Imarati Yafungua Mlango Kuuza Pombe ili Kushajiisha “Uvumilivu” kwa Haram Hiyo
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 3 Januari, 2023, The National iliripoti kwamba Imarati itakuwa ikiondoa ushuru wake wa 30% kwa mauzo ya pombe. Hatua hizo zilielezwa kuwa ni mpango wa kukuza sekta ya utalii na kuimarisha uhamiaji wa msimu wa wageni ambao hushindana na mashirika ya kikanda ambayo yanavutia wageni wasiokuwa Waislamu wanaotafuta starehe katika msimu wa likizo ya kimataifa.