- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Miaka 100 Tangu Kuvunjwa kwa Khilafah: Unafanya Nini Kuirudisha?
Hali yako ikoje hivi sasa? Je unadhani kuwa hali yako ya sasa itabakia na kudumu kama ilivyo? Hali yako ya sasa inahusiana kwa njia ya moja kwa moja au la na nidhamu ya utawala iliyopo? Lau jibu la suali la mwisho ni Nndio ya kukata, basi, umeweka mipango gani ili kubadilisha hali ya mambo?
Masuali hayo lazima yawasumbue wale ambao wako makini na kuwepo kwao katika dunia hii ya muda mfupi. Watu makini huchunga muda wao unaoisha kila kukicha. Uamuzi wao hatimaye huwa ni kuchangamkia mradi ambao utatimiza lengo la kuwepo kwao dunia nalo ni kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) – Muumba wa ulimwengu, mwanadamu na uhai. Lengo hili litatimia kwa kujifunga na kutekeleza kwa upana nidhamu ya Mwenyezi Mungu ya Khilafah ambayo haipo leo.
Ulimwengu umepangika kinidhamu na vile vile maisha ya mwanadamu. Kufaulu na kufeli kwa mwanadamu kunahusiana na nidhamu ambayo amejifunga nayo maishani. Vile vile nidhamu hunasibishwa na hali ambayo mwanadamu anapitia. Ama kuhusiana na hali kubakia na kudumu au la hutegemea fikra zinazobebwa na mwanadamu juu ya nidhamu inayomtawala.
Nidhamu yenye nguvu sasa ni demokrasia duniani kote. Mataifa yenye nguvu kuanzia Amerika, Uchina, Urusi, Uingereza, Ufaransa n.k yote yamejifunga na demokrasia. Baadhi ya mataifa hudai kwamba sio ya kidemokrasia mfano falme za Saudi Arabia, Oman, Kuwait badala yake zina mipangilio fiche. Hata hivyo, dola zote duniani zimesimama juu ya nidhamu ambazo zinachipuza kutoka katika akili yenye kikomo ya mwanadamu!
Kwa kuwa akili ya mwanadamu ina kikomo basi kufikiria kwake ni kadhalika. Hivyo basi, mwanadamu humuhitaji Muumba ili kumpangilia na kumuongoza katika maisha yake yote. Na kujifunga na nidhamu zilizotungwa na wanadamu kama vile demokrasia ambayo inapigiwa debe duniani kuwa ndio suluhisho la matatizo ya wanadamu sio chochote bali ni kosa kubwa! Sio tu kuwa ni kosa, bali ndilo linalo sababisha majanga yasiyohesabika duniani kote hivi leo.
Mradi wa kidemokrasia umefeli wazi wazi! Waasisi na wapigiaji debe wa nidhamu ya utawala ya kidemokrasia wamekata tamaa na wanatafuta sehemu ya kuificha miito na misemo yao hadaifu. Wameipigia debe demokrasia kwa kutumia mtutu wa bunduki kwa wale walioikataa. Kwa upande mwingine, wamewaghilibu waliokata tamaa kwa vijipesa ili waweze kujifunga na nidhamu iliyojaa kashfa na yenye kutamausha.
Hatimaye kufeli huko kumefichuka na sauti za upinzani zinaendelea kunawiri. Kwa kutaja mifano michache: ndani ya Amerika nidhamu hii ndiyo chanzo cha kuwagawanya Waamerika katika mirengo ya rangi na kiuchumi. Wengi wamepoteza matumaini na nidhamu iliyoko na wanalingania kupatikane mbadala. Wamethibitisha kukata tamaa kwao kwa kuvamia jengo la Capitol Hill, ambalo ndio ishara ya kuwa Amerika ndio kinara na ngome ya demokrasia duniani.
Nchini Uingereza wengi wa watu walipiga kura kujiondoa katika Muungano wa Ulaya, wakitumaini mustakbali wenye ufanisi baada ya kuhisi kukandamizwa hapo awali kwa kuwepo kwao katika Muungano huo. Badala yake kunatarajiwa kuweko na hali mbaya Zaidi kwa kuzingatia hali ya kujitenga kwa Uingereza kama kisiwa. Licha ya Uingereza kuwa na haiba ya kuwa ukoloni, nidhamu iliyojifunga nayo ipo kuwalinda ‘mabwana’ na kuwakandamiza ‘watumwa.’
Ndani ya Ufaransa, watu waliandamana kwa nembo ya ‘Harakati ya Vesti ya Njano’ dhidi ya sera za kiuchumu ambazo zinalenga kuzidi kukazanisha vitanzi shingoni mwao! Serikali ya Ufaransa inaendelea kubuni sheria ambazo zina wakandamiza na kuwajasusi raia wao kwa misingi ya kidini na kiuchumi hadi sasa. Yote hayo kwa jina la kulinda nidhamu ya kisekula ya kijamhuri!
Nchini Uchina, chama cha kikomunisti kiko katika michakato ya kuhakikisha kwamba sauti zozote za upinzani zinasitishwa mara moja. Kuwaua na kuwatishia raia wake ndio sera nambari moja katika vipaumbele vyake. Imo katika mchoro mpana na wa kikatili wa kuyasafisha mabongo ya raia wake katika eneo la Xinjiang ili kuwalazimisha kujifunga na imani ya kikomunisti.
Ndani ya Mashariki ya Kati na Afrika kwa ujumla uharibifu ni mkubwa na makovu yameshindwa kupona. Mabwana wakoloni wanaendelea kuwaunga mkono watawala wao vibaraka dhidi ya watu wenyeji. Utajiri unafujwa na kutengewa makampuni machache ya Kimagharibi. Wengi wanatupwa ndani ya umasikini na kudumu katika miradi ya utafutaji tonge.
Orodha ya mifano ni ndefu na imejaa uovu wa sera, sheria na kanuni. Zinazotungwa na tawala za kisekula duniani kote ili kuendesha dola zao zenye kikomo kimipaka. Dola za kitaifa ambazo zinataabika kutokana na madeni, mfumko wa bei, watu waliokata tamaa, miundo mbinu isiyohimili, wasomi na wajuzi waliochanganyikiwa n.k. wakiwa njia panda!
Aliye makini lazima asijiwekee mipaka tu kufikiria ndani ya sanduku la kisekula la kidemokrasia. Badala yake lazima ajitume kuyafuta aliyo yasoma zamani na kujielekeza kwa yaliyo nje ya sanduku la nidhamu ya kidemokrasia. Huo ni mradi adhimu ambao hautakiwi kuwa wa kubahatisha na patapotea. Kwa maana nyingine, lau uko makini, basi unatakiwa kujiepusha na michakato ya kubahatisha kwani inadhamini kufeli kiuhakika mwishoni.
Kufaulu kunaweza kupatikana kwa kurudia lengo kuu la kuwepo kwetu duniani. Mwenyezi Mungu (swt) asema: وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.”(Adh-Dhariyat: 56). Ni muhimu kwa watu wenye kufikiria kunyanyuka juu ya sanduku la kisekula la kidemokrasia na kutafuta suluhisho la kudumu na la kimsingi kwa matatizo yanayo wakumba wanadamu leo duniani.
Hatimaye, mtu mwenye kutafakari lazima ajitwike jukumu la kufanya utafiti utakaomplekea kujiunga na kushirikiana na chama pekee cha Kiislamu cha Hizb ut Tahrir. Chama cha kisiasa ambacho kinawaleta pamoja wanaume na wanawake walio makini katika kuwakomboa wanadamu kutoka katika minyororo ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zenye sumu zikiongozwa na demokrasia. Chama kilicho makini ambacho hakiwajali wanaolaumu au kuwaotesha vidole katika jukumu lake adhimu. Chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu na ndio gundu inayowaunganisha wanachama wake.
Hizb ut Tahrir inafanya kazi usiku na mchana kurudisha maisha ya Kiislamu kupitia kurudisha Khilafah kwa njia ya Utume. Kipaumbele cha Hizb ut Tahrir ni ulinganizi wa Khilafah na sio jingine. Hivyo basi, mtu yeyote makini aliye na hamu ya mabadiliko lazima asipoteze muda wake muhimu na mfupi katika kazi ya kuziba viraka. Badala yake afanye haraka kuitikia ulinganizi wa Mradi wa Khilafah ambao umeshamiri duniani kote. Kusimamisha Khilafah ndiko kutakako dhamini amani, utulivu na ufanisi kwa Ummah. وَيَوۡمَٮِٕذٍ۬ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ “Na siku hiyo Waumini watafurahi.” (Ar-Rum: 4)
#أقيموا_الخلافة #خلافت_کو_قائم_کرو
#ReturnTheKhilafah #YenidenHilafet #TurudisheniKhilafah
Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir