Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 26 Rabi' II 1443 | Na: H.T.L 1443 / 02 |
M. Jumatano, 01 Disemba 2021 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
(مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23].
(Imetafsiriwa)
Kwa nyoyo zilojaa imani na kuridhika na qadhaa ya Mwenyezi Mungu, na kwa macho yanayobubujika machozi, Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon yamuomboleza mbebaji ulinganizi:
Al-Hajj Salih Turki Al-Hasan (Abu Abdullah)
aliyefariki mnamo mkesha wa kuamkia Jumatano 26 Rabi’ Al-Akhir 1443 H sawia na Disemba 1, 2021 M akiwa na umri wa miaka 79. Aliutumia umri wake mwingi katika kubeba da'wah ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, na akafa katika njia hiyo.
Al-Hajj Abu Abdullah, licha ya uzee na ugonjwa wake, hakusita hata kidogo kubeba da’wah, akienda sambamba na kasi ya vijana katika harakati na shughuli, na hata kukimbia nao mbio. Alishiriki katika kila amali ya da'wah, hata kama ingekuwa mbali sana, angekasirika Mashababu iwapo angekosa moja ya maswala ya ubebaji da'wah, na angewalaumu Mashababu endapo wangemsababishia kukosa fursa kwa kisingizio cha kuwa mzee!
Kambi ya Ain Al-Hilweh iliyoko kusini mwa Sidon ilimfahamu kama mtetezi wa da'wah, muwazi na mwenye msimamo mkali, akiwashauri ndugu zake, mwanamaoni wa kisiasa na da'wah, ambaye hakukosa mojawapo ya majukumu ya kijamii, na jicho lake juu ya Khilafah akiwa na yakini kamili kwamba ndiyo itakayoikomboa nchi hii na watu kutokana na uchafu wa kukaliwa na watawala.
Mwenyezi Mungu amrehemu Hajj Abu Abdullah na amruzuku mabustani mapana, na tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwingi wa Rehema, Mwingi wa Ukarimu, ampanulie muingio wake na amjaaliye makaazi yenye baraka, na amruzu rehema zake pana amali njema, na kumwandika miongoni mwa wale ambao dhambi lao la kutofanya kazi ya kuhukumu Shariah ya Mwenyezi Mungu katika ardhi yake na miongoni mwa waja wake limeondolewa.
Nyoyo zinahuzunika, na macho yanabubujika machozi, na tumehuzunishwa na kutengana nawe, na hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu pekee:
(إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ) “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.”
[Al-Baqara: 155-156].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: |