Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 9 Jumada I 1443 | Na: H.T.L 1443 / 03 |
M. Jumatatu, 13 Disemba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Matukio ya Kutisha katika Kambi ya Wakimbizi wa Kipalestina ya Burj al-Shamali Kusini mwa Lebanon
(Imetafsiriwa)
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema kama ilivyosimuliwa na Abu Dawud katika Sunan yake kwa silsila ya riwaya iliyo Sahih:
«إنَّ السعيدَ لَمَنْ جُنِّبَ الفِتَنَ، إنَّ السعيدَ لَمَنْ جُنِّبَ الفِتَنَ، إنَّ السعيدَ لَمَنْ جُنِّبَ الفِتَنَ، ولَمَن ابتُلِيَ فصَبَر؛ فَوَاهاً»
“Mtu mwenye furaha ni yule ajiepushae na fitna, Mtu mwenye furaha ni yule ajiepushae na fitna, Mtu mwenye furaha ni yule ajiepushae na fitna mwenye kupewa mtihani akasubiri.” “ni uzuri ulioje” ikimaanisha: Ni kheri ilioje kwa mwenye kusubiri.
Kwa mtazamo huu, kwa mtazamo wa dini yetu inayotuongoza, na baada ya matukio uchungu mfululizo katika Kambi ya Burj al-Shamali - mlipuko na kisha ufyatualiaji risasi kwenye mazishi! - ambayo yaligharimu maisha ya watu wasio na hatia, ili kwamba badala ya mazishi moja, mazishi mengi yalifanyika katika kambi zaidi ya moja, wahasiriwa ambao walikuwa ni vijana wadogo katikati ya ujana wao, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon tunatoa wito kwa kila mtu kuepuka fitna. na kuwa na subira.
Ni kana kwamba watu wa Palestina nchini Lebanon hawahitaji kitu chengine chochote isipokuwa kupigana wenyewe kwa wenyewe! Haswa kwa kuongezeka kwa majanga haya ambayo hayahitaji kutajwa na kufafanuliwa, katika ngazi zote za kisiasa, kijamii, afya na maisha, ambayo watu wa Palestina wanaishi chini ya hali zilezile nchini Lebanon kama watu wa Lebanon wenyewe.
Ingawa ni muhimu kuchukua msimamo mkali dhidi ya udhihirisho wa silaha wa kipuuzi na wa kupita kiasi katika kila raha na furaha, lakini sasa tunatoa wito kwa maafisa ambao wamejiweka kama viongozi wa watu wa Palestina nchini Lebanon kukusanyika ili kuzuia dhiki, kuepusha kauli za kichochezi za aina yoyote ile, na kutaka kuitishwe mikutano ya dharura ili kuzuia tukio hilo kutumiwa vibaya dhidi ya watu wa Palestina nchini Lebanon, haswa kutokana na wimbi la uchochezi wa kibaguzi dhidi ya haki zao za binadamu.
Vile vile tunatahadharisha dhidi ya kufikisha maneno ya fitna, na kuacha udadisi wa kuizungumzia haswa kwenye mitandao ya kijamii ambayo mingi yake imekuwa mimbari za uchochezi, tukikumbuka maneno ya Mtume wetu Muhammad (saw) kama Imam Muslim alivyosimulia katika Sahih yake:
«كَفَى بالمَرْءِ كَذِباً أَنْ يُحَدِّثَ بِكُلِّ مَا سَمِعَ»
“Inatosha mtu kuwa ni mrongo kwa kuzungumza kila anachokisikia.” Maana yake ni kuwa mtu bila kuepukika anasikia maneno machafu - haswa katika matukio kama hayo - na ikiwa atasimulia basi atakuwa ametenda kitendo kilichoharamishwa.
Kipaumbele cha leo ni kuepuka fitna, kuwa na subira kwa waliojeruhiwa, kusimama pamoja na waliojeruhiwa, na kutanguliza mantiki ya Sharia na hekima ya wenye hekima. Ikiwa sio katika majeruhi kama haya, basi lini?!
Mpaka ukweli ubainike kutokana na uongo, kanuni msingi ni kushikamana na yale aliyotuwajibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) wakati wa mitihani, kama ilivyosimuliwa na Imam al-Bukhari katika Sahih yake.
«سَتَكُونُ فِتَنٌ القاعِدُ فيها خَيْرٌ مِنَ القائِمِ، والقائِمُ فيها خَيْرٌ مِنَ الماشِي، والماشِي فيها خَيْرٌ مِنَ السَّاعِي، ومَن يُشْرِفْ لها تَسْتَشْرِفْهُ، ومَن وجَدَ مَلْجَأً أوْ مَعاذاً فَلْيَعُذْ بهِ»
“Kutakuweko na fitna (na wakati huo) mtu aliyekaa atakuwa bora kuliko aliyesimama, na aliyesimama atakuwa bora kuliko anayetembea na anayetembea atakuwa bora kuliko anayekimbia. Na yeyote mwenye kusimamia fitna hizi zitamsweka, na yeyote atakayepata ulinzi au uepushi basi naajiepushe nao.”
Rambirambi zetu kwa familia zetu, na dua zetu kwa ndugu zetu waliojeruhiwa wapone haraka, na kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kumuandikia kila mtu malipo ya wale waliojeruhiwa na malipo ya subira, dua kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, rehema na uongofu;
[وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ * أُوْلَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ]
“…Na wabashirie wanao subiri, * Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea * Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.” [Surah Al-Baqarah: 155-157].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: |