Alhamisi, 20 Safar 1447 | 2025/08/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  19 Safar 1447 Na: 04 / 1447
M.  Jumatano, 13 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

“Siku ya Uhuru” ya 78
Pakistan Itakuwa Huru Kupitia Kuanzishwa kwa Khilafah Rashida

(Imetafsiriwa)

Chini ya mfumo wa sasa wa kimataifa, kile kinachoitwa uhuru si kitu zaidi ya usanii wa mchezo wa kuigiza, kwan maana ukombozi wa kweli (tahrir) uko pale tu dola inapoweza kupanga mambo yake ya ndani na mahusiano ya nje kwa mujibu wa itikadi yake. Watu wanaoamini “La ilaha illa Allah Muhammadur RasulAllah” kamwe hawatakombolewa kikweli mpaka watabikishe katika ardhi yao mfumo wa Kiislamu wa utawala, uchumi, jamii, elimu, na mahakama, pamoja na sera ya kigeni yenye msingi wa Da‘wah na Jihad. Hii ndiyo maana halisi ya uhuru, na katika suala hili, Pakistan bado haijakombolewa!

Ukitupia macho sera muhimu za Pakistan inatosha kuthibitisha jambo hilo. Je, sera ya Pakistan kuhusu Al-Quds na Gaza haijatungwa katika CENTCOM ya Marekani, Pentagon, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani? Je, sera ya Kashmir haijajengwa juu ya kuomba umakini wa Trump, licha ya ukweli kwamba miezi michache iliyopita tulionyesha kwa vitendo uwezo wa kuikomboa moja kwa moja? Je, sera ya Pakistan kwa Afghanistan imeundwa na Afisi yetu ya Mambo ya Nje, au imetungwa na Wasaidizi wa Mawaziri na makamanda wa kijeshi wa CENTCOM ya Marekani? Je, Pakistan haitungi bajeti yake, sera ya fedha, na sera ya uchumi chini ya uangalizi mkali na maagizo ya IMF? Je, Mawaziri Wakuu hawatamki bila aibu kwamba wataomba kibali cha IMF kupunguza bei ya umeme? Je, mahakama za Pakistan bado haziamua kesi kwa misingi ya sheria za kawaida za Kiingereza? Je, mkuu wa jeshi la Pakistan hakusafiri hivi majuzi hadi Marekani ili tu kuhudhuria sherehe ya kustaafu ya “afisa wake mkuu” wa moja kwa moja, Jenerali Kurilla? Ni aina gani hii ya “uhuru”, ambapo hatuwezi kupigana vita kwa ajili ya Kashmir au Gaza lakini tuko tayari kupigana katika vita vya Amerika?

Pakistan ni mojawapo ya dola saba zilizotangazwa kuwa na nguvu za nyuklia duniani. Dola tano kati ya hizi zenye nguvu za nyuklia zinadhibiti maeneo tofauti ya ulimwengu na kuunda mambo kulingana na maslahi yao ya kimfumo. Ufaransa na Uingereza zinadhibiti siasa za Ulaya; Amerika inalazimisha maagizo yake kote ulimwenguni; Urusi imejikita katika Ulaya ya Mashariki; China inazidi kupanua wigo wake wa ushawishi. Ama kuhusu dola ya Kibaniani, inafanya kazi kwa bidii ili kuwa polisi wa kanda hii. Kwa hivyo Pakistan inasimama wapi katika mlingano huu? Marekani inaweza kufanya, kuvunja, na kufanya upya mkataba wa nyuklia na Iran kwa hiari yake, lakini hatuwezi hata kuhitimisha makubaliano ya ununuzi wa mafuta na Iran. Kwa nini? Huu ni uhuru wa aina gani?

Enyi Maafisa na Wanajeshi wa Jeshi la Pakistan!

Kikwazo cha uhuru na ukombozi (tahrir) wa kweli wa Pakistan sio ukosefu wa rasilimali wala uhaba wa shauku, ujasiri, au uwezo miongoni mwa askari wetu au watu wetu. Mgogoro wetu halisi ni uongozi usio na dira—uongozi ambao lazima uondolewe na ubadilishwe kwa uongozi wa kimfumo ambao kwao Ba’yah ya Nusra (msaada wa kijeshi) inatolewa, ili Khilafah Rashida iweze kusimamishwa nchini Pakistan. Huu ndio ufafanuzi sahihi wa uhuru wa kweli, na jukumu kubwa zaidi la kuufikia liko juu yenu, kuiongoza Pakistan kufikia lengo hili. Hizb ut Tahrir, Chama cha Ukombozi, kinasimama mbele yenu kikiwa na ruwaza ya kimfumo, kinawasilisha kwenu mpango na mradi kamili. Kwa hiyo jitokezeni, katika “Siku ya Uhuru” hii ya 78, muivishe vazi la uhuru wa kweli, kataeni mfumo huu wa kimataifa wa kikoloni, na chini ya bendera ya Raya ya “La ilaha illa Allah Muhammadur RasulAllah,” jenga mfumo mpya wa dunia.

[وَأَنَّ هَٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ]

“Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” [Surah Al-An‘am 6:153]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu