Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 1 Jumada I 1444 | Na: 1444/09 |
M. Ijumaa, 25 Novemba 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Rais Yatoa Kafara Mpya kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumatano, Novemba 23, serikali ya Tunisia ilitangaza, katika taarifa ya pamoja kwa Wizara ya Viwanda, Nishati na Madini, na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Biashara ya Nje, ongezeko la bei za baadhi ya mafuta, kuanzia Alhamisi, 24/11/ 2022 saa sita usiku, kama ifuatavyo:
Petroli isiyo na madini na risasi (lead): millimes 2525 (za dinari ya Tunisia) kwa lita
Gasolini isiyo na sulfur: millimes 2205 kwa lita
Petroli aina ya Regular: millimes 1985 kwa lita
Petroli aina ya Premium unleaded: millimes 2855 kwa lita
Gasolini isiyo na Premium sulfur: millimes 2550 kwa lita
Ongezeko hili la bei ya mafuta ni la tano mwaka huu, kwani ongezeko la kwanza lilikuwa mnamo Februari, la pili Machi, la tatu Aprili na la nne Septemba, na kufanya jumla ya mwaka huu kupanda kwa bei ya mafuta kufikia takriban asilimia 20.
Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, mbele ya dhulma hii waliyofanyiwa watu wa Tunisia, tunaangazia yafuatayo:
1- Bila shaka, kazi ya watawala hawa, kwa kuzingatia hali ya kiutendaji iliyopo katika nchi yetu, ni kutii maagizo ya Mfuko wa Fedha la Kimataifa (IMF). Maagizo haya ni pamoja na kuondoa ruzuku kwa bidhaa, kuunganisha kiwango cha sarafu na thamani ya dolari, na kupunguza matumizi ya serikali, ambayo ina maana kwamba serikali haitumii katika kushughulikia mambo ya watu katika elimu, afya na mengineyo.
2- Ongezeko hili litapelekea kupanda kwa gharama za usafiri, na hivyo kupanda kwa bei na bei kubwa kwa watu kwa kuzingatia viwango vya juu vya umaskini na ukosefu wa ajira na kwa kuzingatia mishahara midogo isiyokidhi bei ya kujikimu kwa lazima, bila kusahau nyumba, mavazi, matibabu na elimu, na itawashughulisha watu kutafuta riziki!!
3- Serikali ya rais ni serikali iliyofeli na isiyo na uwezo wa kusimamia mambo ya nchi na watu. Hamu yake kubwa ni kutekeleza maagizo ya wakoloni wa Magharibi na taasisi zake za fedha, na kutoa mali ya nchi na maslahi ya wananchi kama kafar na mahari kwa IMF, na hivyo kuomba kuendelea kukaa katika kiti cha serikali, chenye maguu mabovu!!
4- Sababu ya kufeli kwa serikali hii ni; upotezaji wake wa dira na utekelezaji wake wa mfumo wa kodi, mfumo wa kibepari, na kurudia masuluhisho yale yale yanayoleta ugumu na taabu, na kuachana kwake na mfumo wa uchungaji, mfumo wa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amemtisha mwenye kutekeleza kitendo hiki kwa kusema:
(وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى) “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 124].
5- Sera hii ni sera ya dhulma, ufukara, njaa na uchovu wa watu, na sababu yake ni ufisadi wa watawala na ufisadi wa mfumo wa kibepari ambao watawala wanautawalisha. Tawala zinazotabikishwa katika nchi yetu na katika nchi nyingine za Kiislamu ni mifumo ya kisekula ya kibepari inayotenganisha dini na dola. Ni mifumo iliyotungwa na wanadamu kulingana na matakwa na matamanio yao, na kwa hivyo bila shaka itasababisha taabu na unyimaji. Tunawakumbusha watawala yale aliyoyasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):
«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ» “Ewe Mwenyezi Mungu, yeyote anayetawalishwa chochote katika mambo ya Umma wangu akawadhikisha, basi na wewe mdhikishe.” [Imepokewa na Muslim]
Kutokana na haya, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia:
Tunalaani vikali mpango wa serikali hii iliyofeli, ambayo iko kwenye njia ya kuiweka rehani na kuiuza nchi hii, ambao ulifanywa na serikali zilizopita. Hii ni kwa sababu mpango huu pamoja na kuupa nguvu ukoloni na zana zake za kifedha katika nchi yetu, unazidi kuwadhalilisha watu wa Tunisia na kuwanyima mali zao za asili kwa manufaa ya makampuni ya kigeni yanayopora mali yao.
Tunaelekeza nasaha zetu kwa watu wetu wa Tunisia: kwamba suluhisho la dhiki tuliyomo ndani yake, ya maishi na utegemezi wa kuchukiza wa makafiri na wakoloni wa Magharibi ambayo inajulikana na sio kuwa haijulikani, ni kukataliwa kwa itikadi ya kibepari na mfumo wake wa kiuchumi na kifedha, na kukataa kuitikia mashinikizo ya kimataifa na taasisi zake za kifedha, haswa IMF, na kukataa misaada ya kimataifa na mikopo kutoka kwa benki zake. Badala yake, kuchangamsha mradi wa hadhara ya Kiislamu ili kuona maisha mapya, salama na amani yaliyo huru kutokana na migogoro ya kiuchumi na kifedha, kwa kuzingatia uadilifu wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu.
Uislamu umeasisi mfumo wa kiwahyi unaozuia tabaka lolote katika jamii kuwadhibiti watu wengine wote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
(فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى)
“...Basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika * Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 123-124].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |