Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  2 Jumada II 1443 Na: H.T.L 1443 / 04
M.  Jumatano, 05 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

            Katika Bazaar ya Uchaguzi wa Wabunge

Malumbano ya Kisiasa na Kuipeleka Nchi Katika Hali ya Kudorora

(Imetafsiriwa)

Huku kuanguka kwa lira kukigusa ukingo wa lira elfu thelathini kwa dolari moja, na kwa bei ya juu ya kutisha katika nyanja zote za maisha, kuanguka kwa uwezo wa ununuzi wa lira hadi kikomo cha asilimia 95 ya thamani yake, na mishahara ya watumishi iliyopungua hata chini ya kujikimu, wanasiasa watawala katika nchi hii wanatujia, ili kuwafanya watu wasikie sauti zao za mifarakano katika kulalamika juu ya madaraka, kurushiana tuhuma, kukwepa majukumu, na kutishia kuvunja makubaliano au kujiuzulu; kana kwamba watu wana pendelea kuwasikiliza, au kutafakari maneno yao.

Watu wamekuwa baina ya matajiri na matajiri kutoka katika tabaka lenu au wale wanaokufuateni au wanaotembea njia yenu, na masikini wasioweza kupata chakula cha siku yao, hivyo kuona uchungu wa watafutaji kwenye madebe ya taka ikiwa ni suala linalojirudia mara kwa mara linaloshuhudiwa kila kona. Pengine - kwa mara ya kwanza nchini Lebanon - tabaka la wastani linakaribia kutoweka! Yote haya ni katika wakati wa enzi yenu ya giza, ufisadi wenu uliokithiri, uchu wenu wa madaraka, na hata kutawala juu ya shingo za watu.

Na tunatambua kwamba mmoja wenu kuruka kutoka kwenye mashua ya mwenzake, au kumtukana mshirika wake, au kurushiana maneno, au hata muungano wa wale mnaoonekana kupingana kati yenu, si jambo geni nchini Lebanon, na kwa kawaida sio zaidi ya jambo moja au mambo yote mawili:

Maagizo yamekuja kutoka kwa bwana wenu Amerika kwamba kinachofaa kwa hatua hii ni kutengwa kwa chama au vyama, kuinua chama au vyama, au kuunda au kuvunja miungano, kwa sasabu za kikanda au kimataifa na bwana wenu, ambaye anajenga juu ya vichwa vyenu ubalozi wa pili kwa ukubwa katika kanda hii, ingawa jengo dogo linatosha kukusimamieni! Lakini ni mali iliyofichwa chini ya mwambao wetu ambayo bwana wenu anafanya bidii yake yote kuipora yeye mwenyewe moja kwa moja, na sio tu kukuteueni pekee kuipora kama ilivyokuwa hapo awali.

Au ni mvutano ambao nyinyi nyote mnauhitaji miongoni mwa raia wenu kuelekea uchaguzi mkuu wa Mei 2022, uchaguzi ambao miko ya kisiasa inakiukwa, miungano inaundwa upya, hata kwa muda tu, na nyuso zinabadilika, lakini nyoyo hazibadiliki, kwa kimaudhui nyinyi muna mtazamo sawa wa nchi na watu wake. Shamba litakalokupeni uporaji na wizi wa rasilimali za nchi, hata kama wananchi ni masikini au wenye njaa!

Lakini sote tunajua hila zenu na uovu wa kisiasa, ambao ni kuimarisha mabwana zenu katika Ikulu ya White House, au hata kidogo ya hilo katika ubalozi wa Amerika, na uimarishaji wa madhehebu na mishipa ya madhehebu kwenye ukingo wa uchaguzi.

Enyi Watu wa Lebanon:

Wakati umewadia wa kutangaza kwa sauti kuu kuondolewa kwa tabaka hili na kulikataa bila ya kusaza, na kufanya kile wanachojaribu kufanya kwenye milango ya uchaguzi kuwa kofi nyusoni mwao; na kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha Dola ya Uadilifu na Uongofu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo kwayo kila mtu anayeishi chini ya udhibiti wake na kubeba uraia wake atapata haki zote, bila kujali dini, dhehebu na rangi, na - angalau - kila mtu ndani yake atahisi usalama wa familia na atakuwa na afya njema; na kuwa na riziki ya siku yake, kabla haijafika siku ambapo mtakuwa pamoja na wanasiasa hawa, kama alivyosema Mola wetu Mtukufu:

(وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا)

“Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.” [Al-Ahzab: 67]. Na hali yao itakuwa kwenu nyinyi, kama Mola wetu Mtukufu alivyosema:

 (إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا)

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata.” [Al-Baqarah: 166].

(هَذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ)

“Hii ni bayana kwa watu wote, na ni uwongofu, na mawaidha kwa wachamngu.” [Aali-Imran: 138]

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu