Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  20 Rabi' II 1446 Na: HTS 1446 / 16
M.  Jumatano, 23 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kukamatwa kwa Ndugu yetu Al-Munawar Hakutabadili Uhalisia wa Vita vya Kipuuzi nchini Sudan
(Imetafsiriwa)

Jana asubuhi, Jumanne, tarehe 19 Rabi` al-Akhir 1446 H sawia na 22/10/2024 M, chombo cha usalama kilimkamata Ndugu Al-Munawar Dafallah Mustafa, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, kutoka nyumbani kwake katika mtaa wa Al-Sharif Al-Aqab katika mji wa Al-Qadharif, kwa misingi ya majadiliano katika kundi la WhatsApp, ambapo Ndugu Munawar alieleza uhalisia wa vita vinavyoendelea nchini Sudan, kwamba ni mzozo kati ya nguzo mbili za ukoloni; Amerika na Uingereza, na kwamba viongozi wa jeshi na viongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka wote ni vibaraka wa Amerika, huku Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko na harakati za kile kinachoitwa mapambano ya silaha ni vibaraka wa Uingereza. Ukweli huu haukumfurahisha mmoja wa wanakikundi, na inaonekana kana kwamba kyeye ni mmoja wa majasusi wa serikali, hivyo akamtishia Ndugu Munawar kupitia rekodi ya sauti, na Munawar alipokosa kujibu tishio hilo, walimkamata wakidhani kwamba wakifanya hivyo wangeweza kunyamazisha sauti ya ukweli. Walivunjika moyo na kupotea!

Tabia hii ya wapambe wa utawala huu inathibitisha kwamba utawala huu ambao ni upanuzi wa mifumo ya dhulma na ukandamizaji, haujajifunza kutoka kwa watangulizi wake ambao walifanya dhulma, kuwakamata na kuwatesa wabebaji da’wah wanachama wa Hizb ut Tahrir. Hili lilizidisha tu imani yao juu ya haki wanayoitangaza, na kuwadhihirishia ubaraka wa watawala hawa kwa Mkoloni Kafiri Magharibi, na kubainisha haja ya Ummah kukombolewa kutoka kwa ukoloni, ambao unaweza kupatikana tu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume; njia halali ya kutekeleza mafundisho ya Uislamu na kuyabeba ulimwenguni. Hizb ut Tahrir na wanachama wake watabakia kuwa imara kama milima mbele ya mkoloni na zana zake za ndani kama vibaraka, wapotoshaji na watu waliodanganyika. Kesho, Mwenyezi Mungu akipenda, guo litainuliwa na pazia itaondolewa, na watu wataona ukweli waziwazi mithili ya jua la mchana. Hapo watajua kwamba lau wangejua ukweli wa yale yanayopangwa dhidi yao, wasingelibakia katika udhalilifu huo!

Wanachama wa Hizb ut Tahrir wataendelea kutangaza haki mpaka muregee kwenye fahamu zenu na mutubu kwa Mwenyezi Mungu, au yale yaliyowapata madhalimu katika zama zote yakupateni.

Alichokifanya ndugu yetu Al-Munawar, Mwenyezi Mungu amlipe malipo mema na amuondoe kifungoni, ni miongoni mwa amali njema kabisa. Ni kitendo cha Manabii na Mitume, wabebaji wa ulinganizi wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na mumwachilieni huru Al-Munawar mara moja, wala musiwe miongoni mwa wanaozuilia Njia ya Mwenyezi Mungu kwa kujitahidi kuifanya ionekane potofu! Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجاً أُوْلَـئِكَ فِي ضَلاَلٍ بَعِيدٍ]

“Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wamepotelea mbali.” [Ibrahim: 3]

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemamji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu