- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Minbar ya Umma: Medali za Heshima!
Akitia taaliki ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali nchini Uturuki kwa kuhukumu ya kifungo cha miaka 52.5 kwa wazungumzaji wanne katika Kongamano la Khilafah lililopangwa kufanyika mnamo 2017 na ambalo lilipigwa marufuku bila sababu yoyote. Kongamano hilo lililopangwa kufanyika 5 Machi 2017, kwa anwani "Kwa nini ulimwengu unahitaji Khilafah?" Bila ya sababu yoyote ya kuingia akilini, kesi ya wazungumzaji katika kongamano hilo ambao ni: Mahmud Kar, Abdullah Imamoglu, Musa Beyoglu na Osman Yildiz.
Na katika kesi hiyo ambayo ilifanyika mnamo 11/27/2020 M mbele ya Mahakama Kuu ya Jinai ya Thalathini jijini Istanbul, mwendesha mashtaka ya umma aliomba jumla ya miaka 52.5 gerezani kwa mashababu hao wanne, kila mmoja wao kwa tuhma ya "kuwa msimamizi na mwanachama wa Hizb ut-Tahrir" na "kueneza propaganda ya Khilafah." Ombi la mwendesha mashtaka wa umma lilikutana na athari nyingi kutoka kwa sekta mbali mbali za jamii, ikiwemo wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, magazeti, tovuti, wanasheria na waandishi.
Jumatatu, 06 Jumada I 1442 H, sawia na 21 Disemba 2020 M
Kwa Maeleo Zaidi Bonyeza Hapa
Kumbuka: "Minbar ya Ummah" ni kituo maalumu kinachopeperusha rekodi zilizochaguliwa za Khilafah zilizoandaliwa na watoto wa Ummah wetu. Rekodi hizo hazikutolewa na Hizb ut Tahrir au vitengo vyake rasmi; bali ni rekodi kutoka kwa watoto wa Ummah wa Kiislamu; ambazo zinapeperushwa katika tovuti yetu ili kueneza kheri kwa ajili ya Uislamu na Waislamu.