Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Matokeo ya Utawala wa Urasilimali na Demokrasia kwa Waislamu na Walimwengu Wote

Miaka 100 imepita tokea tarehe 28 Rajab ya 1342 H, ambapo Khilafah ya Uthmaniya, iliokuwa mrithi wa Dola ya Kiislamu iliyoasisiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Madinatul Munawwarah, kuvunjwa. Kwa miaka mia moja, Ummah mtukufu wa Muhammad (saw), umekuwa kama yatima, umekuwa ukiendelea kukumbana na mateso na maumivu makali chini ya mikono ya maadui zake, wakiwemo viumbe dhaifu waliolaaniwa na Mwenyezi Mungu (swt), Yeye ni Mtukufu na Aliye Mkuu. Hakuna maneno na nguvu zinazotosheleza kutaja maovu yote ya maadui wa Uislamu, ambayo si aliyekuwa hai au hata aliyekufa ameepukana nayo.

Mwenyezi Mungu (saw) amewataka Waislamu kuwa ni Ummah bora kwa maslahi ya viumbe. Wakati huo huo, Bwana wetu Mwenye Mamlaka yote, bila kugawanyika, ameunganisha nafasi hii na wajibu wa kuwaongoza watu, kuwa mlezi, kuhukumu baina yao kwa mujibu wa uongozi wa Uislamu:

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [TMQ 3:110]

Hata hivyo, hivi leo ukweli unaosikitisha wa Ummah wa Kiislamu unashuhudia tofauti. Waislamu hivi leo sio tu wako mbali sana na kuwa ni viongozi wenye thamani katika jukwaa la kimataifa, bali hawawezi hata kutatua matatizo yao wenyewe na migogoro kwa mujibu wa kitambulisho cha Kiislamu. Kinyume chake, nchi zao zimetawaliwa na maadui wa Mwenyezi Mungu, utajiri wao unaporwa, majumba yao yanabomolewa, matukufu yao yananajisiwa, makumi ya mamilioni ya watu wanauliwa kikatili, wanafungwa katika makambi ya mateso au wakihangaika huku na kule wakiwa wakimbizi. Zaidi ya hayo, hivi leo kuwa Muislamu sio ufakhari na hata kulinganishwa na kosa la jinai, na Uislamu umetangazwa kuwa ni chanzo cha ugaidi na tishio kuu kwa walimwengu.

Sababu ya hili ni kuwa Waislamu wamedhoofika katika ufahamu wao wa Uislamu kuwa ni wenye kukusanya muongozo wote wa kimfumo. Wakati huo huo, maadui wao wamejikuza na kujiimarisha kupitia utekelezaji wa Mfumo wa Kirasilimali na utekelezaji wa nidhamu ya kidemokrasia unaotokana nao. Mataifa makuu ya kirasilimali ya Kimagharibi yamefanikiwa katika mashambulizi yao ya kielimu dhidi ya Waislamu, ambayo hatimaye yamehakikishia ushindi wao wa kijeshi na kisiasa dhidi ya Dola ya Kiislamu. Hatimaye, ni kuwa maeneo yote ya Kiislamu na masuala ya kimaisha ya Waislamu yameangukia chini ya utawala wa wasiojali Mungu, Wakoloni wa Kimagharibi na vibaraka wao.

Wakiwa wametia sumu akili za Waislamu kwa fikra za utaifa na uzalendo, makafiri wakoloni wameuvunja umoja wa Waislamu na kuwasukuma kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa maslahi yao ya ubinafsi. Waislamu wamejikuta wakifungika ndani ya dola bandia za kieneo, mipaka yake ikiwa imechorwa kulingana na maslahi ya mataifa makuu ya kirasilimali na kwa kiwango cha ushawishi wao juu ya medani ya kimataifa. Ummah wa Kiislamu umejikuta ukiwa chini ya watawala waovu waliowekwa na wakitegemea juu ya matakwa ya maadui zao, kipengee muhimu cha ajenda yake ya kisiasa ni kuwaondosha Waislamu kutokana na mwamko na maendeleo.

Matokeo ya Waislamu kutawaliwa na mfumo wa kirasilimali ni kuwa, Waislamu walinyimwa fursa ya kuongozwa kwa hukmu za Kisharia zinazotokana na Quran na Sunnah za Mtume (saw). Na suala halikuishia tu kwenye sheria za mfumo wa serikali na adhabu, lakini pia sera za ndani na nje, uchumi, elimu, afya, nk. Hata katika maisha yao ya kibinafsi, Waislamu walizuiliwa kuendesha mahusiano chini ya msingi wa Uislamu, ima uwe unahusiana na ndoa, mirathi, malezi ya watoto, na hata chakula au mavazi.

Ndani ya kiini cha mfumo wa kirasilimali, Ummah wa Kiislamu umepoteza sio tu rasilimali zake za asili na kiuchumi, ambazo zimetwaliwa na mashirika makubwa nyuma ya migongo ya mataifa ya Kimagharibi. Zikiwa zimejisalimisha chini ya miongozo inayoitwa “Sheria za Kimataifa”, ambazo zimekuwa ni vyombo vya ukoloni na kutiwa utumwani, Waislamu, licha ya kuwa na wingi mkubwa wa idadi ya watu, wamenyimwa haki ya kufuata mfumo wa kisiasa unaofaa kwa ajili yao. Licha ya ukweli kuwa wana mfumo mkamilifu na thaqafa ya hali ya juu ya Uislamu, Waislamu wamenyimwa haki ya kuwa na njia yao wenyewe ya maendeleo, ambayo inafichuwa ufisadi wa demokrasia ilio na misingi ya uongo ya “haki za binaadamu na uhuru”.

Kiburi na ujeuri za warasilimali zimefikia kiwango cha kuanza kuingilia kwa uwazi utukufu wa Quran na shakhsia ya Mtume Muhammad (saw). Wameanza kudai kuwa Waislamu waachane na sheria za misingi ya Uislamu, kama Imani na ukafiri, hukumu za Sharia, wajibu wa Jihad, nk. Zaidi ya hivyo, wametaka kwa Waislamu kuacha baadhi ya aya za Quran na Sunnah ili kuuweka Uislamu ambao umeteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) ulingane na kile kinachotengenezwa nao; uwe Uislamu wa Kifaransa, Kijerumani na Kiamerika”.

Utawala wa mfumo wa kirasilimali na demokrasia yake inawapelekea Waislamu sio tu kuhangaika, lakini pia wanaadamu wote, ukiwanyima matumaini mema katika kipindi hiki na cha baadaye. Mabara yote yametupwa kwenye kigezo cha nchi za “ulimwengu wa tatu”; zimenyimwa kila matarajio ya kuzifikia nchi za Magharibi kwa upande wa viwango vya maisha, ambapo maendeleo huhakikishwa kwa utajiri unaoibiwa kutoka kwa watu hawa na kazi za kitumwa. Hata ndani ya nchi kubwa zenyewe zilizo na nguvu za kirasilimali, muitikio wa jamii kwa mzozo wa nidhamu ya kiuchumi haukuishia kwenye maandamano, kama “kuzingira Wall Street” au “harakati ya vizibao vya manjano”. Wanafikra wengi na wanasiasa wameanza kutangaza upotovu na kuvunjika kusikoepukika kwa urasilimali. Achilia mbali juu ya kushindwa kwa demokrasia moja kwa moja katika utekelezaji wa kimaadili, kiroho na thamani ya kiutu.

Yote haya ni matokeo ya kukosekana kwa dola inayotekeleza Uislamu kama nidhamu ya kisiasa, inayotekeleza Jihad kuondoa vizuizi vya kuuleta Uislamu kwa walimwengu wote ukiwa kama mfumo, na kuihifadhi Itikadi kama Imani juu ya Mungu Mmoja. Huu ni utekelezaji kamili wa Uislamu, kwa mujibu wa Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Makhalifah Waongofu waliofuata baada yake, ambapo hatimaye Waislamu watarejea katika nafasi ya kuwa Ummah bora, ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewataka wawe. Ni Dola ya Kiislamu tu, inatakayo simamishwa na Waislamu kwa njia ya Mtume (saw), ndiyo itamaliza zama za uovu na uonevu na kuwaongoza walimwengu wote waondokane na kiza cha ujinga na mzunguko wa maafa kuelekea maendeleo na ustawi jumla.

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mustafa Abu Ibrahim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu