Iwe ni Suala la Mafuriko au Kashmir, Suala la Uchumi au Kukaliwa Kimabavu kwa Mito Yetu na Dola ya Kibaniani —Je, Tutaendelea Kungoja ‘Jumuiya ya Kimataifa’ Mpaka Lini Kutatua Matatizo Yetu?
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya mafuriko makubwa katika majimbo ya kaskazini ya Khyber Pakhtunkhwa, hasa katika Buner na maeneo ya karibu, ambapo mamia ya watu walipoteza maisha na nyumba, mifugo, mali na magari kusombwa na maji, mafuriko mapya sasa yanapitia Punjab na baadaye yataelekea Sindh. Hapo awali, Karachi pia ilikumbwa na mvua kubwa. Tunamuombea Mwenyezi Mungu Mtukufu usalama na kheri, kwani pamoja na utabiri zaidi wa mvua, watawala wetu wameinua mikono juu tu na kuliacha suala zima kwa rehema ya jumuiya ya kimataifa. Wanaendelea kuwasilisha suala hili zima kwa namna ambayo ni kana kwamba haya ni mabadiliko ya tabianchi ambayo hayawezi kudhibitiwa kabisa na wao, na ikiwa ‘jumuiya ya kimataifa’ haitaingilia kati, wataachwa bila msaada kabisa – kana kwamba ulinzi wa maisha na mali ya watu wao sio jukumu lao bali ni la mfumo wa kimataifa!