya Marekani ya Afrika, kwa ushiriki wa takriban wanajeshi 1,100 na waangalizi wanaowakilisha nchi dada na rafiki 12, ambazo ni Algeria, Libya, Morocco, Mauritania, Senegal, Uturuki, Italia, Malta, Ubelgiji, Georgia, na Marekani, pamoja na Tunisia, nchi mwenyeji.”

Soma zaidi...

Mjumbe wa Marekani Anajihusisha na Udanganyifu na Uongo, Ikifichua Ukweli wa Vita kama Pambano lake na Uingereza

Udhalimu wa Marekani na jinai zake dhidi ya Sudan, na dhidi ya ardhi zote za Waislamu, hautakoma—kama vile inavyowapa Mayahudi silaha ili kuiangamiza Gaza na kuwaangamiza watu wake huku ikizungumzia amani na kusimamisha vita. Ukandamizaji huu utasitishwa tu na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, inayoongozwa na Khalifa mwadilifu anayeisimamisha Dini, kutekeleza Sharia, na kuwatetea waumini na wanaodhulumiwa.

Soma zaidi...

Enyi Wanajeshi wa Misri (Kinana): Ni lini Mtaifuta Aibu ya Utawala wa Kihaini na Kuosha Mikono Yenu kutokana Nao?

Siku chache zilizopita, utawala wa Misri ulikanusha kupokea meli ya mizigo katika bandari ya Alexandria ikiwa imesheheni shehena za silaha na vilipuzi kwa ajili ya umbile la Kiyahudi, licha ya kuwepo ushahidi mkubwa kwamba serikali ya Misri iliipokea, kuwezesha kuwasili kwake, na kutoa msaada unaohitajika na mahitaji mpaka shehena yake ifikie umbile hilo nyakuzi ili kukamilisha mwendo wake wa kuua watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa.

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria Mkao wa Masuala ya Ummah

Sisi, katika Hizb utTahrir / Wilayah Sudan, tunafuraha na taadhima kuwaalika waandishi wa habari, wataalamu wa vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wanaopenda masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika Mkao wa kila mara wa Masuala ya Ummah, ambao utakuwa na kichwa: Sera za Uachishaji kazi na Uteuzi na Njia Isiyoepukika ya Utawala Bora.

Soma zaidi...

Utawala wa Sisi Hautaweza Kuficha Usaidizi wake kwa Umbile la Kiyahudi

Sio tu utawala nchini Misri unaochangia kuunga mkono umbile la Kiyahudi katika vita vyake dhidi ya watoto na wanawake wasio na ulinzi wa Palestina. Badala yake, nchi zinazozunguka na zilizo nje ya eneo linaloizunguka Palestina zinaendelea kutoa msaada wa kibiashara kwa siri na dhahiri, kama ilivyo kwa ukanda wa ardhi unaovuka nchi za Kiarabu unaoanzia Ghuba ya Uarabuni hadi Palestina inayokaliwa kwa mabavu ili kupitisha chakula na vifaa vya viwandani kwa umbile la Kiyahudi, pamoja na biashara inayonawiri kati yake na Uturuki.

Soma zaidi...

Vitendo vya Baraza la Uongozi wa Rais na Serikali yake ni Mithili ya Sarabi Jangwani, na Kuporomoka kwa Sarafu ni Shahidi wa hilo

Sarafu ya nchi katika maeneo yanayodhibitiwa na Baraza la Uongozi wa Rais imeshuhudia mporomoko wa kihistoria dhidi ya sarafu za kigeni kwa wiki kadhaa, huku riyal ya Saudia ikivuka kizuizi cha riyal 535, na dolari ya Marekani ilivuka kizuizi cha riyal 2,000. Wakati huo huo, baadhi ya miji ilishuhudia uasi mdogo wa kiraia na kufungwa kwa maduka ya kupinga kuporomoka kwa sarafu hiyo, na maduka kadhaa ya kubadilisha fedha yalifunga milango yake kwa watu baada ya janga hili la kuporomoka na kutoweza kwa serikali kutafuta suluhisho mwafaka kwa hilo.

Soma zaidi...

Ushenzi ni Ufaransa na Historia yake ni Mbaya na Nyeusi, Ewe Macron

Utovu wa nidhamu wa Rais wa Ufaransa Macron umefikia kilele chake kwa kauli zake za kishenzi alizozitoa katika Bunge la Morocco mnamo siku ya Jumanne, 29/10/2024; kuwakashifu Mujahidina nchini Palestina, wanaotetea ardhi na haki zao, kama “washenzi”, na kudai kwamba umbile, halifu vamizi la Kiyahudi lina haki ya kujilinda.

Soma zaidi...

Je! Mauaji na Jinai Hizi Zote Hazijachochea Hisia ya Wajibu kwa wale wenye Vyeo na Medali Kusonga katika Ulinzi wa Watu wa Gaza?!

Alfajiri ya mnamo Jumanne, Oktoba 29, 2024, vikosi vya Kiyahudi vilifanya mauaji mengine ya kutisha kwa kulipua jengo la orofa tano la familia ya Abu Nasr, ambalo lilikuwa lahifadhi watu waliokimbia makaazi yao katika Mradi wa Beit Lahiya kaskazini mwa Gaza. Mauaji haya yalisababisha vifo vya watu 93, wakiwemo watoto wasiopungua 25, huku zaidi ya 40 wakipotea na kadhaa kujeruhiwa, wengi wao wakiwa wamenaswa chini ya vifusi.

Soma zaidi...

Demokrasia Humpa Mwanadamu, Wakiwemo Wasiokuwa Waislamu, Uwezo wa Kufafanua na Kubainisha Imani na Madhehebu Yetu!

Pendekezo la hivi majuzi la Mswada wa Sheria ya Mufti 2024 (Maeneo ya Shirikisho) limezua mjadala mkali kote nchini Malaysia. Tangu kusomwa kwake kwa mara ya kwanza mwezi Julai, Mswada huo umesonga mbele, ukikaribia kusomwa mara ya pili na ya tatu kabla ya kuidhinishwa kamili na bunge. Mwanzo wa Mswada huu unatokana na mjadala unaoendelea kuhusu Ilm al-Kalam (Usomi wa Kiislamu), ambao umeongezeka hivi karibuni nchini Malaysia.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu