- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ummah Unahitaji Khilafah Kulinda Matukufu Yake Sio Mikataba ya Ulinzi ya Kuwalinda Watawala Vibaraka
(Imetafsiriwa)
Habari:
Pakistan na Saudi Arabia zimeingia katika makubaliano ya kihistoria ya ulinzi wa pande zote, ambapo uvamizi wowote dhidi ya dola moja utachukuliwa kuwa shambulizi kwa pande zote mbili. ‘Mkataba wa Kimkakati wa Ulinzi wa Pamoja’ ulitiwa saini na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif na Mfalme Mtarajiwa wa Saudia Mohammad Bin Salman katika Kasri la Al-Yamamah jijini Riyadh mnamo Jumatano, 17 Septemba 2025. (Dawn)
Maoni:
Kufuatia shambulizi la umbile la Kiyahudi dhidi ya Qatar mnamo tarehe 9 Septemba 2025 ambalo lililenga uongozi mkuu wa kisiasa wa Hamas, makubaliano haya ya ulinzi wa pande zote yanaonekana kuwa jibu dhidi ya uvamizi wa umbile la Kiyahudi. Wasemaji wa serikali nchini Pakistan wanatangaza kuwa ni ushindi na ishara ya mafanikio ya sera ya kigeni ya Pakistan. Pia serikali hiyo inayawasilisha kwa vile wamepewa heshima ya kukabidhi jukumu la kulinda maeneo matakatifu ya Makah na Madina.
Makubaliano ya ulinzi kati ya Pakistan na Saudi Arabia si jambo geni. Ushirikiano kati ya dola hizo mbili ulianza mwaka 1967 na kuimarika baada ya kutekwa kwa Msikiti Mtukufu mnamo 1979, pindi vikosi maalum vya Pakistan viliposaidia wanajeshi wa Saudia kuregesha Masjid al-Haram. Mnamo mwaka wa 1982, pande hizo mbili zilianzisha mafungamano ya kiusalama kupitia Mkataba wa Ushirikiano wa Usalama wa Baina ya Nchi hizo mbili ambao uliwezesha wanajeshi wa Saudia kupata mafunzo ya Pakistan, usaidizi wa kiushauri na kutumwa katika ardhi ya Saudia. Wakati fulani, wanajeshi 20,000 wa Pakistan waliwekwa katika ufalme huo, na Saudi Arabia ikawa mnunuzi mkuu wa silaha zilizotengenezwa Pakistan.
Muungano wa Kijeshi wa Kiislamu wa Kupambana na Ugaidi (IMCTC), muungano wa kijeshi wa kukabiliana na ugaidi baina ya nchi 43 wanachama katika ulimwengu wa Kiislamu, ulitangazwa kwa mara ya kwanza na waziri wa ulinzi wa Saudi Arabia Mohammad bin Salman Al Saud (sasa mfalme mtarajiwa), mnamo tarehe 15 Disemba 2015. Mnamo tarehe 6 Januari 2017, Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Pakistan Raheel alitajwa Kamanda wa Kwanza wa IMCTC, na bado angali anaongoza kikosi hiki. Muungano huo una kituo cha operesheni za pamoja jijini Riyadh, Saudi Arabia. Lakini huu unaoitwa muungano wa kijeshi haujawahi kutumika kukomesha ugaidi wa umbile la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wa Palestina na wa kanda hiyo. Hata hivi sasa baada ya Qatar kushambuliwa na umbile la Kiyahudi, muungano huu haukuamriwa hata kuanza mazoezi ya kijeshi.
Kuhusu furaha inayoonyeshwa na watawala wa Pakistan kwa kupata fursa ya kuilinda Misikiti miwili Mitukufu, mtu anashangaa kwa nini hawana shauku ya kukomboa eneo la tatu takatifu katika Uislamu na Kibla cha kwanza, Masjid Al-Aqsa vile vile ambayo imekuwa chini ya kukaliwa kimabavu tangu 1967 na kutoheshimiwa na majeshi ya Kiyahudi kila uchao, huku alhamdulillah Masjid Al-Haram na Masjid An-Nabawwi haiko chini ya uvamizi wa umbile la Kiyahudi.
Tangu tarehe 7 Oktoba 2023 Waislamu wa Pakistan wamekuwa wakiyataka majeshi yao kupelekwa kuwanusuru Waislamu wa Gaza, kwa ajili ya ukombozi wa Masjid Al-Aqsa na kulifuta umbile la Kiyahudi, lakini matakwa yao daima yalikataliwa kwa kisingizio cha kuzorota kwa hali ya ndani huko Khyber Pakhtunkwa na Baluchistan, mikoa miwili ya Pakistan, na kwa sababu ya tishio la uvamizi wa India. Uasi wowote katika mikoa hii uliomalizwa, badala yake umeongezeka, wala tishio la India halijapungua badala yake India inasubiri wakati unaofaa ili kuanza tena Operesheni Sindoor dhidi ya Pakistan. Kwa hivyo inathibitisha kwamba kumekuwa hakuna suala la uwezo wa kupigana katika nyanja mbalimbali, suala daima limwekuwa ni kile ambacho Mfumo wa Ulimwengu wa Amerika unataka kutoka Pakistan. Inaonekana kana kwamba dori ya Pakistan katika mpangilio wa usalama wa Mashariki ya Kati utainufaisha Marekani, hivyo utawala wa Trump ukaruhusu Saudi Arabia na Pakistan kutia saini makubaliano hayo ya ulinzi kwani haimkiniki kuwa uongozi wa watumwa wa nchi zote mbili unaweza kuchukua hatua kama hiyo ya kimkakati peke yao, kwa kuzingatia maslahi ya Waislamu wa eneo hilo.
Mawazo kama vile NATO ya Waislamu yanayowasilishwa na wanasiasa na watawala ni majaribio ya kutuliza hasira ya Ummah kwa kutochukua hatua kwa watawala wa Waislamu kuwasaidia kaka na dada zao huko Gaza. Makubaliano ya ulinzi kati ya watawala wa Waislamu si chochote zaidi ya kujaribu kuzilinda tawala zao. Ni aibu kwamba watawala wa Waislamu wanaweza kuungana kwa ajili ya kulinda serikali zao lakini si kwa ajili ya kuikomboa Palestina na Gaza. Makubaliano ya Ulinzi wa Pamoja kati ya Saudi Arabia na Pakistan hayana thamani yoyote kwa sababu ushirikiano huu hautawahi kuanzishwa dhidi ya muungano wa Marekani-Yahood (Mayahudi) hata kidogo.
Msingi wa umoja wa Waislamu unapaswa kuwa Aqida ya Kiislamu. Uokovu wa Umma wa Kiislamu upo katika umoja na njia pekee ya kuunganisha Ummah ni kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Kitu chochote kando na kuanzishwa kwa Khilafah daima kitakuwa ni udanganyifu kama vile kuzaliwa kwa OIC na Jumuiya ya Waarabu kumekuwa ni uhadaifu. Uislamu unatuamrisha kuwa Ummah mmoja wenye mtawala mmoja, Khalifa, sio Ligi ya Mataifa.
[إِنَّ هَذِهٖ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَّاحِدَةً وَّأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ]
“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiyah, 21:92]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shahzad Shaikh – Wilayah Pakistan