Jumapili, 12 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  19 Safar 1446 Na: 1446 / 02
M.  Jumamosi, 24 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mgogoro wa Nishati nchini Jordan na Suala la Ufisadi wa Kiuchumi wa Mradi wa Al-Attarat, Utiifu wa Kisiasa, na Kuongezeka kwa Deni
(Imetafsiriwa)

Ripoti ya habari ya Shirika la Habari la Jordan, Petra, ya tarehe 6 Agosti 2024, ilisema kwamba “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi iliamua kwamba serikali wala Kampuni ya Kitaifa ya Umeme hazihitajiki kulipa sehemu yoyote ya gharama kwa Kampuni ya Umeme ya Al-Attarat.” Habari hizi za upotoshaji zinakusudiwa kuficha hasara inayotarajiwa ambayo serikali ya Jordan itaipata kutokana na ukweli wa hukumu hiyo, inayosema: “Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi inaamuru kwamba mkataba huo ni halali na hauhusishi ukosefu mkubwa wa haki.” Kwa maana nyengine, serikali ilishindwa katika kesi ya usuluhishi wa kimataifa iliyodumu kwa miaka minne na kulazimika kufidia gharama za kufungua kesi hiyo inayokadiriwa kufikia dinari milioni nane licha ya uthibitisho wa awali kwamba ingepoteza kesi ya usuluhishi kabla ya kuwasilishwa mnamo 2020!

Kwa kuzingatia ulaghai huu wa vyombo vya habari, unaoambatana na ufichuaji wa ufisadi wa utawala huo kwa kuficha na kupotosha ukweli badala ya kusimama kidete na masuala ya taifa kwa kufichua ukweli na ufisadi unaolizunguka, na kuwasilisha ukweli sahihi kwa wananchi ili waweze kuchukua misimamo makini na yenye taarifa juu ya michezo ya utawala nchini Jordan na serikali zake, udanganyifu huu unalazimu uchunguzi wa tatizo la nishati nchini Jordan, hasa Mradi wa Al-Attarat na nini kiko nyuma yake:

- Wizara ya Nishati na Rasilimali za Madini hivi majuzi ilionyesha kuwa Jordan ina zaidi ya tani bilioni 116 za mafuta ya shale, ambayo iko ndani ya zaidi ya 60% ya ardhi ya Jordan. Kiwango cha wastani cha mafuta ya shale ya Jordan ni 10.5%, na shale ya mafuta inaweza kutumika kuzalisha mafuta na kuzalisha nishati, hasa umeme.

- Mkakati wa kina wa wizara kwa sekta ya nishati kwa miaka 2020-2030 unasema kuwa mchango wa shale ya mafuta katika uzalishaji wa umeme utafikia 15% ifikapo 2030, pamoja na gesi asilia na nishati mbadala kama vyanzo vya nishati.

- Makubaliano na Kampuni ya Al-Attarat Power yalifanywa wakati wa serikali ya Abdullah Ensour mnamo Oktoba 2014. Ni muungano wa makampuni kutoka China, Malaysia, na Estonia, yenye umiliki wa 45% kwa China na Malaysia na 10% kwa Estonia. Mradi huo unalenga kuzalisha nishati ya umeme kutokana na shale ya mafuta katika eneo la Al-Attarat Um Al-Ghudran na kuiuza kwa Kampuni ya Kitaifa ya Umeme. Inatarajiwa kutoa 15% ya mahitaji ya umeme ya kila mwaka ya Ufalme huu kwa miaka 30, na gharama ya uwekezaji ya $ 2.1 bilioni, ambayo nyingi yake, $ 1.6 bilioni, zilifadhiliwa na benki za China. Mapema Julai 2023, Kituo cha Umeme cha Al-Attarat kilizinduliwa, kikifanya kazi kwa uwezo kamili wa megawati 470.

- Mradi huu ulikadiriwa kuimarisha kiwango cha usalama wa nishati ya Jordan kwa sababu ni chanzo salama, kinachozalishwa ndani ya nchi ambacho hakiathiriwi na uwezekano wa kupunguzwa kwa usambazaji wa gesi kutoka kwa umbile la Kizayuni, kama ilivyotokea wakati usambazaji wa gesi ulipositishwa kwa siku kadhaa baada ya vita vyake dhidi ya Gaza. Hata hivyo, ufisadi, mipango duni, mikataba mibovu, na utiifu wa kisiasa uliisukuma serikali ya Jordan kutafuta usuluhishi katika Chama cha Kimataifa cha Biashara jijini Paris.

- Mnamo 2016, makubaliano yalitiwa saini kati ya Kampuni ya Kitaifa ya Umeme ya Jordan, ambayo inamilikiwa kikamilifu na serikali, na kampuni ya Marekani (Israel) ya Noble Energy. Makubaliano hayo yanabainisha kuwa umbile la Kizayuni litaipatia Jordan gesi ya takriban mita za ujazo bilioni 45 katika kipindi cha miaka 15, kuanzia Januari 2020, badala ya dolari bilioni 10.

- Sababu iliyoifanya serikali kutumia usuluhishi ni kwamba mwaka 2020, iligundua kuwa Jordan ilikuwa na ziada ya uzalishaji wa umeme baada ya kutia saini makubaliano ya kufedhehesha na yaliyokataliwa sana ya kuingiza gesi kutoka kwa umbile linalokalia kwa mabavu la Kizayuni kwa dolari bilioni 15 kwa muda wa miaka kumi. Badala ya kufutilia mbali makubaliano ya gesi na mvamizi, serikali ilipendelea kuwasha mgogoro na China juu ya mradi wa Al-Attarat kwa kisingizio cha ukosefu wa haki. Zaidi ya hayo, ilizingatia uhakiki wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambao ulihusisha gharama za uzalishaji wa nishati na miradi ya uzalishaji, ukitaja hasa mradi wa mafuta ya shale.

- Imedhihirika kuwa makutano kati ya maslahi ya kiuchumi ya Jordan na China na utiifu wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi wa utawala wa Jordan kwa Marekani katika harakati zake za kuitawala kimataifa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vinavyokwamisha miradi ya China, hususan Mradi wa Al-Attarat. Hapo awali, serikali ilighairi mkataba na Huawei wa 5G kwa ajili ya Nokia na Ericsson kutokana na vitisho vya moja kwa moja vya Marekani.

- Katika mahojiano maalum na Arabi Post, Hossam Al-Abdullat, mkuu wa Shirika la Mabadiliko la Jordan aliangazia suala la uwajibikaji, akisema kuwa “faili la nishati na petroli nchini Jordan halijakamilika kabla ya kuidhinishwa kwanza na Mahakama ya Kifalme yenyewe, kupitia Idara ya Uchumi katika Mahakama, na inawasilishwa kwa Mfalme binafsi Baada ya hapo, serikali ya Jordan inafanya kazi juu ya utekelezaji wake.

- Ripoti moja ya shirika la habari la Associated Press mnamo Jumatano, Julai 5, 2023, yenye kichwa “Beijing Traps Amman in Debt,” ilizua taharuki kubwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mizozo ya kisheria kati ya Jordan na China kuhusu makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa Al-Attarat kiwanda cha nguvu za umeme, ambacho kinazalisha umeme kutoka kwa mafuta ya shale. Ripoti hiyo ilifichua kutofurahishwa na Marekani, huku David Schenker, aliyekuwa Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akisema, “Kwa kweli tulikuwa na wasiwasi kuhusu demokrasia, uwazi na ufisadi, lakini dola za kiimla zinaungana na China na kusogea karibu nayo.” Ripoti hiyo inahimiza kuendelea kwa makubaliano ya kuagiza gesi asilia kutoka kwa umbile la Kizayuni na kutawala kwake sekta ya nishati huku ikionyesha makubaliano ya ushirikiano wa Jordan na China kama “diplomasia ya mtego wa madeni,” lebo ambayo inafaa zaidi kwa Marekani.

- Ripoti ya Hali ya Nchi ya 2020 ya Baraza la Uchumi na Kijamii la Jordan, chombo cha kiserikali, ilisema: “Usalama wa nishati unaendelea kuyumba kati ya maamuzi ya kisiasa na kiuchumi. Kuingia kwa makubaliano ya gesi ya ‘Israel’, ingawa inaonekana kijuujuu kama sehemu ya vyanzo mbalimbali vya nishati, imedhoofisha usalama wa nishati kwa muda mrefu, na makubaliano ya gesi ya ‘Israel’ yana utata mkubwa wa vifaa, kiidara, na kifedha.”

- Ripoti ya Hali ya Nchi ya mwaka 2021 ya baraza hilo hilo ilisema: “Mradi wa uchomaji wa moja kwa moja wa mafuta ya shale wa Kampuni ya Al-Attarat unatekelezwa hivi sasa. Ni moja ya miradi ya kimkakati katika sekta ya nishati kutokana na matumizi yake ya vyanzo vya nishati.”

- Hatimaye, Waziri wa Nishati na Rasilimali za Madini, Mhandisi Saleh Kharabsheh, alitabiri kuwa hasara ya sekta ya umeme itafikia dinari bilioni kumi ifikapo 2030. Thamani ya uagizaji wa jenereta za nishati mwishoni mwa 2022 ilikuwa takriban dinari bilioni 3.5, huku serikali ikionyesha nia ndogo ya kuagiza gesi kutoka nchi za Ghuba tajiri ndani yake, kama vile Qatar, UAE, na Algeria, kwa bei za ushindani.

Huu ni mtazamo tu wa mgogoro wa nishati nchini Jordan na ufisadi na upotevu wa fedha unaohusishwa nayo. Yote haya yanatokana na misimamo ya kisiasa inayotumiwa na utawala huo katika kunyenyekea na kujisalimisha kwa wakoloni wa Magharibi, wakiongozwa na Marekani na Ulaya, pamoja na washirika wao, wanaompuuza Mwenyezi Mungu na maadili. Hizi ni pamoja na serikali na watu ambao wameuza maisha yao ya akhera kwa ajili ya faida za kidunia za watawala watiifu ambao hawamjali Mwenyezi Mungu wala maadili. Kutokana na hayo hapo juu, tunafafanua yafuatayo:

- Kiini cha tatizo kiko katika mfumo wa kisiasa na ukosefu kamili wa utashi wa kisiasa linapokuja suala la kutumia rasilimali za nchi, pamoja na kuakhirisha mambo, udanganyifu na ufisadi katika miradi ya kiuchumi ambayo inaweza kusaidia uchumi wa nchi.

- Mafuta ya Shale nchini Jordan ni mojawapo ya madini yasiyokwisha na ni mali ya umma kwa wananchi wote. Kwa hivyo, serikali haipaswi kutoa umiliki wake kwa watu binafsi au makampuni. Badala yake, ni lazima ichimbue madini hayo yenyewe kwa niaba ya Waislamu na kutunza mambo yao, na kila kinachochimbwa kimilikiwe kwa pamoja na wananchi wote.

- Dhurufu zinazowakabili watu wa Jordan wakati wa vita dhidi ya Gaza na Palestina - ambapo vikosi vya jeshi vinafungwa minyororo kutokana na kuwasaidia, na utawala huo unasimama pamoja na umbile la Kizayuni, ukitoa msaada wa uhai kupitia daraja la ardhini kwa ajili ya chakula na kuendelea na miradi yake ya kiuchumi pamoja nalo—ikiiweka Jordan na watu wake kwenye rehema ya adui katili na asiyejali. Adui huyu hata sita kukata umeme na maji katika vita vinavyoweza kutokea ikiwa mzozo huo utapanuka. Hali hii inalazimu upinzani mkubwa na wa dhati kwa yeyote anayefuja rasilimali za nchi na kufanya kazi kwa maslahi ya maadui zake.

- Ingawa watu wa Jordan, kwa uwezo wao wenyewe, wangeweza kuishi maisha bora ya kiuchumi kuliko hali mbaya ya sasa iliyosababishwa na utawala wa Jordan, suluhu ya mwisho ya migogoro inayoikabili Jordan na nchi nyingine ni kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Hii itazifanya ardhi hizi kuwa sehemu ya dola moja, kuunganisha rasilimali zao na kuzindua miradi ya kutumia nishati, inayofadhiliwa ndani bila utawala wa kigeni au deni. Khalifa atatawala kwa mfumo wa Kiislamu, pamoja na mfumo wa kiuchumi.

Enyi Waislamu wa Jordan: Mumefika kwenye kilele cha udhalilifu na fedheha, na utawala wa Jordan umewakandamiza sana. Unaiba riziki ya watoto wenu, unanyakua mali zenu, unapora mali zenu, na unakula njama dhidi ya Ummah wenu kwa manufaa ya umbile la Kizayuni na makafiri wa Magharibi, huku nyinyi mkiwa kimya, hamchukui hatua yoyote, ambayo inautia moyo tu katika dhulma yake na uonevu!

Enyi Waislamu wa Jordan: Hakuna wokovu kwenu kutoka katika hali yenu ya sasa isipokuwa kwa njia ya Khilafah. Ni amri ya Mola wenu Mlezi, chanzo cha utukufu wenu, mwenye kumshinda adui yenu, na mkombozi wa ardhi yenu. Ni Khilafah itakayolinda nchi yenu na rasilimali zake, na kulinda mali ya umma ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameifanya kuwa haki yenu.

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf:21]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu