بسم الله الرحمن الرحيم
Watawala wa Pakistan Wanawatoza Kodi Masikini na Wenye Madeni Bila ya Huruma ili Kujaza Mifuko ya Wale Wanaoendeleza Dhambi la Riba
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 11 Juni 2021, katika tangazo lao la bajeti, watawala wa Pakistan walifanya shangwe kubwa ya kupunguza ushuru kwa sekta fulani na kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa serikali. Halafu, ndani ya siku kadhaa, vinywa vya watawala vilifanya shangwe kubwa zaidi, kupitia kila jukwaa linalopatikana kwao.
Lakini, katika bajeti hiyo hiyo, watawala wa Pakistan waliongeza ushuru wa jumla hadi kiwango cha juu cha kihistoria cha karibu rupia trilioni sita, ambayo inamaanisha bajeti hiyo ni sawa na kuweka katika mfuko mmoja, na kisha kuchukua hata zaidi kutoka kwa mwengine. Kwa kuongezea, watawala wa Pakistan wanakusudia kuchukua ushuru kutoka kwa kila mtu bila kuzingatia Uislamu, ambao hauchukui mapato ya Zakah kutoka kwa masikini na wenye madeni, badala yake Zakah ni haki yao. Baya zaidi, watawala hawa watatumia zaidi ya rupia trilioni tatu kufanya malipo ya riba, licha ya kuwa riba ni dhambi kubwa katika Uislamu na tangazo la vita kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Hivyo basi mbwembwe hizo kubwa ni za nini?!
Badala ya kukataa kulipa riba ya rupia trilioni 3 kama Uislamu unavyoamuru, watawala wa Pakistan watachukua mikopo zaidi ya riba, kusaidia kulipia nakisi ya shirikisho ya trilioni 3.5. Kwa hivyo, serikali ya sasa inaizamisha Pakistan zaidi katika deni linalotokana na riba, kama ambavyo kila serikali ya zamani imefanya. Mnamo 1971, deni la Pakistan lilikuwa rupia bilioni 30, lakini kufikia 1991, liliongezeka hadi rupia bilioni 825. Kufikia mwaka wa 2011, deni la Pakistan liliongezeka hadi rupia trilioni 10 na sasa limeongezeka mara nne, likikaribia rupia 40 trilioni, miaka kumi tu baadaye! Hivyo basi mbwembwe hizo kubwa ni za nini?!
Baya zaidi, katika shangwe yao kubwa, watawala wa Pakistan kwa uwongo wanadai kwamba unafuu na utajiri uko karibu. Lakini, badala yake, watawala wa Pakistan wanashirikiana na IMF kuhakikisha kuwa uchumi unaojitahidi wa Pakistan unanyonywa damu yote, ili kujaza mifuko ya wale ambao wanaoendelea na dhambi kuu la riba. Ushuru ulikuwa zaidi ya rupia trilioni moja kwa mwaka wa kifedha wa 2008 - 2009, lakini baadaye uliongezeka mara mbili hadi zaidi ya trilioni mbili kwa 2013 - 2014. Kufikia 2018 - 2019, ushuru uliongezwa mara mbili tena kwa rupia trilioni nne, wakati watawala wa Pakistan sasa wanalenga karibu trilioni sita kwa 2021 - 2022. Hii ni huku wakijitahidi, kuanzia sasa, kukidhi mahitaji ya IMF ya ushuru wa rupia trilioni kumi, kwa mwaka wa fedha wa 2024 - 2025. Ikiwa ongezeko kama hilo la ushuru lingehakikisha kutetea heshima ya Mtume (saw), au kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa na Kashmir iliyokaliwa, Waislamu wa Pakistan wangetoa kila kitu majumba mwao na kufunga mawe matumboni mwao. Lakini, kufukuzana na maskini wetu na wenye deni bila huruma, ili kugharamikia juu ya dhambi kubwa, ni uhalifu wa kinyama ambao unapaswa kulaaniwa na kupingwa kila kona ya Pakistan! Hivyo basi mbwembwe hizo kubwa ni za nini?!
Baya zaidi bado, ni kuomba kulazimishwa kupitia janga linalozidi kuwa baya la deni la riba lililosababishwa na wao wenyewe, watawala kisha hujisalimisha kwa masharti angamivu ya IMF. Kutokana na masharti haya ya IMF ya kushusha thamani, wanadhoofisha sarafu yetu ili kuyafanya mahuruji yetu kuwa ya bei rahisi kwa dola za Kimagharibi kununua, huku maduhuli yakiwa ghali zaidi, na vilevile kila kitu nchini Pakistan, ikiwemo deni lake linalotokana na riba. Kwa hivyo, mnamo Januari 2001, Rupia 59 zilinunua dolari moja lakini mnamo Juni 2021, Rupia imedhoofishwa kwa kiwango ambacho Rupia 154 hununua dolari moja ya Amerika. IMF pia inalazimisha sharti la ubinafsishaji wa vyanzo vya mapato makubwa ya hazina ya serikali, kuhakikisha utegemezi endelevu wa mikopo ya riba. Hivyo basi, hazina ya serikali inanyimwa mapato makubwa kutoka kwa kawi, madini na utengenezaji wa kiwango kikubwa, ambao sasa hujaza mifuko ya wamiliki wa kibinafsi, wa ndani pamoja na wa kigeni.
Na kisha baada ya kutufukarisha vilivyo, watawala hawa wanasihi kuwa sisi ni masikini mno wa kuzuia matakwa ya wakoloni wa Kimagharibi juu ya Uislamu na matukufu yake!
Enyi Waislamu wa Pakistan!
Mwenyezi Mungu (swt) asema,
)وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى)
“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Surah Taha: 124]. Chini ya nidhamu iliyoko sasa ya kiuchumi ya kumuasi Mwenyezi Mungu (swt), hakutakuwa na mwisho wa mateso yetu na matatizo yetu. Hebu na tujitoeni kutokana na nidhamu hii katili, Enyi Waislamu, kupitia kufanya bidii kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.
Mwenyezi Mungu (swt) asema,
)وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَعْمَالُهُمْ كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّى إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئاً)
“Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji.” [An-Noor: 39]. Chini ya watawala walioko sasa, wanaofadhilisha maagizo ya makafiri waongo juu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), daima tubaki na njaa, huku tukilishwa ahadi za uongo za mwisho wa njaa yetu. Hebu na tujitoeni kutokana na watawala hawa wa fedheha na waovu, Enyi Waislamu, kwa kuwataka baba zetu, kaka zetu na watoto wetu katika vikosi vya jeshi kutoa Nusra yao kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena mara moja Khilafah kwa Njia ya Utume.
Ni Khilafah pekee ndiyo itakayomaliza uchukuaji bila huruma wa fedha kutoka kwa masikini wetu na wenye deni na kuzitumia kulipia malipo maovu ya riba. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayochukua viwango asili vya mikopo kutoka kwa mali ya maafisa na watawala wafisadi, kwani Uislamu unakataza utajiri wa ubadhirifu (ghalool). Kwa hivyo, Khilafah mwishowe italifunga jeraha lenye kuendelea, linalokua, linalotokwa na damu ubavuni mwa mwili wetu, ili tuweze kuelekeza nguvu zetu kikamilifu katika kujitahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw).
Ama kuhusu kuongeza mapato makubwa ya kutumia katika majukumu ya Uislamu, kama vile kuandaa majeshi yetu kwa Jihad dhidi ya maadui zetu au kuwaondolea masikini umaskini wao na wenye deni deni lao, Khilafah itafanya hivyo bila kuwabebesha mzigo maskini wetu na wenye deni. Khilafah itakusanya mapato makubwa kutoka kwa yenye uwezo wa kifedha, kama Kharaaj kutoka kwa wamiliki wa ardhi ya kilimo na Zakah kutoka kwa wamiliki wa bidhaa za biashara. Khilafah itakataza ubinafsishaji wa kawi na madini kwani katika Uislamu ni mali ya umma, ambayo mapato yake yanapaswa kutumiwa kwa mahitaji ya umma. Khilafah pia itaendesha vyema viwanda vizito vinavyomilikiwa na dola ili kuzalisha bidhaa zenye thamani kubwa, kama mashine za viwandani na magari, ikizalisha mapato makubwa kutoka kwa mauzo yake. Endapo mapato bado yanabaki kuwa na uhaba, Khilafah atatoza ushuru wa dharura kutoka kwa matajiri zaidi kati yetu.
Na Khilafah itamaliza udhoofishaji wa kuendelea kwa sarafu na utawala wa dolari, ambao umetuzamisha katika mafuriko ya mfumko wa bei. Khilafah itaifanya dhahabu na fedha kama msingi wa sarafu, kuhakikisha bei madhubuti, kama ilivyokuwa kwa karne nyingi chini ya Khilafah.
Kwa hivyo bado ingali haijakuwa wazi kwetu, Enyi Waislamu, kwamba hakuna chochote isipokuwa kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume (saw) ndiyo itakayokomesha uchungu wetu wa kiuchumi wa kudumu?! Mwenyezi Mungu (swt) asema,
(أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ) “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” [Surah al-Mulk 67:14].
#KhilafahEndsSlaveryToIMF
H. 3 Dhu al-Qi'dah 1442
M. : Jumatatu, 14 Juni 2021
Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan